DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Oohhh, mleta mada, kwanini hau invest wewe ukaweka hilo daraja? litajilipa tu.
 
Nimetumia mifano hapo juu kuwa daraja la China na hata hili linalopendekezwa la Saudia yamegharimu dola bilioni 3! Ukifikiria sana siyo hela nyingi kihivyo! Two years ago Tanzania imetumia dola bilioni 1 kwa ajili ya stimulus package! In the past decade we have lost almost 10 billion USD katika corruption!

Binafsi siamini kama tatizo ni fedha! We don't have that problem at all.

Hujajibu swali, hujatuambia kuna kina kirefu gani, kitakachohitaji daraja liwe la teknolojia gani, itakayogharimu kiasi gani, ambacho safari za kwenda Zanzibar sasa hivi kwa boat zikibadilishwa na kufanywa kwa daraja tutafaidika vipi na biashara itaongezeka vipi na ni muda gani utapita kabla ya hizo fedha hazijarudishwa.

Sio tunaiga tembo kunya wakati biashara hatuna, fedha hatuna, na chache tulizonazo zina mambo mengine mia kidogo yenye umuhimu mkubwa zaidi.

China inaweza kuwa na sababu nyingi za kujenga daraja, hata kama hakuna sababu za kibiashara sana, China ina haki ya kutaka kuonyesha economic and technological might kujenga hili daraja. Jana nilikuwa nasoma WSJ Wa-Nigeria wanahamisha fedha za reserve Central Bank yao kutoka USD kwenda Chinese Yuan pole pole. Soma habari hapa.Sie tunaweza kusema hivyo?

Kitu gani hasa kinachohitaji umuhimu wa daraja wakati watu hawana umeme, elimu, makazi, madawa etc?
 
hivi kuna Mtu humu anaweza kufikiria kuwa kujenga daraja kama hili linawezekana hapa Bongo??. Kama mradi utakadiriwakuwa 1.5 trn likiisha utaambiwa zimetumika 10trn . Tunashindwa na vitu kama madawati umeme leo uje kufikiria kitu kama hiki
 
Inawezekana kabisa. Tatizo hatuna ujasiri wa kuthubutu yale ambayo yanaonekana ni magumu.
 
Hujajibu swali, hujatuambia kuna kina kirefu gani, kitakachohitaji daraja liwe la teknolojia gani, itakayogharimu kiasi gani, ambacho safari za kwenda Zanzibar sasa hivi kwa boat zikibadilishwa na kufanywa kwa daraja tutafaidika vipi na biashara itaongezeka vipi na ni muda gani utapita kabla ya hizo fedha hazijarudishwa.

miye nimetoa udadisi na uchokozi tu; la umbali nilishaweka huko nyuma (ni chini kidogo ya daraja hilo la China); suala la Kina kuna mtu alishawahi kuandika -rejea posts za awali.
 
Kitu gani hasa kinachohitaji umuhimu wa daraja wakati watu hawana umeme, elimu, makazi, madawa etc?

Swali zuri lakini siyo sahihi; kwani China wananchi wote wana umeme, elimu, makazi na madawa? India yenyewe wanajenga ile ring ya barabara kuzunguka Delhi lakini haina maana India watu wote wanaishi peponi. Wamarekani walipojenga hizi interstate highways miaka ya 1950s haina maana watu wote wa Marekani walikuwa wanaishi maisha mazuri - wengi walikuwa hata haki ya kupiga kura hawakuwa nayo! Kuwepo kwa matatizo mengine siyo sababu ya kutofanya mambo makubwa! Vinginevyo, tusijenga kabisa barabara au madaraja mengine hadi tuhakikishe kila mtu ana elimu, nyumba na chakula kizuri.
 
Bora tujenge daraja au kuweka ferry ya uhakika kwenda mafia tupafungue kiutalii..mafia ni yetu na siyo znz ambao nationalistic tendencies ziko juu sana ni muungano uliounganishwa kwa mawazo ya watu wawili watatu..kwa ukweli huu muungano siyo sustainable kabisa vizazi vijavyo havitaubeba huu ujinga..
 
MJJ, Wazo changamoto lakini lina matatizo mengi kuanzia ya kiufundi hadi ya kiupendeleo. Kiufundi ni vigumu sana kujenga daraja kwenye deep ocean kwa umbali mkubwa.

