Makaimati
JF-Expert Member
- Apr 4, 2011
- 462
- 87
Bila ya shaka utakuwa umesikia leo taarifa ya lile daraja refu zaidi kupita bahari limefunguliwa huko China leo. Daraja hilo liitwalo Daraja la Qingdao Jiazhou lina urefu wa kilometa 42 (sawa na umbali wa mbio za marathoni) kama mile 26 hivi. Daraja hilil la China la kisasa kama picha zinavyoonesha limejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.5 (karibu na shilingi za Kitanzania Trilioni 2 na ushee). Daraja hili lilianza kujengwa mwaka 2006 na limekamilika mwaka 2011 kama ilivyotarajiwa.Zanzibar for Zanzibaris.
- Nakubaliana na wewe Mkuu kuwa bahari si kikwazo cha kuunganisha sehemu mbiili za nchi moja lakini hii dhana ya kuwa Tanzania ni nhi moja ni ya kwenu tu
- Kama nia ya kujenga daraja ni kuimarisha "muungano", sisi hatuna haja nao
- Kama ni kuungana, unganeni na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Msumbiji wala hakutakuwa na gharama yoyote ile zaidi ya kupoteza utaifa wenu kama sisi mlivyotupotezea wetu
- Endeleeni na ufisadi muimalize nchi yenu
- Hivi sasa hakuna daraja na mmejaa tele, jee ikijengwa"
- Hatutaki daraja wala "muungano", kama ni udugu wa damu, tunao kabla ya kuungana.
- Msiendelee kujidanganya, "muungano" haupo.
