Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Hiyo haizuii kuchepuka, bora angetoa sadaka hiyo hela. Kafanya ujing wa kiwango cha juu
Mtangazaji Zamaradi Mketema ametrend sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kukodi Bango na kuweka ujumbe wa mahaba kwa mume wake kama zawadi ya siku ya valentines.

Bango hilo liko maeneo ya Morocco Dar es Salaam ambayo ni barabara anayopita mumewe kila siku.

View attachment 2118894

Zama amesema kuwa mumewe Bwana Shabani alifurahi sana alipompeleka eneo la tukio hadi machozi kumtoka.

View attachment 2118895

Bango hilo litakaa kwa muda wa mwezi mzima.

Note: Madanga ya shemeji yetu yajipange pamoja na mke mkubwa (kama yupo) mwenzao kawazidi kete bango kuubwa kama tangazo la Condomu.
 
Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza....
Mapenzi ya kuutangazia ulimwengu si mapenzi ni maigizo
Mwanamke utaijenga nyumba kwa mikono yako na mikono yako itaibomoa nyumba... kumuweka mtu hadharani ni kwa ajili ya biashara sana sana sasa huyu amekuwa bidhaa
Lakini inategemea uzuri na ubovu wa bidhaa kupata wateja..
Ni kukosa uelewa na ni zaidi ya ushamba na ujinga
Sura sura jamani khe! Aibu unaona we mwingine
 
Back
Top Bottom