Zambia imesitisha zoezi la kuhesabu kura kote nchini leo Ijumaa kufuatia ripoti za vurugu katika baadhi ya maeneo. Afisa mkuu wa uchaguzi Brown Kasaro amesema "Ghasia hizo zinawalenga wafanyakazi wa uchaguzi, na katika baadhi ya matukio zimesababisha wizi wa karatasi za kura kwenye masanduku ya kura".
Ameongeza kuwa tume hiyo itatathmini upya uamuzi wa kusitishwa zoezi hilo ndani ya saa 24. Taifa hilo lenye utajiri wa shaba kusini mwa Afrika lilipiga kura Alhamisi katika uchaguzi ulioangazia zaidi hali ngumu ya kiuchumi.
Soma pia:Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini zambia
Rais Hakainde Hichilema, ambaye amekuwa madarakani tangu 2021, alikabiliana na Brian Mundubile, waziri wa zamani mwenye umri wa miaka 55 katika serikali iliyopita ya Patriotic Front (PF). Mundubile amedai kushinda, huku Hichilema akisema timu yake inapokea "matokeo ya kutia moyo".
Tume imesema imesitisha mara moja kuhesabu kura kutokana na hali ya usalama na vitisho vinavyoendelea vya vurugu. Uamuzi huo utapitiwa upya ndani ya saa 24.
Wakati huo huo, kiongozi mkuu wa upinzani, Brian Mundubile, ametangaza ushindi akidai kuchelewa kwa matokeo kunaweza kutoa nafasi ya kuingiliwa au kubadilishwa kwa matokeo.
Mundubile pia amedai kuwa wanajeshi walichukua udhibiti wa vituo vya kuhesabia kura katika mji mmoja na kwamba baadhi ya masanduku ya kura yaliondolewa vituoni, ingawa hakutoa ushahidi wa madai hayo.
Source: DW Swahili