Hivi kinachokutisha wewe ni gharama au nini?
Maana sababu ya kujenga ipo wazi kabisa, na uwezo tunao pia..
Tunachosema hapa ni kwamba pamoja na kwamba tunahitaji shule, vyuo na railways..
Tunahitaji daraja la umoja kutoka zanzibar hadi tanganyika..pia
Ni swala la kuajdili ipi ianze..kwangu mimi zote zina umuhimu ulio sawa lolote litakaloanza ni sawa tu..
tujenge daraja bana
Kuna picha za kina Rembrandt kibao ziko museums za Ulaya zinauzwa, kama swala ni kufanya kitu cha kifahari tunaweza kuzinunua kuzining'iniza, si ni m project mkubwa nao? tena hiyo mipicha haitakuwa na gharama kubwa ya ukarabati.
Mimi naangalia, unapojenga daraja licha ya kujenga daraja tu, kuna shughuli gani ya kiuchumi itakayo justify ujenzi wa daraja hilo?
Kama kungekuwa na kisiwa kina mlima wa almasi huko mie mara moja ningekwambia jenga madaraja hata matano, moja linatokea Tanga, lingine Pwani, lingine Kunduchi, lingine kuanzia City Centre na lingine linatoka Rufiji kupitia mafia kuunga Unguja na Pemba. Ili kusudi ndugu zetu wenye kuchanja chale mbili wakijisikia hata kutembea kutoka Msanga mpaka P[emba, kwa kupitia Mafia, waweze. Si wanaenda kukata mlima wa almasi bwana? na waende tu, hizo gharama zitarudishwa mwaka mmoja tu.
Sasa Zanzibar sijakataa kujenga daraja, nataka mnionyeshe namba zinazomake sense hapa.
Kuanzia jinsi gani mtaiweka miguzo kwenye channel pale kwa kulinganisha walivyofanya wachina na channel yetu, mpaka hicho mtakachofanya Zanzibar na watu wa Zanzibar watakachofanya bara kikubwa ambacho sasa hivi hakiwezekani!
Tusiongee utopia ya kutaka kufanya vitu kama vile all our other needs can be stopped.
Kuna kina babu na bibi wa East African community wanajifia wanaikosesha nchi radhi hawajalipwa mafao mpaka sasa.
Sio kwamba sitaki vitu vizuri na vikubwa (I am contemplating that new Evoque by the way) lakini vitu vyenyewe vi make sense basi. Mie najua budget yangu hata leo nikiamua kununua Evoque naweza, bila kubana kitu kingine chochote. Lakini bado nafikiri mara mbili mbili, jamani hili Evoque nalipenda liko relatively fuel efficient when it comes to Range Rovers etc, lakini nalihitajio au nalitaka tu?
Do I need the Evoque or do I just want it?
Hili daraja tunalihitaji au tunalitaka tu?
Y'all need some Suzie Orman in your lives.
Muungano wenyewe unavunjika keshokutwa, mtatalikiana na deni halafu mbakie na uhasama nani atalipa!!!