"Zanzibar Cup " Dkt. Conte: Tupeleke ujumbe mzito wa amani na udugu miongoni mwa watu!

"Zanzibar Cup " Dkt. Conte: Tupeleke ujumbe mzito wa amani na udugu miongoni mwa watu!

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
"Zanzibar Cup " Dkt. Conte: Tupeleke ujumbe mzito wa amani na udugu miongoni mwa watu!

Ni vizuri Dk. Stefano, tuombe hilo, na je Unalo jambo lolote zaidi ambalo ungependa kuwaeleza wasikilizaji na wasomaji wa makala hii?

Kwanza kabisa ninaomba niwashukuru wale waliofanikisha mradi wangu. Awali ya yote napenda kumshukuru Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ambaye aliiamini Zanzibar Cup tangu kukutana kwa mara ya kwanza huko Roma alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na amekuwa akitusaidia daima.

Napenda pia kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar Dk Samia Suluhu Hassani ambaye kila mtu anamfahamu kama: “Mama Samia” na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi kwa ukarimu wao na kuchangia kuifanya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuwa maarufu zaidi duniani. Pia nataka kuishukuru kampuni inayoandaa, Zannet, pamoja na BMTZ, ZCT na PDB. Nawashukuru pia wadhamini wote waliotuamini: Asas, Mecco, Vigor, Melia, Planhotel, Neptune, Dongwe, Kendwa Rock, Serena na Marumaru.

Na mwisho, namshukuru kila mtu ambaye atatusaidia kufikia mafanikio makubwa kama vile: migahawa ya Amuri na Vuai, wasambazaji wa boti wakiongozwa na Rama, wajumbe wa kuamua na waandishi wa habari wote watakaoshiriki katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na BMTZ utakaofanyika tarehe ishirini na nne au ishirini na tano mwezi wa Agosti katika hoteli ya Marumaru na ambao ninatumaini watanipa ripoti nzuri za video kuhusu shindano hilo. Baadaye nitatuma ripoti hizi za video kwa vyombo vya habari duniani kote. Nawakumbatia nyote na kuwasubiri mwisho wa Agosti kule Kiwengwa kwa ZC.

Hayo ndiyo yalikuwa maelezo ya Daktari Stefano Conte kutoka Roma, na ambaye kama tulivyomsikia kwamba kwako wewe msikilizaji/ msomaji anajulikana Stef kutoka Zanzibar ambaye ni mhusika mkuu wa Mpango wa Toleo la nne la ZC (Zanzibar Cup wa Kitesurfing), mchezo ambao umekuwa wa kimataifa na unapoendwa sana. Usikose kujiandikisha katika toleo hili litakalofanyika, la mashindano ya freestyle (mtindo huru) na fainali ya regatta Dominika tarehe 31 Agosti 2025.

FB_IMG_1754935314758.jpg
 
Back
Top Bottom