Kaka umeeleza vizuri but kwa muktadha wa tunacho kijadiri, je serikali iingilie kati kuhusu malori ya Zambia kwenye bandari yetu? Nadhani (kwa mtazamo wangu ) hili sio sahihi, serikali ihakikishe bandari yetu inaendelea kupendwa na nchi jirani ziendelee kuitumia Dar port then hayo masuala ya gari za wapi zichukue mzigo liwe jukumu la sekta binafsi kuhakikisha linatoa huduma za uhakika ili wafanyabiashara wa nchi nyingine wapende vya kwetu; Unajua hata Kagame aliweza kutunga sheria za namna hiyo kama Zambia, huoni pia kuna Azam Rwanda? Kuna malori kibao ya Azam yenye plates number za Rwanda na sio Bongo, ni hivo hivo.
Kutokua na Amani Msumbuji (sio kitu kizuri anyway) ni fursa kwetu, tuitumie vizuri, ndicho ambacho USA ilikitumia na inakitumia hadi sasa and i think hata ustawi wa Israel hutegemea sana AMANI ya mataifa ya Kiarabu ya pale mashariki ya kati, yakiwa na amani halafu wakawa wanafanya na vikao vyao vya OPEC vizuri then stability ya Israel hua inakua very poor, wakianza maujinga yao ya kupigana pigana na kutokuamina kama ilivyo sasa, Israel huaga inastawi sana. Ni hayo tu, nina heshimu sana mchango wako kwa uzi hu.