DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hakika ni wazo zuri na huenda umezindua akili za wabunge kuweza kusema chochote bungeni kuliko kwenda na invisible matresses ukaona wanaota ndoto wako hospitalini wakipata dawa za usingizi. Likijengwa liitwe MWANAKIJIJI BRIDGE
 
bado ni ndoto... ma si kwa serikali hii..... ukizingatia kero za muungano inafanya hili wazo kuwa impossible tuanze na la kigamboni kwanza
 
Bila ya shaka utakuwa umesikia leo taarifa ya lile daraja refu zaidi kupita bahari limefunguliwa huko China leo. Daraja hilo liitwalo Daraja la Qingdao Jiazhou lina urefu wa kilometa 42 (sawa na umbali wa mbio za marathoni) kama mile 26 hivi. Daraja hilil la China la kisasa kama picha zinavyoonesha limejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.5 (karibu na shilingi za Kitanzania Trilioni 2 na ushee). Daraja hili lilianza kujengwa mwaka 2006 na limekamilika mwaka 2011 kama ilivyotarajiwa.

e51fd62d93389c0ef10e6a706700fb3f.jpg


2011-06-30T113121Z_01_PEK07_RTRIDSP_3_CHINA.jpg





(Picha zote na AP na Reuters)

Tunajifunza Nini?

a. Bahari si kikazo cha kuunganisha sehehu mbili za nchi moja.
b. Gharama ya kujenga daraja kama hili kuunganisha Tanzania moja ziko ndani ya uwezo wetu na ninaweza kuargue kuwa tunaweza kufanya kwa fedha zetu wenyewe japo utaalamu na wataalamu tunaweza kuwashirikisha rafiki zetu wa China - tukiwapa BAES!
c. Gharama ya dola bilioni 1.5 ni sawa na fedha zilipotea katika ufisadi kwa mwaka mmoja uliopita tu. Tukichanganya fedha zilizopotea kwa miaka kumi iliyopita tungeweza kabisa kuunganisha Zanzibar mara tatu - kutokea Tanga kwenda Pemba, kutoka Dar (au Bagamoyo-the closest points to the mainland from Unguja?) na Pemba na Unguja! - by the Way kwa miaka kumi iliyopita ufisadi umegharimu zaidi ya bilioni 10 (dola!!)
d. Kwenye kile kinachoitwa Mpango wa Maendeleo ambao uko tayari kutumia shilingi trilioni 42 hakuna mpango wa kuthubutu kama huu.
e. Tunapoelekea miaka 50 ya Uhuru hakuna kitu kitakachoonesha Muungano wetu kuwa umehimiri vishindo na matatizo kama kuzinduliwa kwa daraja la Muungano (Union Bridge) japo sehemu yake mwaka 2014 huku likikamilika 2015.
f. Naamini ujenzi wa daraja/madaraja ya kuunganisha Zanzibar na Bara utasaidia sana katika kuleta maendeleo visiwani na kuusogeza ule udugu wa damu kati yetu karibu zaidi kwani kwa mara ya kwanza bahari itaondolewa kama alama ya kutengana kwetu, watu wa Zanzibar na bara wataweza kwenda nchini mwao wakati wowote na mahali popote bila kutishiwa sana na masuala ya usalama kama ilivyo sasa.
g. Bara nako kutanufaika sana na kufunguliwa kwa njia hii mpya.


Maswali ya Kutafakari:
Je kuna uongozi wowote ndani ya CCM wenye mawazo ya namna hii au mwitikio wa kwanza 'hatuwezi?
Je, Rais Kikwete anaweza kuja na mpango kama huu madhubuti wakati daraja la kuunganisha Kigamboni na Kivukoni tu pale limeshindikana hadi hivi sasa licha ya kuwa katika mipango kwa muda mrefu?
Je, yawezekana wazo hili haliwezi kuletwa, kutetewa wala kusimamiwa na viongozi wetu wa sasa - kwani hawana uwezo wa kulisimamia kama Nyerere alivyosimamia kujengwa kwa reli ya Uhuru (of course lazima nirushe dongo kidogo tu!)?
Je, yawezekana Chama cha Mapinduzi kimepoteza kabisa uwezo wake wa kuthubutu mambo makubwa na sasa kimeamua kufanya mambo madogo kama "mabarabara ya juu kwa juu"?
Je, tusubiri uongozi mpya ambao utakuwa tayari kuliunganisha taifa letu.

