Zanzibar inachangia nini kwenye Serikali ya Muungano? Isije ikawa wanatumia Kodi za Bara

Mkuu Zanzibar inachangia Jina maana hebu piga picha tu Tungeendelea kuitwa "Tanganyika" jina lenyewe linahuzunisha kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
BOT msingi wake zanzibar ndio walitoa fedha nyingi za kigeni kuanzishwa kwake leo Tanganyika wanajifaragua na BOT wamesahau msingi wake, TRA inakusanya kodi kule zanzibar lakini zile kodi zinaenda kutumika kwa maendeleo ya Tanzania Bara, hizo fly over zote ni hela za karafuu
 
Sio kweli Zanzibar haitambuliki duniani ndioaana haina kiti UN wala haipo FIFA
 
Nyinyi hata pesa ya mishahara mnategemea itoke bara
 
Mkuu sasa naona uko tayari "kushika nyati sehemu za Siri"
 
Zanzibar ndio inalipa mishahara ya watanganyika kupitia kodi za TRA waliotapakaza ofisi kule Zanzibar. Zanzibar hainufaiki na kodi za TRA hela yote inakuja huko kwenu unyamwezini, ki ufupi bila Zanzibar hakuna Tanganyika
Nyinyi hata mchanga wa kujengea mnataka utoke bara halafu unakuja kupiga kelele
 
Mkuu Zanzibar inachangia Jina maana hebu piga picha tu Tungeendelea kuitwa "Tanganyika" jina lenyewe linahuzunisha kabisa
Hahahahahah kwahio Zanzibar mchango wake ni jina tu! Wonders shall never end ila poa tu waiche Zenji ije itekwe ili akina Alshababu wapitie zenji kuja kuwaua bara na kupora mali! Nafikiri hilo litapendeza sana maana kinachotokea Kinshasa na Brazavile huku hamna ufahamu nacho!
 
Mkuu tumeona miaka hii sukari ni shida na bei ya juu, lakini Znz wana sukari na bei ya chini.

Sheria hairuhusu wa Znz kutuuzia sisi sukari, ila sisi tunaruhusiwa kuwauzia wao.

Je unahisi nani anafaidika? Viwanda vya Znz ama vya huku kwetu?
Bara tupo millioni 55,Zenj wapo millioni tano tu,bara kwa wingi wa watu ni soko kubwa,ukiruhusu sukari ya Zenj,ije bara,bei itakuwa kubwa sana Zenj,wananchi watapata tabu sana,
 
Mawazo hayo ndio yale akina lukuvi, uwongouwongo ilimradi maisha yaende

Sent from my SHARK MBU-H0 using JamiiForums mobile app
 
Muungano huu hauna faida kwa watanganyika. Unawafaidisha wazanzibari tu.

Anayebisha anyooshe mkono juu, au hata afanye kama anajikuna. Halafu alete faida moja tu ambayo mtanganyika anaipata.
Sasa kama wewe unasema kuwa muungano hauna faida kwa watanganyika hebu twambie ni kwa nini basi watanganyika ndio walio mbele zaidi kukataa kuuvunja huu muungano? Wazanzibari wamekuwa wakipiga kelele kila siku wanataka nchi yao kwa nini hamuwapi? Kama kweli zanzibar inaitia hasara tanganyika na inawazuia kupata maendeleo ya haraka ni kwa nini viongozi wenu wote wa ngazi zote bado wanasisitiza muungano uenzwe? Ukiwa na mke na akafanyii lolote jema na kila siku kukicha anadai talaka yake, hivi utabaki nae au utampa talaka na akafie mbeleni? Sasa kwa nini wadangabyika hamfanyi hivyo? Na toa onyo kabisa hapa msije na kasumba eti kuwa sisi ni ndugu, au tumechangaya udugu! hiyo ni BS tu. Wazanzibari wamechanganya damu na wakenya zaidi kuliko watanganyika!

Huko nyuma miaka ya nyerere ilielezwa sababu kuu ya muungano ilikuwa ni kuilinda na kuipa nguvu zaidi tanganyika kutoka kwa maadui wa eastern and western block. Mfumo wa siasa duniani umebadilika na tanganyika haina sababu yeyote ile ya kuhofia siasa za blocks hizi mbili, sasa kwa nini bado mnang'ang'ania visiwa hivi?
 
Bara tupo millioni 55,Zenj wapo millioni tano tu,bara kwa wingi wa watu ni soko kubwa,ukiruhusu sukari ya Zenj,ije bara,bei itakuwa kubwa sana Zenj,wananchi watapata tabu sana,
Kwa logic hii, Kuwait wasiuze mafuta, haiwezekani nchi ndogo kama wilaya ya Tanzania iuze mafuta bei itapanda sana kwao.

Hakuna kitu kama hichi mkuu, zamani Zanzibar ilikuwa center ya biashara, walikuwa na vitu vingi sana na nchi nyingi walienda kufungaShia mzigo kule, ila sisi tumewaminya kwa kuweka sheria zetu za kikoloni, wanachozalisha wao ni Chao wauziane ila tunachozalisha sisi tunaruhusiwa kuwauzia wao, hii Sera imewaacha Hoi taabani viwanda na biashara zao.

Juzi kati nilikua Zanzibar biashara na maduka yamechoka, unakuta tu vikavakava vya simu kama Agrey.
 
Wazanzibari wakishajitenga na kuwa nchi ya kujitegemea, watafika mbali sana. Na manyanyaso, masimango hayatakuwepo tena



Ushauri wangu kwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan, kaa na wazanzibari uwasikilize hoja na matakwa yao ya muda mrefu bila kupoteza muda.. huu ndio wakati wao kuyasema yaliyo moyoni mwao wakijua wana RAISI mwenye hekima, busara na huruma. na mkubaliane kwa amani na utulivu dhidi ya huu muungano usio na faida kwao, ni heri uvunje muungano huu ubaki ukijitegemea. Mh Raisi usiwasikilize wanaotaka muungano uendelee, otherwise utakua hujawatendea haki wazanzibar, ilhali wanaoumia na kuteseka ni wao, huku wabara wenzangu nilionao wakila bata na kwendelea kuchekelea muungano uendelee kuwepo. Nakuomba mama yangu, nayasema haya nikiwa bara, lakini sipendi kuona wazanzibar wakisemwa na kunyanyaswa kiasi hicho.


Kwako Raisi Samia Suluhu Hassan.

Hakika wewe ni jembe
 
Muungano huu hauna faida kwa watanganyika. Unawafaidisha wazanzibari tu.

Anayebisha anyooshe mkono juu, au hata afanye kama anajikuna. Halafu alete faida moja tu ambayo mtanganyika anaipata.

Ebu igeuze kinyume chake utakua umetenda haki, watu wanaishi kama yatima alafu mnasapoti muungano uendelee kuwepo!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…