  1. Utahitaji piles foundations kubwa na za gharama sana, ndio maana hata kuchimba mafuta huko kwenye deep ocean ni kugumu/gharama. Daraja la China na lile la US yaliyo marefu sana (running miles), yako kwenye maeneo ya vina vifupi ukilinganisha na open sea yetu.
  2. Traffic volume/count ya kuhitaji hilo daraja sidhani kama ipo, magari 1000 kwa siku pia sidhani kama yatafika. Daraja litakuwa a white elephant. Znz ni padogo sana (kiuchumi na population).
  3. Tuna maeneo mengine ambayo hiyo pesa ingeweza kutumika vema zaidi na ikainua uchumi haraka. Km, pipeline ya mafuta na gesi, barabara ya lami na kujenga reli kuunganisha DRC, Rwanda, Burundi na Uganda na bandari zetu ni muhimu zaidi kuliko hilo daraja.
  4. Kupanua na kurutubisha (modernize) bandari zetu au kujenga mpya ingekuwa bora kuliko daraja la ZNZ.
  5. Kuhakikisha tunakuwa na umeme wa kutosha na ulio bora ili wanaotaka kuanzisha viwanda waweze kuwa na uhakika na investments zao.
  6. Kusambaza optics fiber nchi nzima ingeinua na kurahisisha mawasiliano (simu, internet n.k) ambako ulimwengu ndio unakoelekea. Hii ina faida nyingi zadi ya mawasiliano.
Kwa kifupi ni kwamba, given U$2bil, TZ kuna mengi ambayo tunaweza kufanya lakini huwa tunazinywa au tunachagua mabaya. Kwa mfano tumetumbua zaidi ya U$300mil kwa Twin towers ambazo zingegharimu around U$80million, almost 400%.
 
Hivi mnafikiria huko China hakuna ufisadi? Au China viongozi wote ni wazuri na wazalendo?

ndugu yangu hakuna serikali ambayo ni clean kwa 100%. lakini pale inapotokea mambo makubwa kama yaha yana-outway ufisadi uliopo, ni jambo la faraja sana. think big ndugu!!!!!!
 
Swali zuri lakini siyo sahihi; kwani China wananchi wote wana umeme, elimu, makazi na madawa? India yenyewe wanajenga ile ring ya barabara kuzunguka Delhi lakini haina maana India watu wote wanaishi peponi. Wamarekani walipojenga hizi interstate highways miaka ya 1950s haina maana watu wote wa Marekani walikuwa wanaishi maisha mazuri - wengi walikuwa hata haki ya kupiga kura hawakuwa nayo! Kuwepo kwa matatizo mengine siyo sababu ya kutofanya mambo makubwa! Vinginevyo, tusijenga kabisa barabara au madaraja mengine hadi tuhakikishe kila mtu ana elimu, nyumba na chakula kizuri.

nimeamini kuwa kweli watu wengi bado tuko kwenye enzi za ujima. unaweza kushangaa watu wengine wanawaza kwa kutumia nini!!!!!!!!!!!!!
 
MJJ, Wazo changamoto lakini lina matatizo mengi kuanzia ya kiufundi hadi ya kiupendeleo. Kiufundi ni vigumu sana kujenga daraja kwenye deep ocean kwa umbali mkubwa.

  1. Utahitaji piles foundations kubwa na za gharama sana, ndio maana hata kuchimba mafuta huko kwenye deep ocean ni kugumu/gharama. Daraja la China na lile la US yaliyo marefu sana (running miles), yako kwenye maeneo ya vina vifupi ukilinganisha na open sea yetu.
  2. Traffic volume/count ya kuhitaji hilo daraja sidhani kama ipo, magari 1000 kwa siku pia sidhani kama yatafika. Daraja litakuwa a white elephant. Znz ni padogo sana (kiuchumi na population).
  3. Tuna maeneo mengine ambayo hiyo pesa ingeweza kutumika vema zaidi na ikainua uchumi haraka. Km, pipeline ya mafuta na gesi, barabara ya lami na kujenga reli kuunganisha DRC, Rwanda, Burundi na Uganda na bandari zetu ni muhimu zaidi kuliko hilo daraja.
  4. Kupanua na kurutubisha (modernize) bandari zetu au kujenga mpya ingekuwa bora kuliko daraja la ZNZ.
  5. Kuhakikisha tunakuwa na umeme wa kutosha na ulio bora ili wanaotaka kuanzisha viwanda waweze kuwa na uhakika na investments zao.
  6. Kusambaza optics fiber nchi nzima ingeinua na kurahisisha mawasiliano (simu, internet n.k) ambako ulimwengu ndio unakoelekea. Hii ina faida nyingi zadi ya mawasiliano.
Kwa kifupi ni kwamba, given U$2bil, TZ kuna mengi ambayo tunaweza kufanya lakini huwa tunazinywa au tunachagua mabaya. Kwa mfano tumetumbua zaidi ya U$300mil kwa Twin towers ambazo zingegharimu around U$80million, almost 400%.

Mkuu naona umeconclude mjadala huu, tunakushukuru kwa hilo. Kujenga daraja kwenda Zenji hailipi kabisaaaaaa! Mnaotaka kwenda huko jipandieni vidau tu, manake meli zao mbovu hawazikaguagi.
 
Ni wazo zuri ila halitalipa maana hamna economic activity ya maana btn znz na bara kujustify hiyo investment. Ningekubaliana na wewe kama lingejengwa daraja juu ya lake tanganyika kuunganisha tz na drc congo. Kwa kule kuna biashara na italipa gharama za uwekezaji.
 
Back
Top Bottom