LGE2024 Zanzibar hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tupeane elimu kidogo kuhusu Chaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Hivi karibuni huko Tanzania Bara kumekuwa na mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo leo Novemba 27, 2024 Wananchi wanapiga kura.

Mimi kama mdau wa siasa na mifumo ya Uchaguzi Zanzibar nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu kwanini Zanzibar kumekuwa hamna shamrashamra za Uchaguzi kama ilivyo Bara.

Nianze kwa kusema kuwa huku Visiwani, kwa miaka yote hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Viongozi wote wa Serikali za Mitaa huteuliwa na viongozi wa Serikali Kuu hawachaguliwi na wananchi.

Huku Zanzibar kwa ngazi ya chini kabisa ya Serikali za Mitaa huwa tuna Masheha ambao kwa Bara ni kama viongozi wa Kata.

Hawa Masheha huteuliwa na Wakuu wa Mikoa na huwa wako kwenye level ya chini kabisa ya Uongozi.

Ukitoa ngazi ya Sheha anayefuata ni mtu wa Halmashauri alafu ndo anakuja Mkuu wa Wilaya ambao wote wawili yaani mtu wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya wanateuliwa na Rais.

Kwa ujumla sisi wananchi wa Zanzibar hatuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Badala yake huwa tunashiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ambapo katika Uchaguzi Mkuu sisi huchagua viongozi watano ambao ni Diwani, Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, tunapiga na Rais wa Zanzibar alafu tunapiga na zile mbili za Bara ambazo ni za Mbunge pamoja na Rais.

Pia soma ~ Hivi Zanzibari nako kuna Uchaguzi Serikali za Mitaa? Kweli CUF haina mgombea hata mmoja mwaka 2024?
 
Kiufupi unaongozwa na kiongozi ambaye haujamchagua
 
Hivi karibuni huko Tanzania Bara kumekuwa na mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo leo Novemba 27, 2024 Wananchi wanapiga kura.

Mimi kama mdau wa siasa na mifumo ya Uchaguzi Zanzibar nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu kwanini Zanzibar kumekuwa hamna shamrashamra za Uchaguzi kama ilivyo Bara.

Nianze kwa kusema kuwa huku Visiwani, kwa miaka yote hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Viongozi wote wa Serikali za Mitaa huteuliwa na viongozi wa Serikali Kuu hawachaguliwi na wananchi.

Huku Zanzibar kwa ngazi ya chini kabisa ya Serikali za Mitaa huwa tuna Masheha ambao kwa Bara ni kama viongozi wa Kata.

Hawa Masheha huteuliwa na Wakuu wa Mikoa na huwa wako kwenye level ya chini kabisa ya Uongozi.

Ukitoa ngazi ya Sheha anayefuata ni mtu wa Halmashauri alafu ndo anakuja Mkuu wa Wilaya ambao wote wawili yaani mtu wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya wanateuliwa na Rais.

Kwa ujumla sisi wananchi wa Zanzibar hatuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Badala yake huwa tunashiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ambapo katika Uchaguzi Mkuu sisi huchagua viongozi watano ambao ni Diwani, Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, tunapiga na Rais wa Zanzibar alafu tunapiga na zile mbili za Bara ambazo ni za Mbunge pamoja na Rais.
Serikali za mitaa na masuala yote ya TAMISEMI si mambo ya Muungano.Ni makosa makubwa kuyapeleka of is
ofisi ya rais ambaye siyo Mtanganyika.Tamisemi irudishwe ofisi ya waziri mkuu kwa Sasa.
 
Back
Top Bottom