Jambo pekee ambalo tuna uhakika nalo kwa kuangalia China ni kuwa inawezekana kuunganisha kwa daraja umbali wa kilomita 42 (au hata zaidi) kwani Zanzibar iko kati ya Maili 16-31 sawa na kilomita 25-50 hivi (kutegemeana na eneo unalosimama kutoka bara). Hii ina maana tukiangalia mahali ambapo ni shortest distance. Hivyo swali la kama inawezekana kiteknolojia au vinginevyo limeshabiwa. Kwa upande wetu ni swali la kisiasa zaidi - je tuna viongozi ambao wanaweza kubuni, kusukuma na kusimamia mpango huu?
Hivi wewe unaakili timamu? au umechanganyikiwa kwa kuchezeya matapu tapu bila ya kula? Zanzibar katu hawakubali kuunganishwa na kwa daraja na Tanganyika? Hawataki Muungano seuze daraja juha Mkubwa wrewe.
 
[h=1]Land and Sea Bridge To Connect Saudi Arabia and Egypt[/h] [h=6]Arwa Aburawa | March 1st, 2012 | 2 Comments | Email this[/h] 50Share
Plans to build a Red Sea bridge connecting Saudi Arabia and Egypt have been revived but there are some serious environmental concerns
More than two decades after it was first planned, Egypt and Saudi Arabia may be about to start work on a land and sea bridge connecting the two countries. The proposed bridge would run 50 kilometres from the Tabuk region in Saudi, across the Red Sea to the Gulf of Aqaba in Egypt. Conservationists in Egypt have however raised concerns about the possible destruction of coastal and marine environments in the process of building the bridge. Some explain that the bridge could negatively impact protected areas including coral reefs, the nesting grounds of turtles and the Tiran Island sea birds.
saudi-egypt-causeway.jpg
According to local news sources, Egypt and Saudi Arabia will be meeting in the next few week to discuss the technical details of project. Costing an estimated US$3 billion, the project is by no means a small undertaking. In fact, the size and scale of the project is what concerns conservationist as there appears to be very little in the way of environmental assessment.
Smaller proposals to build artificial islands and bridges in the region have been criticized in the past for their potential environmental damage to the coastline and marine life. In Egypt, there is a constant threat to pristine ecosystems due to tourism industry and efforts to grow the sector following the Arab Spring. However, there should to be clear balance between the environment costs and the economic benefits and at the moment that balance is missing.
Speaking to a conservationist in Egypt, there are concerns about the impact the actual construction of the bridge will have on the marine environment. Building around sensitive marine ecosystems is deeply problematic and there could be long-term implications on fisheries, corals, the sea floor and water quality. Bringing a whole new trading centre to the region will also put pressure on the marine environment and its resources.
And all those in the tourism industry need to bear in mind the impact of this environmental degradation on their sector as the diving and beach industry could be negatively affected. The disruption to those currently living in the area such as local bedouins is another issue which needs to be addressed.
The bridge is designed to facilitate the movement of goods and also pilgrims during the hajj season by reducing the time it takes to cross the borders. Indeed, the bridge would serve as a connection between two continents and it is believed that the cost of the project would be recovered in 10 years through tolls and fees.
::Egypt Independent
 
A great idea, on the other hand, tatizo la terrorism linaweza likatukwamisha kama kutakuwepo na mambo ya msingi tusiyokubaliana kuhusiana na muungano, sijui kulinda itawezekanaje, cha muhimu tuungane kwa kukubaliana na kuridhiana kwanza.
 
