Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania kwa hofu ya kuenea kwa COVID-19

Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania kwa hofu ya kuenea kwa COVID-19

Who will bleach...
Who will breach...

That letter is possibly fake just by that error of one letter.
 
Kuna nchi zitawataadharisha wananchi wao wasije Tanzania kutalii, apo ndo jiwe ataelewa Kuna watu wako serious
 
Ninavyomjua Jiwe atampigia simu Lungu kumsihi afungue mpaka na kuonesha mbele ya vyombo vya habari kuwa Zambia haina nia ya kufunga mpaka wake na Tanzanzania bali tangazo hilo lilitolewa na wahuni kwa nia ya kuharibu uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo.
 
Wabongo ni wavivu balaa, yaani mijamaa badala ya kupiga kazi inawaza ilale ndani..

nchi zote walio kaa ndani wataondoa hiyo lockdown yao tu hakuna namna, ujerumani wanaforce shule zifunguliwe mwezi huu kama siyo week hii
Kwani Nani alikuambia lockdown itakaa milele
 
Mbona hicho kinachotaka kufanywa na Zambia kinaelekeana na moja ya options anazozifikiria Museveni? Museveni amesema kuwa option mojawapo anayoifikiria ni madereva wa malori toka Tanzania waishie pale mpakani. Toka mpakani malori yaendeshwe na Waganda kuingia ndani ya Uganda. Hivyo wasafirishaji watatakiwa kuwa na madereva wawili, mmoja wa kuwepo Tanzania, na mwingine ndani ya Uganda.

Option ya pili wapimwe mpakani halafu waruhusiwe kuendelea ndani ya Uganda lakini wasichangamane na yeyote, waende mpka kituo kitakachokuwa kimepangwa, wasubirie majibu. Ukiwa positive, unaishia hapo hapo. Ukiwa negative, unaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msiwe mnaimba tu kama kasuku. Ni US ya wapi imeondoa lockdown?

Kuna States chache sana, nadhani 5 tu ambazo wanafikiria kupunguza kiwango cha lockdown na siyo kuondoa kabisa. Katika States hizo, shughuli chache sana wanataka ziruhusiwe kuendelea.

Hata hivyo white House imeweka vigezo vya State kuruhusiwa kuondoa lockdown, na kigezo kikuu ni kwamba cases za maambukizi ni vifo viwe vinapungua mfululizo kwa wiki 2. Mpaka sasa hakuna State ambayo imetimiza sharti hilo.

Watu sijui wanaokota wapi hizi habari kwamba US imeondoa lockdown! Mtu hajui chochote, lakini anataka kuonesha anajua kwa kuwadanganya watu.

Soma hapa kuweza kujua masharti ya kuondoa lockdown US
US states weeks away from being able to lift lockdowns, model shows


Sent using Jamii Forums mobile app
Achana na hao kunguni watakuchosha tu bure hawana chochote wanachokijua
 
Japo Watz hulia sana dhidi ya Kenya, lakini naona wamefungiwa na majirani wote hadi wale wao huwaita ndugu wa damu kule SADC, hii yote imetokana na kukaidi kwao kuchukua tahadhari na kuendelea kushupaza shingo huku wakishikilia mambo yasiyo na misingi ya kisayansi, ndugu zetu mtaendelea kutengwa sana kwenye hili la kuogelea ndani ya kirusi huku mkikaidi taratibu zilizoshauriwa na wataalam duniani.
WHO wamewasema sana kwa hili la ukaidi.....

2379433_0055BF42-3858-43EC-85A6-C1EF1F8CD16A.jpeg

Acha watutenge hawa ila sisi tukiwatenga nao watalia na kusaga meno, ila sisi tutapona kabla yao maana maabukizi yanatoka kwao kuja kwetu kwa hiyo wakijitenga sisi tutabaki kutibu masalia tu.
 
Hii ngoma niyazungu,MUNGU ameamua kuonyesha utukufu wake,angalia wazungu wanavyo teseka,sisi hatuna uwezo wa kujikinga au kuwa makini Kama wazungu,lkn kitu bado kimekomaa nao tuu,eti nchi za kiafrica zinaweza kujilockdown!eti Kenya lockdown ni usiku tuu machana watu wanatembea,(maajabu) Italia waliamua ku unlockdown baada ya kuona uchumi unaelekea kukwama,MUNGU angetuletea kitu original Kama cha marekani mbona tungeisha wafrica wote..MUNGU MUUMBA MBINGU NA ARDHI ANDELEA KUTULINDA(AMINA)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo ni wavivu balaa, yaani mijamaa badala ya kupiga kazi inawaza ilale ndani..

nchi zote walio kaa ndani wataondoa hiyo lockdown yao tu hakuna namna, ujerumani wanaforce shule zifunguliwe mwezi huu kama siyo week hii
Plan ya kuondoa Lockdown ilikuwepo wakati wanaweka Lockdown, aim ilikuwa kuflatten curve ya maambukizi halafu wana ease Lockdown.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitaa za madereva wa Tanzania na Zambia hizo. Naona serikali ya Zambia imeingia kichwa kichwa kwenye mzozo na kuwapa back up raia wake (Madereva). Wanataka madereva wa Zambia ndio waendeshe hizo gari za IT kutoka Boda kuingia Zambia. Wakati mkataba wa kutoa gari ya IT unamtaka dereva aitoe gari Dar port hadi Zambia. Bifu ndio iko hapo.
Out of order soma vizuri hiyo barua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pesa tunazotafuta kama nchi mwisho wa siku hatutozipata.

Wakati wenzetu wamemaliza corona, sisi tutakuwa bado na maambukizi, watatublock kila nchi duniani, tutabaki kama kisiwa kidogo
Wenzetu wakimaliza corona? Duuh! Hivi mkuu hukuwahi kujiuliza kwa nini nchi kubwa za dunia ya kwanza zilishindwa kuzuia ugonjwa huu usingie kwao then wakasubiri uingie ndio wafungie watu ndani?

Amini amini nakuambia kama corona itaisha Zambia, Kenya, Burundi, Rwanda nk na Tanzania pia itaisha. Kama ambavyo ilivyoanza China hakuna aliyeweza kuizuia isiingie nchini kwake vivyo hivyo hakuna atayeweza kuzuia corona ishishe Tanzania wakati dunia nzima imeisha.

Ni Mungu pekee ndio mwenye kujua corona itaisha lini duniani. Hata sasa njia tunazotumia kuudhibiti huu ugonjwa kisayansi tunaita trial and error, hakuna mwenye huwakika na njia yake, ndio maana kuna wengine hufanya total lockdown wengine partial lockdown, wengine wameanza kufuta lockdown na wengine hawakufanya lockdown kabisa. Wote hawa wanaweza kuwa sahihi kwa namna moja ama nyingine maana hakuna mwenye huwakika na njia yake.
 
Tutaathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya sababu ya nchi yetu kugoma kufunga mipaka yake katika kipindi hiki ni kukwepa athari ya kiuchumi. Sasa wale tunaoona ni wateja wetu nje ya mipaka ya nchi yetu wameanza kugomea huduma zetu! Mteja akisusa, utamhudumia nani? Diplomasia zaidi inahitajika juu ya suala hili la Covid-19.
Hata hili litapita kama Ebola
 
Back
Top Bottom