Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania kwa hofu ya kuenea kwa COVID-19

Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania kwa hofu ya kuenea kwa COVID-19

Pesa tunazotafuta kama nchi mwisho wa siku hatutozipata.

Wakati wenzetu wamemaliza corona, sisi tutakuwa bado na maambukizi, watatublock kila nchi duniani, tutabaki kama kisiwa kidogo
Corona si ya kuisha leo au kesho hii. zungumzia habari ya chanjo ikitoka.
 
Jamani sasa hawa Wazambia mbona wanataka kuwatesa Wakongo
 
Sasa sisi watanzania tunaadhirika vipi.mi naona wao ndio wataumia.sisi ahh tunawatazama wao
Tutaathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya sababu ya nchi yetu kugoma kufunga mipaka yake katika kipindi hiki ni kukwepa athari ya kiuchumi. Sasa wale tunaoona ni wateja wetu nje ya mipaka ya nchi yetu wameanza kugomea huduma zetu! Mteja akisusa, utamhudumia nani? Diplomasia zaidi inahitajika juu ya suala hili la Covid-19.
 
Pesa tunazotafuta kama nchi mwisho wa siku hatutozipata.

Wakati wenzetu wamemaliza corona, sisi tutakuwa bado na maambukizi, watatublock kila nchi duniani, tutabaki kama kisiwa kidogo
Natamani mganga wa kienyeji aisome hii comment yako Mkuu pengine atafanya maauzi yenye busara
 
Vitaa za madereva wa Tanzania na Zambia hizo. Naona serikali ya Zambia imeingia kichwa kichwa kwenye mzozo na kuwapa back up raia wake (Madereva). Wanataka madereva wa Zambia ndio waendeshe hizo gari za IT kutoka Boda kuingia Zambia. Wakati mkataba wa kutoa gari ya IT unamtaka dereva aitoe gari Dar port hadi Zambia. Bifu ndio iko hapo.
Shida covid 19 braza. Usitafute mchawi. Fungeni milango hao hao wanakuja.
 
Kufuatia maelekezo ya SADC kuwa Corona inasambazwa na safari za ndani ya nchi, kati ya nchi moja na nyingine, na kwamba inashauri safari za aina hiyo zisitishwe, Zambia imeamua kufunga mpaka na Tanzania. Zambia imetoa sababu kuwa kutokana na kuongezeka kwa visa vya korona nchini Tanzania basi imeamua kufunga mpaka wake na Tanzania.

Naona Wazambia wameweka mbeke afya za watu wao badala ya pesa.

Hii ni meseji kwa nchi yetu kuwa wenzetu wanatuona hatuko serious vya kutosha namna tunavyoendesha vita vyetu juu ya ugonjwa huu.

Wakati huohuo Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwa wale walioumwa Corona wakapona hawawezi kuumwa tena, taarifa hii ni pigo kwa wale wasiochukua hatua za kutosha kupambana na ugonjwa huu wakiamini eti wakiugua watu wengi wakapona basi kinga ya jumuia itapatikana baada ya miili kujenga natural immunity. Tahadhari hii ni muhimu maana tukiendelea kutochukua tahadhari za kutosha na kirusi kusambaa nchi nzima hiyo kinga ya jumuia inaweza isipatikane na nchi nzima ikaangamia kwa mamilioni ya vifo

IMG_20200425_204602.jpg
 
Back
Top Bottom