Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Ninavyoisoma picha:-
1. Bwana yuko na hostility and very passive.
2. Mioyo yao haina connections hatakidogo.
3. Hiyo ndoa mama ndiye anaithamini zaidi, wakati upande wa pili ukiwa full irresponsible.
4. Hiyo sura ya mshangao kwa baba ni kwa drama lakini moyo wake wala hauko hapo.
5. Analazimisha kufurahi lakini he seems not to wish, hii ingetokea.
6. Analia kwa kushindwa kubeba deni analopowa na mke wake, kwa sababu hawezi kubadilika na kufanya anachotaka mama.
7. Mjukuu wangu wa kiume haonyeshi huba, lolote kwa mke wake. Ama hayuko romantic na kwamba anategemea kuwa provoked na mke wake ili angalau achangamkie love.
8. Mwanamme anaonekana kuwa na majuto makubwa sana ndani ya huo uhusiano.
9. Mama anajua yote nilyoyasema na zaidi ya hayoe mengine siwezi kuyaandika mtandaoni kwa heshima ya ubinadamu wa wahusika.
10. Anajua anaupinzani mkali lakini ameamua kulinda mhusiano yake kwa uvumilivu na gharama kubwa kwa sababu anaepusha madhara kujirudia.
11. Mama anatunza mahusiano kwa kulinda hadhi yake katika jamii na familia yake.
12. Anajua anapitika vipindi vigumu sana katka mahusiano yake lakini ameamua kujitoa dhabihu kwa hehsima yake na ama watoto au watu wanaomtegemea.
13. Mama kisaikolojia anajitegemea 14wala hategemei chochote kikubwa kutoka kwa huyo jamaa ambaye moyo wake uko mbali, isipokuwa jina na kulinda aibu yake.
14. Hiyo picha hajapeleka ili kuonyesha namna gani anampenda mme, wake bali ni kuwathibitishia wapinzani wake kwamba yeye zaidi, na kutaka kumrejesha mme wake pengine akiona kama anajali, ataplay nafasi yake.
15. Mwanammen anadeka lakini pia hana hakika na uaminifu wa mke wake.
16. Mama anajitahidi kuonyehs moyo wake kwamba ni mweupe na sababu yoyote anayotumia yule baba kujustify, kutokuwa naye ki-moyo, si ya kweli.

Ninaona mengi sana kwenye hii picha lakini ujumbe wangu.
Naona naanza kupata hasira, acha niishie hapa. lakini hii siyo tangazo la furaha katika mahusiano wala tangazo la upendo, bali ni sauti ya mwanamke, baada ya kulia sana katika utumwa wa mapenzi, sasa anakata rufaa kwenye mahakama iitwayo dunia. Dunia ione, dunia iwe shahidi, dunia isuluhishe, dunia ifurahi, dunia icheke, dunia ijifunze, iamue na lolote litakaloendelea, baada ya hapa, "mama kanawa", ingawa kwa huzuni kubwa.

Wanawake acheni kuolewa na wanaume wasioonyesha kuwapenda, haijalishi umepitia mahusiano mangapi, haijalishi watu watakuonaje, lakini afadhali kuchelewa na kupata mme atakayekupenda na kujali upendo wako, kuliko kuwa mtumwa wa mapenzi na mwanamme asiyejali thamani yako. Matokeo yake ndiyo haya.

BANGO LIKO KWENYE PUBLIC DOMAIN, NA NDIYO NGUVU YANGU YA KUANDIKA NILIYOYAONA KWENYE PICHA ILE.
Mkuu umeandika kwa hisia saaaana hii comment daaaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale wenye wapenzi wanaotembea kwa miguu aka TZ 11 ,sio mbaya mkabandika picha hata za black and white kwenye njia wanazopita unahakikisha ile mistimu au minazi iliyokuwa njiani unabandika picha yake.

Mimi wangu ameniambia nitembelee bango lilopo kwa m/kiti wa serikali ya mtaa au kwa mjumbe wetu nitajiona.
 
Narudia

KAMA HUMFIKISHI KILELENI kiasi aka Squirt KAMWE USITEGEMEE KUPENDWA.

OVA
 
!
20220114_054121.jpg
 
Dia wewe unaweza mtundika mmeo bangoni? Kimbuka adui wa mme ni rafiki zako siku moja watakuonesha kuwa kumtundika bangoni sio kupendwa
Mimi sio mtu wa drama namna hiyo...Haki siweziiii hata dunia igeuke siweziiiii ...We ngoja atakomeshwa na wenzie
 
[emoji16][emoji16][emoji16] mie ni panick kisa gani? kila mtu aishi namna anavotaka. Nyie mnamuona ana unafki mnaongea mawazo yenu ambayo sio lazima iwe ndo uhalisia. Kila mtu anafanya kitu kinachompa furaha yeye binafsi afterall mapenzi hayanaga kanuni.
Sawa na ule ujinga wanawake wanaambiwa kwamba mwanaume akikasirika usimjibu. Kwa wanaume wengine akiongea af ukakaa kimya anaona una kiburi hapo ndo unaharibu zaidi.
So jifunzeni kuishi mnavyotaka kulingana na aina ya mtu mlienae. Period.
dada kaona mume wake anapenda nini kampa anachopenda af nyie ndo mnateseka[emoji16][emoji16][emoji16]
Tuteseke sisi kisa bango?hebu kuwa mkubwa kwanza ndio urudi tuzungumze....maana naona unapanic panic tu
 
Mtangazaji Zamaradi Mketema ametrend sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kukodi Bango na kuweka ujumbe wa mahaba kwa mume wake kama zawadi ya siku ya valentines.

Bango hilo liko maeneo ya Morocco Dar es Salaam ambayo ni barabara anayopita mumewe kila siku.

View attachment 2118894

Zama amesema kuwa mumewe Bwana Shabani alifurahi sana alipompeleka eneo la tukio hadi machozi kumtoka.

View attachment 2118895

Bango hilo litakaa kwa muda wa mwezi mzima.

Note: Madanga ya shemeji yetu yajipange pamoja na mke mkubwa (kama yupo) mwenzao kawazidi kete bango kuubwa kama tangazo la Condomu.
Acha ibaki hivyo. Tuone
 
Back
Top Bottom