Zanzibar kufuta mitihani ya Taifa na kuwa na Mfumo Mpya wa Elimu

Zanzibar kufuta mitihani ya Taifa na kuwa na Mfumo Mpya wa Elimu

Sijakuelewa, funguka zaidi.
Siku ikiingia serikali nyingine itabadirisha mfumo tena, yani hakuna mfumo rasmi wa elimu, kila ajaye anafanya anavyoona ni sawa kwake. Hakuna tafiti wala majaribio ya mifumo hii mipya inayopendekezwa.

Watasema North Korea wanafanya hivyo, China,na Urusi wana fanya hivyo, basi nasi tunafanya hivyo. Nchi ngumu sana hii.

Nakumbuka huku Bara, mifumo imeshabadirishwa hata sijui huwa wana weka record au la, Profesor kapuya alikuja na yake, Mungai naye alikuja na yake, Dr. Shukuru Kawambwa alikuja na yake, Dk.Ndalichako alikuja na yake, sasa tunaye huyu mpya naye ana yake.

Sijui kwa huko Zanzaibar, lakini hili la kubadili mifumo ya elimu kila siku ni kuwasumbua watoto wetu bila sababu za msingi.
 
Kunapokuwa na mitaala tofauti , je Wanafunzi wa Zanzibar watatathminiwa sawa na wa Bara wakati wanaomba nafasi za kusoma vyuo huku Bara? au ndiyo itakuwa 'upendeleo maalumu wa 21%'
 
Nadhani haya mageuzi ya Elimu yalichelewa sana. Ndio naana tuna tatizo kubwa la ajira yaani kijna anasoma kuanzia darasa la kwa hadi chuo kikuku anatoka hana ujuzi wowote wakati huo huo anajiona msomi anadharau wakulima na wafugaji wakati yeye kulima hajui, kufuga hajui na elimu enyewe ni ya mashaka mashaka.
 
Kunapokuwa na mitaala tofauti , je Wanafunzi wa Zanzibar watatathminiwa sawa na wa Bara wakati wanaomba nafasi za kusoma vyuo huku Bara? au ndiyo itakuwa 'upendeleo maalumu wa 21%'
Hili halina tatizo. Hivi sasa Watanzania wanaomba masomo nchi zote duniani nao wamefanya mitihani ya Tanzania kwa mitaala ya Tanzania. Muhimu mitaala ikidhi vigezo na iwe na kiwango kinachokubalika.
 
Siku ikiingia serikali nyingine itabadirisha mfumo tena, yani hakuna mfumo rasmi wa elimu, kila ajaye anafanya anavyoona ni sawa kwake. Hakuna tafiti wala majaribio ya mifumo hii mipya inayopendekezwa.
Watasema North Korea wanafanya hivyo, China,na Urusi wana fanya hivyo, basi nasi tunafanya hivyo. Nchi ngumu sana hii. Nakumbuka huku Bara, mifumo imeshabadirishwa hata sijui huwa wana weka record au la, Profesor kapuya alikuja na yake, Dr. Shukuru Kawambwa alikuja na yake, Dk.Ndalichako alikuja na yake, sasa tunaye huyu mpya naye ana yake.
Sijui kwa huko Zanzaibar, lakini hili la kubadili mifumo ya elimu kila siku ni kuwasumbua watoto wetu bila sababu za msingi.
= itabadilisha.
= imeshabadilishwa.

Binafsi naamini katika kusoma, siyo kusomeshwa. Haijalishi ni mfumo upi unatumika au utatumika au umeletwa na nani. Kama hatujasoma wenyewe hatutaelimika.

Mgfumo pekee ambao unamuelimisha mtu na unamfanya kila mmoja asome ni wa madrassa.
Unaufahamu mfumo wa madrassa?
 
Hii mbona ilishatangazwa na waziri wa Elimu Wa JMT alisema pia Kwa sasa Shule za Msingi watasoma mpaka Darasa la sita na Kuingia moja kwa moja Form one.

Pia alisema kuwa kutakuwa na mafunzo ya amali kama muziki na elimu ya kazi secondary na hakuna haja ya mtu kusma ma Physics wala ma Chemistry wala ma history.

Kama huu mtaala utafanikiwa nitakuwa wa kwanza kuipongeza Serikali ya CCM rasmi
Kusomea hizo fani ni kwa muda gani na ni kwa kipindi kipi hasa? Baada ya kumaliza darasa la 6
 
Kunapokuwa na mitaala tofauti , je Wanafunzi wa Zanzibar watatathminiwa sawa na wa Bara wakati wanaomba nafasi za kusoma vyuo huku Bara? au ndiyo itakuwa 'upendeleo maalumu wa 21%'
wanafunzi wa Zanzibar ni vilaza sana,tangu kuanzishwa kwa benki kuu, deputy govenor alipaswa awe Mzazibari mwenye PhD ya finance,hawakuwa nae for more than 30 years hadi alipopatikana Juma Reli.

Kwenye elimu ya darasani, Wazanzibari ni vilaza sana, shuhudia hapa Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!. hivyo kwenye elimu ya juu, wanapewa kwa mserereko wa quota ya 4.5% percentage .
P
 
wanafunzi wa Zanzibar ni vilaza sana,tangu kuanzishwa kwa benki kuu, deputy govenor alipaswa awe Mzazibari mwenye PhD ya finance,hawakuwa nae for more than 30 years hadi alipopatikana Juma Reli.

