Zambia yalalamikiwa kwa kujimilikisha kazi ya kubeba Mizigo Bandari ya Dar es Salaam

Zambia yalalamikiwa kwa kujimilikisha kazi ya kubeba Mizigo Bandari ya Dar es Salaam

Waanzishe road toll kwa magari ya kigeni
... unapozungumzia magari ya kigeni utawaathiri hata wasiohusika, wasio na sheria ya hovyo kama hiyo ya Zambia. Kuanzia DRC, Burundi, Malawi, Rwanda, Zimbabwe, etc. waathirike na road toll kwa sababu ya Zambia?
 
2 Apr 2021
Lusaka ,Zambia

OMCAZ Happy With Government’s Stance Against Erring Oil Marketing Companies

The Oil Marketing Companies Association of Zambia-OMCAZ has supported government’s stance against erring Oil Marketing Companies.

Government has warned to revoke licenses of Oil Marketing Companies-OMCs refusing to sub-contract local transporters in line with the provisions of the tax waiver on importation of finished petroleum products.

On Wednesday, local oil tanker drivers staged a protest against some OMC’s defying tax waiver conditions whose Statutory Instrument provides for the allocation of 50 percent transportation of oil, in the Country, to local transporters.
 
Hapa tunafanya upembuzi yakinifu wa Geopolitics.

Beira ilikumbwa na tufani kali toka baharini na miundo mbinu kuharibiwa. Waasi wa Kaskazini mwa Mozambique wanaendelea kuwa tishio kwa miundo-mbinu na usalama maeneo ya majimbo ya Kaskazini na ya kati ya Mozambique.

Nchi jirani ya Mozambique imeshindwa kutoa uhakikisho kwa wawekezaji wake usalama na ulinzi kutokana na majeshi ya usalama ya Mozambique kupenda rushwa, kukosa morali ya kupigana na waasi, kuuza silaha kwa waasi.

Na nchi hiyo ya Mozambique kuendeshwa kikanda mfano viongozi wa juu kutoka kaskazini ya Mozambique hawana utashi kuhakikisha tishio la waasi kaskazini likiisha kwani kwanza waasi ni ndugu zao, pili kwamekashimisha majeshi ya kampuni binafsi "wapambane" na waasi ili makampuni hayo yatoe rushwa kwa viongozi wa serikali ya Mozambique.

Kifupi mikutano hii ya dharura ya troika huko Mozambique inazungumzia hatari iliyopo inayotishia uchumi na usafiri wa eneo hilo la kati ya Mozambique na kaskazini ya Mozambique.

Tanzania itumie geopolitics yake vizuri kuwabana hawa wenzetu wa Zambia kuwa warudi mezani kwa manufaa yao.

Tatu ushawishi wa Tanzania kwa nchi za Kusini ya Afrika ni mkubwa kuliko "lugha ya kiswahili ya Palamagamba", hapa diplomasia ya kiuchumi itumike ipasavyo kwa lugha mama ya Diplomasia ya Kimataifa ambayo ni Kiingereza kukumbushia maagano, mapatano, maazimio na protokali zote za SADC juu ya kuwepo biashara huria huru miongoni mwa nchi wanachama zizingatiwe na kuwa sheria mbaya hii ya Zambia imekiuka na kukengeuka matumaini ya uwepo wa SADC imara.
Kaka umeeleza vizuri but kwa muktadha wa tunacho kijadiri, je serikali iingilie kati kuhusu malori ya Zambia kwenye bandari yetu? Nadhani (kwa mtazamo wangu ) hili sio sahihi, serikali ihakikishe bandari yetu inaendelea kupendwa na nchi jirani ziendelee kuitumia Dar port then hayo masuala ya gari za wapi zichukue mzigo liwe jukumu la sekta binafsi kuhakikisha linatoa huduma za uhakika ili wafanyabiashara wa nchi nyingine wapende vya kwetu; Unajua hata Kagame aliweza kutunga sheria za namna hiyo kama Zambia, huoni pia kuna Azam Rwanda? Kuna malori kibao ya Azam yenye plates number za Rwanda na sio Bongo, ni hivo hivo.
Kutokua na Amani Msumbuji (sio kitu kizuri anyway) ni fursa kwetu, tuitumie vizuri, ndicho ambacho USA ilikitumia na inakitumia hadi sasa and i think hata ustawi wa Israel hutegemea sana AMANI ya mataifa ya Kiarabu ya pale mashariki ya kati, yakiwa na amani halafu wakawa wanafanya na vikao vyao vya OPEC vizuri then stability ya Israel hua inakua very poor, wakianza maujinga yao ya kupigana pigana na kutokuamina kama ilivyo sasa, Israel huaga inastawi sana. Ni hayo tu, nina heshimu sana mchango wako kwa uzi hu.
 
