DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
,,,Usipende kuona mawazo YAKO ndo ya WAZANZIBARI woote bana,kuna wengine tuna mawazo tofauti kabisa na wewe,,Mwanakijji hilo ni wazo zuuri sana,hakika kuna watu wanafikiria mbali,Muungano uwepo au usiwepo daraja litasaidia pande zote mbili KIUCHUMI na hata KIJAMII kwa ujumla,kwani tuna akina ANKALI zetu huko moro,akina AUNTIE zetu NATA NZEGA huko.

Kama mliweza kupata ankali bila daraja sasa tatizo nini? Na kuhusu mawazo sawa hayo yawe yako na pia hayawezi kuwa ndio uamuzi wa mwisho kwa Wazanzibari. Lakini sioni kama hawa jamaa wana uwezo wa kufanya hivyo hasa nikitilia maanani yale majumba makubwa kule ni ya watu wengine sio Watanganyika original.
 
Mimi nawaambia tungekuwa na viongozi kweli wenye maono ya kuthubutu, uthabiti wa vitendo na siyo "tutafikiria na kupanga mchakato" tungeweza kujenga Kigamboni (miaka kumi iliyopita) na la Zanzibar lingekuwa tayari; tungekuwa tayari tumejenga Stielger's Gorge dam badala ya hivi vya 20MW na 100MW plants! Stielger's ilipokaridiwa wakati ule ingegharimu dola bilioni kama 2 hivi! kiasi ambacho tunakipoteza kwa ufisadi every two years or so.

Hivi, mmesahau mambo ya opportunity cost? Gharama ya kweli ukiangalia siyo ya vile ambavyo tunafikiria tumevifanya!!

Una maana hii tunge.. haiwezi kuwapo kwa hiyo ndoto yako?
 
Si wazo jipya kama mtoa mada anavyotaka, hili wazo ni lazamani sana na limezingumzwa sana toka 70s.
 
Si wazo jipya kama mtoa mada anavyotaka, hili wazo ni lazamani sana na limezungumzwa sana toka 70s. Labda ni jipya kwa kulileta JF.
 
Ndio nshasema hivyo, labda wewe unanijua.

Makaimati,

Zanzibar hakuna mtu anayeitwa mzanzibari mzawa hiyo ni fikra ya kibaguzi iliyoanzishwa na Nyerere na Karume kubaguana zanzibar kuwa eti kuna wanzanzibari na wasiowazanzibari. Zanzibar imechanganyika makabila mengi kuna waarabu (wako sana pemba), wasandawe, wanyamwezi, wazaramo, wareno, wachina, wangazija sasa niambie nani mzawa zanzibar?????
 
Naam! Tunapokea hiyo chalenge yako!

Huyu jamaa nadhani wale wanzanzibari mamluki wasioyoijua zanzibar kila kukicha anadai zanzibar yao iachwe itengwe. Kuitenga Zanzibar ni ujinga na kukosa mantiki yote nia na madhumuni ni kuficha ufisadi ulio nyuma ya fikra zao. Wakijitenga wataanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe hasa baina ya wapemba na waunguja. Macho yao yote yamekalia kwenye mafuta hakuna kengine.

Pili Zanzibar ikijitenga kuna swala la mipaka ya Zanzibar iko wapi ramani ya kabla inaonyesha mpaka wa zanzibar ni pwani yote ya tanganyika na kenya na visiwa vya unguja na pemba matatizo yataanzia hapo je mipaka ya zanzibar ipi? Bora na afadhali tudumishe muungano kurekebisha kasoro zilizopo au kuunda serikali tatu. Kujitenga kwa zanzibar kunaweza kutibua masuala mengi.

Hilo sio mada husika hapa ni mada je daraja lina faida gani? Mile 22 sio nyingi na daraja litasaidia mengi badala kuwa na fikra chanya vijitu vichache vyenye fikra mgando kama huyu wanakuja na kelele za kujitenga kila siku. Wanawadanganya wazanzibari walio wengi ambao hawajasoma kwa kuwajaza fikra hasi kwa matakwa yao.

Muungano una mapungufu na kweli kuna maeneo umechangia kuua uchumi wa zanzibar ila hizo ni hasara za muungano la msingi ni kuimarisha yale mapungufu ili tuendelee na sio kila siku kujitenga kujitenga.
 
Mkuu MMKJJ pamoja na umuhimu wa kuwa na ndoto za aina hiyo, ni mpaka pale tu tutakapojikomboa na fikra za kusherehekea misaada ya "vyandarua, madawati hafifu, na matundu ya vyoo mashuleni" ndipo tutakapoweza angalau kutafakari mambo makuu ya aina hiyo ambayo, ni dhahiri, tunayaweza chini ya mfumo makini wa uongozi; sio huu wa kisanii (mediocre) tulio nao.
 
