Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo wakishinikiza kuwa hawataki Kanisa katika eneo lao.
Hii ni kunyume kabisa na sheria za nchi zinazoruhusu Uhuru wa Kuabudu. Kama jambo halitafanyika basi ni wazi kuna kiongozi mbaguzi wa dini anaewalinda wabomoaji na pia hii itachochea sehemu nyingine makanisa na makazi ya wachungaji kubomolewa.
Pia miezi michache ijayo kipindi cha mfungo kikianza huwa ni marufuku kwa wakristo kula sehemu za wazi, ukikutwa unafungwa mpaka mfungo uishe, wengine huwa wanapigwa sana, sasa hapa ni kwamba mtu kama umeamua kufunga kwa imani yako iwaje hutaki kuona wenzako hawali, ni kwamba imani yako no nyepesi sana kuisimamia, kama ni hivyo kuna haja gani ya kufunga.
View attachment 2146530
View attachment 2146523
============================================
Taarifa uhakika juu ya tukio hilo ni kuwa Mchungaji
David Victor Suna ni mzaliwa wa Sumbawanga, lakini kwa miaka mingi amekuwa akiishi Zanzibar baada ya familia yake kuhamia huko. Kaka yake naye ni mtu wa kanisani lakini anafanya shughuli zake Dar es Salaam.
Alipoanza harakati za kutafuta eneo kwa ajili ya kanisa alipata wakati mgumu kwa kuwa walikuwa wanamkatalia, baadaye akabadili gia na kutafuta eneo la kununua la kwake binafsi na siyo kwa ajili ya kanisa.
Baada ya kutafuta eneo lake binafsi ndipo akapata eneo hilo lililopo Sebleni, Unguja. Akanunua kwa Sh 16,000,000 (milioni 16) akalipa fedha taslimu, akasaini mkataba rasmi wa mauziano (tazama picha), japokuwa katika eneo hilo alikuta mmiliki tayari amejenga banda ambalo nalo lilikuwa sehemu ya mkataba wa manunuzi.
Baada ya kununua akajenga ukuta kuzungushia eneo husika kisha akaanza shughuli zake za ibada, baada ya majirani kubaini kuwa mnunuzi ameanzisha kanisa eneo hilo ndipo mgogoro ulipoanzia.
Wakamwabia hatakiwi kuwa na kanisa eneo husika lakini David Victor Suna akashikilia msimamo wake kuwa ataendelea na shughuli zake za kanisa.
Mhusika ambaye aliuza eneo hilo naye akamvaa David Victor Suna na kumtaka arejeshe eneo hilo kwa kuwa hakuuza kwa ajili ya kanisa bali kwa ajili ya kujenga makazi, bado David Victor Suna akagoma kubadilisha matumizi wala kurudisha eneo.
David Victor Suna akawa asisistiza kuwa yeyote mwenye malalamiko aende Mahakamani ambapo haki itatendeka, hata waliposhirikisha Serikali za mtaa nao wakawa wanamshawishi ama kubadili matumizi au kurejesha eneo, msimamo ukawa ni uleule.
Ndipo siku ya tukio, lilikuka bulldoza likaanza kuvunja eneo husika wakati wahusika wakiwepo wachache wakiendelea na ibada kama kawaida, kanisa likavunjwa na baadhi ya vitu vikiwemo viti vikaharibiwa na gari hilo.
Mamlaka za Serikali za mtaa hazijawa tayari kuzungumzia tukio hilo, naye David Victor Suna amekuwa mgumu kuzungumzia kinachoendelea kwa kile kinachodaiwa hajatulia hadi sasa.
SERIKALI YAINGILIA
Taarifa zinaelezwa kuwa Mkuu wa Wilaya wa eneo husika anatarajiwa kutolea ufafanuzi suala hilo mchana wa leo Machi 11, 2022.
Nitarudi kuwapa kilichoendelea kuhusu tamko la Serikali.
ITAENDELEA...
View attachment 2146667
View attachment 2146668
View attachment 2146670
View attachment 2146671 View attachment 2146672