Ni serikali yetu Tanzania ikae na wamiliki wa malori Tanzania TATOA kuona itafanyaje, tumeona ushaidi serikali ya Zambia imekaa vikao na madereva wa malori na sekta ya usambazaji mafuta OMC ili kuweka utaratibu wao wa kujaribu kutatua changamoto kwa haraka na uwazi.
 
Hii inaweza kujibiwa na reciprocal action, hiyo mizigo ikivuka mpaka kuja tz ichukuliwe na wa tz ktk ratio hiyo hiyo ya wazawa, tazara, na wengineyo
Si kwa awamu hii ya kujikombakomba.
 
Hii issue ime raise kipindi hiki ambacho wasafirishaji wengi wakubwa huko Tanzania kuhamia Zambia,nina imani ni wao ndio wanao lobby hili jambo,huyo lukumay anajua hili,wazambia kipindi za nyuma gari zilizokuwa zikija huko Tanzania kwa wingi ni Nsembo Trans,wakakata mguu huko sababu wanasema ni gharama .
 
Serikali ijenge bandari kavu hapo TUNDUMA,maroli yote ya Mizigo yaishie TUNDUMA,nchi za kigeni zichukulie Mizigo Yao hapo!pia tunaweza kuachana na Malori tukaamua kuitumia reli ya TAZARA!

Nmeandika utafikiri wananisikia😆😆
 
Kumbe jamaa wako sahihi, kila nchi inawalinda madereva wake dhidi ya kukosa ajira.

Tanzania, Malawi, SA, Mozambique na Zimbabwe mtindo ni huo huo ndio maana Zambia ambao walikuwa hawajaanzisha sera hii wasafirishaji wanalalamika kuwa wamelazimika kupaki malori. Wako sahihi.
 
Ni serikali yetu Tanzania ikae na wamiliki wa malori Tanzania TATOA kuona itafanyaje, tumeona ushaidi serikali ya Zambia imekaa vikao na madereva wa malori na sekta ya usambazaji mafuta OMC ili kuweka utaratibu wao wa kujaribu kutatua changamoto kwa haraka na uwazi.

26 June 2021​

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ANAZUNGUMZA NA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Source: millard ayo
 
26 June 2021
Dar es Salaam, Tanzania

NGALULA : CHANGAMOTO NYINGI ZA SEKTA BINAFSI ZIMEFANYIWA KAZI NDANI YA MUDA MFUPI

Katika mkutano wa 12 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Juni 26, 2021 Ikulu Dar es salaam, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini TPSF Angelina Ngalula, amezipongeza wizara zote zinazoshirikiana na sekta binafsi.

Lakini pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka historia ya kufanya mazungumzo na wafanyabiashara mara tatu ndani ya miezi mitatu ambapo jambo hilo halikuwahi kutokea.

Aidha, Bi. Ngalula ameeleza kuwa kama taasisi waliwiwa vigumu kuandaa hoja za kuja kuzungumza kwenye mkutano huo kwa baadhi ya changamoto nyingi za kila sekta zilizokuwa zikiiibuliwa zimefanyiwa kazi kwa muda mfupi na nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi kwa kuwekwa kwenye bajeti ya mwaka 2021/22.
Source : BizTV Tanzania
 
Back
Top Bottom