Daraji la Feri - Kigamboni tu hata Kilometa 1 haifiki, but mpaka leo ni hadithi,
sembuse kilometa 40?
Kwanza muungano wenyewe kwa sasa ni kama umeungwa na gundi ya mate, yakikauka tu hakuna tena muungano
 
..Zanzibar itachangia kiasi gani?

..wa-Tanganyika watafaidika vipi na mradi huu?

..naomba mnieleze faida za KIUCHUMI za mradi kama huo, kwa maoni yangu umekaa kisiasa-siasa zaidi.
 
wacheni ndoto za ali nacha hizo..Corruption Goverment ya TZ Haiwezi kufanya kitu kama hicho Mawazo makubwa ya JK na Cabinet yake ni kumaliza Kujenga Nyumba zao (Palace) na kuwa na Business Company zao kabla ya Uchaguzi ujao 2015
Tuletee Wazo ambalo na sisi wa TZ tuwe na angalau City Rail na Speed Bus angalau tufikie kiwango ambacho majirani wetu wa nchi za Africa:clock:


Addis Ababa, Ethiopia Over pass High way
The road, which cost 353 million Br, is meant to ultimately connect Ethiopia to Berbera Port in Somaliland, located 937km from Addis Ababa.
2010249524.jpg



Nigeria lagos City light Rail and High speed bus

4-Image-4.jpg


Morocco City light Rail
19822512733622.jpg
 
Acha utani! Tumeshindwa kujenga daraja kigamboni lisilozidi mita 400.Thubutu across Zanzibar channel thats beyond our wildest dream and honestly a herculian engineering task.Muzuri zaidi kuandaa timu ya marathon ikapige lap Qingdao Jiazhoij bridge, hii burudani tosha.
 
..Zanzibar hakuna ufisadi kama huku Tanganyika.

..watumie mapato yao wenyewe kujenga hilo daraja.

..mahesabu yote yanapigwa kwa kuangalia vyanzo vya Tanganyika. how about Zanzibar?
 
Huyu jamaa nadhani wale wanzanzibari mamluki wasioyoijua zanzibar kila kukicha anadai zanzibar yao iachwe itengwe. Kuitenga Zanzibar ni ujinga na kukosa mantiki yote nia na madhumuni ni kuficha ufisadi ulio nyuma ya fikra zao. Wakijitenga wataanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe hasa baina ya wapemba na waunguja. Macho yao yote yamekalia kwenye mafuta hakuna kengine.

Pili Zanzibar ikijitenga kuna swala la mipaka ya Zanzibar iko wapi ramani ya kabla inaonyesha mpaka wa zanzibar ni pwani yote ya tanganyika na kenya na visiwa vya unguja na pemba matatizo yataanzia hapo je mipaka ya zanzibar ipi? Bora na afadhali tudumishe muungano kurekebisha kasoro zilizopo au kuunda serikali tatu. Kujitenga kwa zanzibar kunaweza kutibua masuala mengi.

Hilo sio mada husika hapa ni mada je daraja lina faida gani? Mile 22 sio nyingi na daraja litasaidia mengi badala kuwa na fikra chanya vijitu vichache vyenye fikra mgando kama huyu wanakuja na kelele za kujitenga kila siku. Wanawadanganya wazanzibari walio wengi ambao hawajasoma kwa kuwajaza fikra hasi kwa matakwa yao.

Muungano una mapungufu na kweli kuna maeneo umechangia kuua uchumi wa zanzibar ila hizo ni hasara za muungano la msingi ni kuimarisha yale mapungufu ili tuendelee na sio kila siku kujitenga kujitenga.


,,,,Kula TANO baba!
 
Mdondoaji said:
Pili Zanzibar ikijitenga kuna swala la mipaka ya Zanzibar iko wapi ramani ya kabla inaonyesha mpaka wa zanzibar ni pwani yote ya tanganyika na kenya na visiwa vya unguja na pemba matatizo yataanzia hapo je mipaka ya zanzibar ipi? Bora na afadhali tudumishe muungano kurekebisha kasoro zilizopo au kuunda serikali tatu. Kujitenga kwa zanzibar kunaweza kutibua masuala mengi.

Mdondoaji,

..Zanzibar iliyojiunga na Tanganyika ni visiwa viwili vya Unguja na Pemba.

..mipaka ya Zanzibar inaeleweka na kutambulika.


..
 
Wazo hata mimi nimelipenda. Kutokea maeneo ya Mbweni, Bagamoyo kuelekea kusini ya kisiwa cha Unguja maeneo ya Kizimkazi Dimbani ni kilomita 36.4 au 22 miles. Mradi kama huu utaleta maantiki zaidi ikiwa toll road mosi - ili fedha za mradi zirudi na pili - ili daraja liweze kujiendesha lenyewe.

