Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Ni wivi tu na roho mbaya.

Angefanya mzungu hapo ingekua sawa ila kwa kua ni Mtanzania wanaona eti ulimbukeni...
wote wanaoponda ni hawa👇
FB_IMG_16443501117756787.jpg
 
Hapo zamaradi anaona kama amemuonesha upendo mume wake kumbe ndio anaipalilia makaa ndoa yake.

Kwanini nasema hivi? Siku zote wanawake hawapendani. Mwanamke anaweza akawa na rafiki mwenzake wa kike na kila jambo kuhusu mahusiano yake anamuweka wazi shosti yake lkn utashangaa shosti anamzunguka na kumuibia bwana.

Kumuweka kwenye bango kumewapa "alert" mashosti na wanawake wengine kuhisi Zamaradi anaishi maisha ya raha wkt wao kutwa kucha wanateseka na ndoa. HAWATOFURAHI. Mwisho wa siku watakimbizana kwa huyo jamaa na kumpa mitego ya kila aina na sidhani kama ataweza kuikwepa na mwisho atamsaliti na upendo walioujenga kwa miaka zaidi ya mitano kuisha na kuishia kupost status za kinyonge kutuita wanaume wote ma mbwa...

Haya mambo ya kuonyesha jamii umezama sana kwenye huba tuwaachie wenzetu. Huwa nawaheshimu sana wanaopendana kwa dhati na kuishi private life.

Anyways kupanga ni kuchagua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanasema bora Wali Dagaa kuliko walimwengu..
Ni wachache wanapenda kusikia furaha na mafanikio yako..
Kupitia hili bango,ajiandae kisaikolojia mme wake kusumbuliwa na wasio mtakia mema,just for the sake ya kumkomoa..


Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Mtangazaji Zamaradi Mketema ametrend sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kukodi Bango na kuweka ujumbe wa mahaba kwa mume wake kama zawadi ya siku ya valentines.

Bango hilo liko maeneo ya Morocco Dar es Salaam ambayo ni barabara anayopita mumewe kila siku.

View attachment 2118894

Zama amesema kuwa mumewe Bwana Shabani alifurahi sana alipompeleka eneo la tukio hadi machozi kumtoka.

View attachment 2118895

Bango hilo litakaa kwa muda wa mwezi mzima.

Note: Madanga ya shemeji yetu yajipange pamoja na mke mkubwa (kama yupo) mwenzao kawazidi kete bango kuubwa kama tangazo la Condomu.


Mtangazaji Zamaradi Mketema ametrend sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kukodi Bango na kuweka ujumbe wa mahaba kwa mume wake kama zawadi ya siku ya valentines.

Bango hilo liko maeneo ya Morocco Dar es Salaam ambayo ni barabara anayopita mumewe kila siku.

View attachment 2118894

Zama amesema kuwa mumewe Bwana Shabani alifurahi sana alipompeleka eneo la tukio hadi machozi kumtoka.

View attachment 2118895

Bango hilo litakaa kwa muda wa mwezi mzima.

Note: Madanga ya shemeji yetu yajipange pamoja na mke mkubwa (kama yupo) mwenzao kawazidi kete bango kuubwa kama tangazo la Condomu.
Ninavyoisoma picha:-
1. Bwana is hostile and very passive.
2. Mioyo yao haina connections hata kidogo.
3. Hiyo ndoa mama ndiye anaithamini zaidi, huku upande wa pili ukiwa full irresponsible.
4. Hiyo sura ya mshangao kwa baba ni drama . Moyo wake wala hauko hapo.
5. Analazimisha kuonyesha furaha lakini kiuhalisia wala hana mpango na anaonekana hajali wala hakutaka hii itokee.
6. Kwa namna wanavyoishi na watu wao wa karibu wanavyowafahamu, bwana anaona kama embarassment.
7. Analia kwa kushindwa kubeba deni analopewa na mama, kwa sababu anajua hawezi kubadilika na kufanya anachotaka mama.
8. Mjukuu wangu wa kiume haonyeshi huba, lolote kwa mke wake. Ama hayuko romantic na kwamba anaonekana ni mtu wa kuwa provoked na mke wake ili angalau achangamke.
9. Mwanamme anaonekana kuwa na majuto makubwa sana ndani ya huo uhusiano.
10. Mama anajua yote niliyoyasema na zaidi ya haya. Mengine siwezi kuyaandika mtandaoni kwa heshima ya ubinadamu wa wahusika.
11. Mama anajua ana upinzani mkali sana katika hayo mahusiano, lakini ameamua kuyalinda kwa uvumilivu na gharama kubwa ili kuepusha madhara kujirudia.
12. Mama anatunza mahusiano kwa kulinda hadhi yake katika jamii na familia yake.
13. Anajua anapita katika vipindi vigumu sana katka mahusiano yale lakini ameamua kujitoa dhabihu kwa hehsima yake na ama watoto au watu wanaomtegemea.
14. Mama kisaikolojia anajitegemea wala hategemei chochote kikubwa kutoka kwa huyo jamaa ambaye moyo wake uko mbali, isipokuwa jina ili kuepuka aibu.
15. Hiyo picha hajapeleka ili kuonyesha namna gani anampenda mme, wake bali ni kuwathibitishia wapinzani wake kwamba yeye zaidi, na kutaka kumrejesha moyo wa mmewe kwa kudhani kwamba pengine kwa tukio hilo, ataona mama anajali na huenda atarejesha moyo na kuplay nafasi yake.
16. Mwanamme anaonekana anadeka lakini pia hana hakika na uaminifu wa mke wake.
17. Mama anajitahidi kuonyesha weupe wa moyo ili kumfanya bwana yule kuona kwamba tuhuma anazotumia kujustify umbali wake katika mahusiano si za kweli.
18. Mama ana IQ kubwa kubwa but lonely, wakati baba ana IQ ya chini na ndiyo sababu anaonekana kuishi kwa kufuata upepo wa mitazamo ya watu wengine, bila juhudi zake za kuelewa na kupima kwa usahihih kabla ya kuamua. Actually anaamuliwa na yeye anapata amani ya kutii maamuzi ya watu wa nje over his wife.

Ninaona mengi sana katika picha ile hadi naanza kupata hasira, acha niishie hapa.
Lakini hii siyo tangazo la furaha katika mahusiano wala tangazo la upendo, bali ni sauti ya mwanamke, baada ya kulia sana katika utumwa wa mapenzi, kujitoa na kufanya mengi makubwa kwa kujipendekeza ili akubalike, bila mafanikio, sasa anakata rufaa kwenye mahakama iitwayo dunia. Dunia ione, dunia iwe shahidi, dunia isuluhishe, dunia ifurahi, dunia icheke, dunia ijifunze, iamue na kwa lolote litakaloendelea, baada ya hapa, "mama kanawa", ingawa kwa huzuni kubwa.

Wanawake acheni kuolewa na wanaume wasioonyesha kuwapenda, haijalishi umepitia mahusiano mangapi, haijalishi watu watakuonaje, lakini afadhali kuchelewa na kupata mme atakayekupenda na kujali upendo wako, kuliko kuwa mtumwa wa mapenzi na mwanamme asiyejali thamani yako. Matokeo yake ndiyo haya.

BANGO LIKO KWENYE PUBLIC DOMAIN, NA NDIYO NGUVU YANGU YA KUANDIKA NILIYOYAONA KWENYE PICHA ILE.
 
Back
Top Bottom