Je kuna uongozi wowote ndani ya CCM wenye mawazo ya namna hii au mwitikio wa kwanza 'hatuwezi?
...Hii mada ulikuja nayo ili uwaponde viongozi wa CCM?
Je, Rais Kikwete anaweza kuja na mpango kama huu madhubuti wakati daraja la kuunganisha Kigamboni na Kivukoni tu pale limeshindikana hadi hivi sasa licha ya kuwa katika mipango kwa muda mrefu?
...Kwanini aje na mpango kama huu? Is this a priority to us? I mean, we have got a lot of issues, and they are very basic. We should deal with those first.
Je, yawezekana wazo hili haliwezi kuletwa, kutetewa wala kusimamiwa na viongozi wetu wa sasa - kwani hawana uwezo wa kulisimamia kama Nyerere alivyosimamia kujengwa kwa reli ya Uhuru (of course lazima nirushe dongo kidogo tu!)?
...Hawawezi na hata wewe ukija kesho it will not feature in the list of your priority, as a leader to your people!
Je, yawezekana Chama cha Mapinduzi kimepoteza kabisa uwezo wake wa kuthubutu mambo makubwa na sasa kimeamua kufanya mambo madogo kama "mabarabara ya juu kwa juu"?
...Hii ni fitna.
Je, tusubiri uongozi mpya ambao utakuwa tayari kuliunganisha taifa letu.
...Kama nani? Jussa? Nani kakwambia litaunganishwa kwa mara ya pili?
Jambo pekee ambalo tuna uhakika nalo kwa kuangalia China ni kuwa inawezekana kuunganisha kwa daraja umbali wa kilomita 42 (au hata zaidi) kwani Zanzibar iko kati ya Maili 16-31 sawa na kilomita 25-50 hivi (kutegemeana na eneo unalosimama kutoka bara). Hii ina maana tukiangalia mahali ambapo ni shortest distance. Hivyo swali la kama inawezekana kiteknolojia au vinginevyo limeshabiwa.
...Nothing is impossible under the sun!
Kwa upande wetu ni swali la kisiasa zaidi - je tuna viongozi ambao wanaweza kubuni, kusukuma na kusimamia mpango huu?
...Jibu la kisiasa zaidi ni kuwa, utakuwa na kichaa kuwekeza kwenye ujenzi kama huo wakati watoto wanasoma chini ya mti. Wajengee hata kibanda cha udongo na makuti kwanza. Halafu ndio ujikite kwenye "the bridge to nowhere" !
 
...Jibu la kisiasa zaidi ni kuwa, utakuwa na kichaa kuwekeza kwenye ujenzi kama huo wakati watoto wanasoma chini ya mti. Wajengee hata kibanda cha udongo na makuti kwanza. Halafu ndio ujikite kwenye "the bridge to nowhere" !

DsL, kwanini tulijenga reli ya Tazara wakati sehemu kubwa ya wananchi wetu walikuwa wanaishi katika umaskini? Kwanini tulifanya upanuzi mkubwa wa barabara ya kwenda Kusini na ile ya kwenda Zambia? Kwanini tumetumia fedha nyingi kutengeneza barabara ya kwenda Mwanza? Yote haya tumeyafanya wakati watoto wetu bado wanasoma "chini ya mti"?

Je kwanini tumeamua kujenga daraja la Kigamboni wakati labda ni wakazi wachache sana wa Kigamboni wenye kutumia magari na labda kuna watu bado wako wanaishi kwenye nyumba za tembe huko Kigamboni?

Leo tumesikia Wakenya, Ethiopia na Sudan wanataka kujenga bandari mpya na reli mpya unataka tufikirie kuwa Kenya, Ethiopia na Sudan watoto wao wanaishi katika mazingira bora zaidi kuliko wa Tanzania?
 
@Dar si Lamu

Hilo daraja ndio mwanzo wa kuondoa umaskini pia..

Umaskini wa kazi, pato nk..
 
DsL, kwanini tulijenga reli ya Tazara wakati sehemu kubwa ya wananchi wetu walikuwa wanaishi katika umaskini? Kwanini tulifanya upanuzi mkubwa wa barabara ya kwenda Kusini na ile ya kwenda Zambia?
...Reli walijenga Wachina kwa hela yao. Na ilikuwa siasa zaidi ya uchumi. We all know that by now.
Kwanini tumetumia fedha nyingi kutengeneza barabara ya kwenda Mwanza?
...Lini? Hivi karibuni? Kwani we hujui huko kuna nini?
Yote haya tumeyafanya wakati watoto wetu bado wanasoma "chini ya mti"?
...Issue ya Mwanza tofauti. Hiyo barabara inajilipa yenyewe. Hilo daraja la kwenda Zenj unafikiri litajilipa? Hayo mambo waachie Wachina na ujinga wao wa kupima "ya nani ndefu".
Je kwanini tumeamua kujenga daraja la Kigamboni wakati labda ni wakazi wachache sana wa Kigamboni wenye kutumia magari na labda kuna watu bado wako wanaishi kwenye nyumba za tembe huko Kigamboni?
...Serikali ijengee watu nyumba za bati? Halafu, huu mradi si ni wa NSSF. Labda wamepiga hesabu unalipa.
Leo tumesikia Wakenya, Ethiopia na Sudan wanataka kujenga bandari mpya na reli mpya unataka tufikirie kuwa Kenya, Ethiopia na Sudan watoto wao wanaishi katika mazingira bora zaidi kuliko wa Tanzania?
...We all know these is a different story. We all know!
 
hata madawati ya cyprus hayatoshelezi tuanze kuhangaika kujenga daraja na fiji... hawataki muungano, we dont need to invest hapo
 
Gharama za daraja zitakuwa kiasi gani na zitarudishwaje?