Cheki ramani hapo chini nimechukua screen shot toka google earth

Wanzagi nimependa hiyo point maana yake, yawezekana hapo ni the shortest distance which is about under 20Miles! ina maana hata gharama yake it could be less than a Billion Dollar. Tuwape Wachina tu!
 
..Zanzibar itachangia kiasi gani?

..wa-Tanganyika watafaidika vipi na mradi huu?

..naomba mnieleze faida za KIUCHUMI za mradi kama huo, kwa maoni yangu umekaa kisiasa-siasa zaidi.

JokaKuu, sidhani kama Tanzania imesha exhaust its full economic potential. Ninaamini we can be a great nation kama tukitaka. Nilikuwa napitia nyaraka fulani za H. Kissinger vitu alivyovisema vya Tanzania ya 1976 (kwenye secret conversation na Rais Ford) vinashangaza sana. Alitambua kuwa Tanzania ndio "intellectual leader" of the Southern Africa. Tulikuwa (katika umaskini wetu) kufahamika kuwa we had the brightest minds then - hata leo utaona kuwa wasomi wetu wengi wa enzi hizo walienda na kujenda Namibia na Botswana ya leo, na baadhi yao kumbe waNyarwanda wamerudi kwao na kujenga Rwanda.

Sasa, kupoteza huku njia kuna maana ya kuwa kumetuathiri sana kwenye uzalishaji na consumption sana. Naamini kutengeneza infrastructure kama hii inaweza isitufaidishe mimi na wewe leo lakini huko mbeleni ikawa ni catalyst kubwa ya maendeleo ya visiwani na pwani.. Kwa sababu fikiria mojawapo ya vikwazo vikubwa vya Zanzibar kiuchumi ni kuwa bidhaa zake ili zisafirishwe zinahitaji meli au ndege au boti! Lakini kutengeneza Barabara kunaifungua Zanzibar kwa upya kabisa. Hisia ya kujitenga na kufungwa kama "kisiwa" itaondolewa, na uwekezaji hata wa kutoka bara nao utakuwa mkubwa tu visiwani. Kimsingi naamini itakuwa ni mwanzo wa kutatua kero nyingi tu ambazo zipo leo hii.

Ila ukifikiria kwa maana ya faida ya "sasa" sidhani kamatunaweza kuiona bila kuangalia faida ya mbele.
 
Acha utani! Tumeshindwa kujenga daraja kigamboni lisilozidi mita 400.Thubutu across Zanzibar channel thats beyond our wildest dream and honestly a herculian engineering task.Muzuri zaidi kuandaa timu ya marathon ikapige lap Qingdao Jiazhoij bridge, hii burudani tosha.

Unaweza usiwe na uwezo wa kuvunja minyororo ambayo mtu amekufunga nayo mikononi na miguuni na kukuona mtumwa wake. Lakini usipoweza kuvunja minyororo ya kifikra basi unajibitisha kuwa ni mtu mwa wa kifikra. Wale waliokuwa wakituchukua utumwa walifanya kitu cha kwanza kikubwa ni ku-dehumanize us and demoraliize hivyo, wakatufanya tujishuku kuwa si binadamu kama wao na hivyo kutumikishwa kwao. Walipotokea watu kusema "tutake uhuru wetu" na kuwa "na sisi tunaweza kuishi kama watu huru" (angalia filamu ya Amistad) wengine hawakuamini hilo. Waliamini kuwa watawala wao wana uwezo juu ya maisha yao.

Mojawapo ya vitu ambavyo nimeviona kwenye wazo hili ni athari za ufisadi na utawala mbovu. Watawala wetu wametudemoralize kiasi kwamba hata tukisema tuanze mradi mkubwa wa kujenga mifereji ya kisasa ya taka JIji la Dar jibu la kwanza "hatuwezi" au "mbona tumeshindwa x,y". Tunanyong'onyea.

Sishangai sentiment yako kwani nimeitarajia kwenye hoja yangu ya msingi hapo juu; kwa sababu ninafahamu madhara ya kutawaliwa kifisadi. Ili kuvunja minyororo hii kwenye fikra zetu ni lazima tupige kelele kuwa na sisi "tunaweza, tunastahili" na kuzinjilia mbali. Ni hapo utaona kuwa daraja hili na la Kiagmboni yanaweza yote kutengenezwa ndani ya bajeti moja! Incredible? Yes! Doable? Absolutely!!
 
wananchi wa mtwara bado hawajaunganishwa na lami kutoka dar, unafikiria mradi wa kujenga lami baharini?
 
Back
Top Bottom