... unapozungumzia magari ya kigeni utawaathiri hata wasiohusika, wasio na sheria ya hovyo kama hiyo ya Zambia. Kuanzia DRC, Burundi, Malawi, Rwanda, Zimbabwe, etc. waathirike na road toll kwa sababu ya Zambia?Waanzishe road toll kwa magari ya kigeni
Kaka umeeleza vizuri but kwa muktadha wa tunacho kijadiri, je serikali iingilie kati kuhusu malori ya Zambia kwenye bandari yetu? Nadhani (kwa mtazamo wangu ) hili sio sahihi, serikali ihakikishe bandari yetu inaendelea kupendwa na nchi jirani ziendelee kuitumia Dar port then hayo masuala ya gari za wapi zichukue mzigo liwe jukumu la sekta binafsi kuhakikisha linatoa huduma za uhakika ili wafanyabiashara wa nchi nyingine wapende vya kwetu; Unajua hata Kagame aliweza kutunga sheria za namna hiyo kama Zambia, huoni pia kuna Azam Rwanda? Kuna malori kibao ya Azam yenye plates number za Rwanda na sio Bongo, ni hivo hivo.Hapa tunafanya upembuzi yakinifu wa Geopolitics.
Beira ilikumbwa na tufani kali toka baharini na miundo mbinu kuharibiwa. Waasi wa Kaskazini mwa Mozambique wanaendelea kuwa tishio kwa miundo-mbinu na usalama maeneo ya majimbo ya Kaskazini na ya kati ya Mozambique.
Nchi jirani ya Mozambique imeshindwa kutoa uhakikisho kwa wawekezaji wake usalama na ulinzi kutokana na majeshi ya usalama ya Mozambique kupenda rushwa, kukosa morali ya kupigana na waasi, kuuza silaha kwa waasi.
Na nchi hiyo ya Mozambique kuendeshwa kikanda mfano viongozi wa juu kutoka kaskazini ya Mozambique hawana utashi kuhakikisha tishio la waasi kaskazini likiisha kwani kwanza waasi ni ndugu zao, pili kwamekashimisha majeshi ya kampuni binafsi "wapambane" na waasi ili makampuni hayo yatoe rushwa kwa viongozi wa serikali ya Mozambique.
Kifupi mikutano hii ya dharura ya troika huko Mozambique inazungumzia hatari iliyopo inayotishia uchumi na usafiri wa eneo hilo la kati ya Mozambique na kaskazini ya Mozambique.
Tanzania itumie geopolitics yake vizuri kuwabana hawa wenzetu wa Zambia kuwa warudi mezani kwa manufaa yao.
Tatu ushawishi wa Tanzania kwa nchi za Kusini ya Afrika ni mkubwa kuliko "lugha ya kiswahili ya Palamagamba", hapa diplomasia ya kiuchumi itumike ipasavyo kwa lugha mama ya Diplomasia ya Kimataifa ambayo ni Kiingereza kukumbushia maagano, mapatano, maazimio na protokali zote za SADC juu ya kuwepo biashara huria huru miongoni mwa nchi wanachama zizingatiwe na kuwa sheria mbaya hii ya Zambia imekiuka na kukengeuka matumaini ya uwepo wa SADC imara.
Kaka umeeleza vizuri but kwa muktadha wa tunacho kijadiri, je serikali iingilie kati kuhusu malori ya Zambia kwenye bandari yetu? Nadhani (kwa mtazamo wangu ) hili sio sahihi, serikali ihakikishe bandari yetu inaendelea kupendwa na nchi jirani ziendelee kuitumia Dar port then hayo masuala ya gari za wapi zichukue mzigo liwe jukumu la sekta binafsi kuhakikisha linatoa huduma za uhakika ili wafanyabiashara wa nchi nyingine wapende vya kwetu; Unajua hata Kagame aliweza kutunga sheria za namna hiyo kama Zambia, huoni pia kuna Azam Rwanda? Kuna malori kibao ya Azam yenye plates number za Rwanda na sio Bongo, ni hivo hivo.
Kutokua na Amani Msumbuji (sio kitu kizuri anyway) ni fursa kwetu, tuitumie vizuri, ndicho ambacho USA ilikitumia na inakitumia hadi sasa and i think hata ustawi wa Israel hutegemea sana AMANI ya mataifa ya Kiarabu ya pale mashariki ya kati, yakiwa na amani halafu wakawa wanafanya na vikao vyao vya OPEC vizuri then stability ya Israel hua inakua very poor, wakianza maujinga yao ya kupigana pigana na kutokuamina kama ilivyo sasa, Israel huaga inastawi sana. Ni hayo tu, nina heshimu sana mchango wako kwa uzi hu.
Si kwa awamu hii ya kujikombakomba.Hii inaweza kujibiwa na reciprocal action, hiyo mizigo ikivuka mpaka kuja tz ichukuliwe na wa tz ktk ratio hiyo hiyo ya wazawa, tazara, na wengineyo
Ule wizi wa mafuta bandarini mpaka leo hii haijulikani nini kinaendelea. Hii ni zaidi ya dhaifu.Lukumay atulie tu, kwa sasa hatuna serikali ya kutetea wananchi wake, tuna Rais dhaifu mwenye upeo dhaifu pia.
Ni serikali yetu Tanzania ikae na wamiliki wa malori Tanzania TATOA kuona itafanyaje, tumeona ushaidi serikali ya Zambia imekaa vikao na madereva wa malori na sekta ya usambazaji mafuta OMC ili kuweka utaratibu wao wa kujaribu kutatua changamoto kwa haraka na uwazi.