Kujenga daraja ndio kutatupa matumizi bora kabisa ya fedha hizi?
 
Gharama za daraja zitakuwa kiasi gani na zitarudishwaje?

Kujenga daraja ndio kutatupa matumizi bora kabisa ya fedha hizi?
tunahangaika kujenga badhari, airport terminal, hata urban planning... sio haja ya kuanza kuvuka bahari wakati hata kwalit ya barabara za nchi kavu ni questionale

we are not there yet
 
...Reli walijenga Wachina kwa hela yao. Na ilikuwa siasa zaidi ya uchumi. We all know that by now. ...Lini? Hivi karibuni? Kwani we hujui huko kuna nini? ...Issue ya Mwanza tofauti. Hiyo barabara inajilipa yenyewe. Hilo daraja la kwenda Zenj unafikiri litajilipa? Hayo mambo waachie Wachina na ujinga wao wa kupima "ya nani ndefu". ...Serikali ijengee watu nyumba za bati? Halafu, huu mradi si ni wa NSSF. Labda wamepiga hesabu unalipa. ...We all know these is a different story. We all know!


Of course, sijasema tu tujenge kwa ajili ya mapambo! La kwanza ni je ina maana kuunganisha? Well hili ni swali ambalo naamini linaweza kujibiwa in the affirmative.

a. Je kuna watu wa bara na Zanzibar wanasafiri mara kwa mara kati yao? Kuna nini bara au Zanzibar ambacho kinaweza kufaidika kwa kuwepo kwa daraja la kudumu?

b. Daraja la Kigamboni halijengwi kwa fedha za "NSSF" tu; kumbuka NSSF siyo taasisi "binafsi" bali ni taasisi ya umma. Na haijengi daraja kutokana na maamuzi yake yenyewe bali kutekeleza sera ya muda mrefu ya CCM ya kuunganisha Kigamboni. Je, kuna ulazima wa kujenga daraja la Kigamboni wakati kuna pantoon na kuna uwezo wa kupita nchi kavu - japo kwa kuzunguka - kufika huko?


c. Je kuiunganisha Zanzibar kunaweza naamini kuvunja sana fikra za "ukisiwa" na kutengana ambazo zimekuwa zikilazimishwa sana. As a matter of fact naamini kujengwa daraja kutafisha fikra hizo kwani za hii mentality ya kujitenga inachangiwa sana na hizi hisia za ukisiwa.
 
Gharama za daraja zitakuwa kiasi gani na zitarudishwaje?

Kujenga daraja ndio kutatupa matumizi bora kabisa ya fedha hizi?

Nimetumia mifano hapo juu kuwa daraja la China na hata hili linalopendekezwa la Saudia yamegharimu dola bilioni 3! Ukifikiria sana siyo hela nyingi kihivyo! Two years ago Tanzania imetumia dola bilioni 1 kwa ajili ya stimulus package! In the past decade we have lost almost 10 billion USD katika corruption!

Binafsi siamini kama tatizo ni fedha! We don't have that problem at all.
 
Nimetumia mifano hapo juu kuwa daraja la China na hata hili linalopendekezwa la Saudia yamegharimu dola bilioni 3! Ukifikiria sana siyo hela nyingi kihivyo! Two years ago Tanzania imetumia dola bilioni 1 kwa ajili ya stimulus package! In the past decade we have lost almost 10 billion USD katika corruption!

Binafsi siamini kama tatizo ni fedha! We don't have that problem at all.

Mitanzania itakwenda kupanga nyanya darajani kama lile la manzese, daraja litakufa kwa acid tu ya nyanya na ndimu. Bado huko. Waweke la kawe tu (old Bwagamoyo road) kwanza linatusumbuwa kwa foleni, wewe unasema la Unguja? unavuta eeenhh?
 
Back
Top Bottom