Zamaradi Mketema ameachana na Wasafi Media?

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Mtangazaji wa zamani wa Clouds Media Group, Zamaradi Mketema ambaye baada ya kuvunjika kwa mahusiano yake ya kimapenzi na Mkurugenzi wa CMG, Ruge Mutahaba, alihamia Wasafi Media kuendelea na career yake.

Baada ya uzinduzi rasmi wa Wasafi TV na Wasafi FM, ilitarajiwa mtangazaji huyu mahiri kuanza kuonekana kwenye runinga akiendesha kwa mafanikio kipindi kama alivyokuwa akifanya Take One na kituo chake cha kazi cha zamani.

Tofauti na matarajio ya wengi, ghafla mwanadada Zamaradi ameanza kujiondoa kushiriki kwenye kazi zote zinazohusiana na Wasafi pengine kabla hata ya kuanza. Na kwa tukio la hivi karibuni la Wasafi Festival, hakuonekana kuongelea chochote kama ilivyo ada kwenye projects nyingine za Mwajiri wake huyo mpya.

Sasa, kwa sababu bado hakujatoka official say, naomba kupitia uzi huu tukajaribu kudodosa endapo kuna lolote linaloendelea linalopelekea awe kimya kabisa huku akionekana kuwa busy na shughuli zake nyingine.

Maswali ya shauku;

1. Mgongano wa kimaslahi na kukomoana baina ya Wasafi Media na Clouds Media umemweka njia panda?
2. Hali ya Afya ya mzazi mwenzie (Ruge) imemfanya ashindwe kuvumilia kuhimili vishindo vya kejeli kutoka kwa wanaofurahia anguko lake?
3. Ameshindwana malipo na Wasafi Media?
4. Anaamua kuwa freelancer?
5. Ana mpango wa kurudi Clouds Media Group?

Hayo ni miongoni mwa maswali yanayoweza kutupatia majibu. Na yeye mwenyewe anaweza kuja hapa kuliongelea suala hili ili kuondoa sintofahamu kwa wapenzi wa kazi zake.
 
Ongeza na lile SAKATA LAKE NA MAMA DEEDYLAN KWENYE MSHONO WA NGUO.Alipata tabu saana,na style yake ya kujaza andiko instagram.
 
Heshimu ulikotoka kwani siku zote pale Juu ulipo Leo ulipita chini kwanza na pale chini ndipo palipokusaidia kufika Juu hata kama hutapapenda pale chini ndio moja ya msingi uliokushikilia huko Juu kumbuka kupaheshimu chini ili uwe Juu. Kutoka Juu ni rahisi kuliko kupanda UFA Tu wa chini utakusababisha kushuka chini kwa haraka sana. Jifunze kuheshimu ulikotoka.

Naona kakumbuka huu msemo baada ya kuona child support inakaribia kuyeyuka,daah kama sio yeye aliyevujisha ile clip ya ruge akimlilia
 
Back
Top Bottom