Kwenye elimu ya darasani, Wazanzibari nvilaza sana
P
Mkuu, hili si jambo la hatari?
Kwa maana wanapewa 21% ya nafasi za kazi za Tanganyika popote. Si nafasi za Muungano ni pamoja na za Tanganyika
 
Mkuu, hili si jambo la hatari?
Kwa maana wanapewa 21% ya nafasi za kazi za Tanganyika popote. Si nafasi za Muungano ni pamoja na za Tanganyika
Kuna Tanzania na Zanzibar, hakuna Tanganyika. Hivyo Wazanzibari wanastahili nafasi stahiki kama Watanzania wengine wote, kisha wao wana nafasi za ziada za asilimia 4.6% kama Wazanzibari.
P
 
Kuna Tanzania na Zanzibar, hakuna Tanganyika. Hivyo Wazanzibari wanastahili kama Watanzania, na ziada kama Wazanzibari.
P
..... "wazanzibari wanastahili kama watanzania, na ziada kama wazanzibari"

Ajabu bado wanalalamika hawautaki muungano, kumbe ni kwasababu wengi wao ni wajinga wasioweza kuzitumia hizo nafasi za upendeleo walizopewa.
 
Kuna Tanzania na Zanzibar, hakuna Tanganyika. Hivyo Wazanzibari wanastahili nafasi stahiki kama Watanzania wengine wote, kisha wao wana nafasi za ziada za asilimia 4.6% kama Wazanzibari.
P
Hii Tanzania inaundwa na nani? Na kwanini kuwe na nafasi za Zanzibar?
Masahihisho ni 21%

Pili, ikiwa unasema ni 'Vilaza' huoni kuna hatari kupitia nafasi maalum
 
..... "wazanzibari wanastahili kama watanzania, na ziada kama wazanzibari"

Ajabu bado wanalalamika hawautaki muungano, kumbe ni kwasababu wengi wao ni wajinga wasioweza kuzitumia hizo nafasi za upendeleo walizopewa.
Usiwatukane wajinga, ni vilaza tuu wa elimu ya darasani tuu ndio ma zero
yamepangana, lakini ni very bright and brilliant kwenye mambo mengi mengine zikiwemo biashara
P
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya mageuzi makubwa ya mfumo wa elimu kuanzia sasa hivi. Watakuwa na mpango wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Katika mipango hiyo kuna mitihani ya Taifa ambayo itafutwa kabisa. Hawaoni sababu ya kuwepo kwa mfumo wao mpya wa elimu.

Jinsi nilivyolisikiliza tamko hili (video chini) la awali, inaonesha kama ni mipango mizuri. Watakuwa na mafunzo ya amali kuanzia mapema, yaani wanafunzi watafundishwa fani mbali mbali za kazi wakati wanaendelea na masomo yao mengine, na si kama ilivyo sasa kwa Zanzibar, kuwa mwanafunzi mpaka amalize kwanza form four ndiyo aweze kwenda vyuo vya kazi. Jisikilizie ufafanuzi zaidi:

Ni mambo ya kujidanganya tu. Wanafeli sana kwasababu watoto hawasomi halafu badala ya kutatua tatizo wame tafuta njia ya kuficha.

Nilienda Ilboru 2022 pale wanafunzi ni lazima wasome hata weekend masaa matatu jumamosi na jumapili sasa wenzetu wanaolesha watoto, kazi za ndani na kushinda kupiga zogo. Hii haitasaidia jamii ni wazo baya sana
 
Hii Tanzania inaundwa na nani
Tanzania ni nchi moja yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, ambapo raia wote wa Tanzania wakiwemo Wazanzibari wana haki sawa bin sawa ila Wanzanzibari kwasababu ni the minority wana haki za ziada za Wazanzibari wakaazi ambazo ni special and specific kwa Wazanzibari pekee.
Na kwanini kuwe na nafasi za Zanzibar?
Masahihisho ni 21%

Pili, ikiwa unasema ni 'Vilaza' huoni kuna hatari kupitia nafasi maalum
Kuna nafasi special za Wazanzibari kwasababu ni the minority. Hesabu ninayoitambua mimi ni asilimia 4.5%, hiyo 21% siijui wala sijui ilifikiwaje.

Yes Wazanzibari ni vilaza kwa elimu ya darasani compared to Watanzania bara, Shule za Zanzibar, zero zimeongozana, ila Wazanzibari ni wazuri sana tuu katika maeneo mengine mengi
P
 
Tanzania ni nchi moja yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, ambapo raia wote wa Tanzania wakiwemo Wazanzibari wana haki sawa bin sawa ila Wanzanzibari kwasababu ni the minority wana haki za ziada za Wazanzibari wakaazi ambazo ni special and specific kwa Wazanzibari pekee.
Huu ni mjadala tofauti, ninachoweza kusema ni kwamba neno Tanzania linatumiwa vibaya ili kuipa nafasi Zanziar ku abuse Muungano. Watu 1.5 wanapewa 9% ya Bajeti(kwa mujibu wao wenyewe). Kwamba 2023/24 ni 49 Trilioni na Zanzibar watapewa almost 4.2 Trilioni wakati Bajeti yao ni 2.8Trilioni.
Swlali wana invest nini katika Muungano? Zero halafu wanapata resorce kwa Uzanzibar
Kuna nafasi special za Wazanzibari kwasababu ni the minority. Hesabu ninayoitambua mimi ni asilimia 4.5%, hiyo 21% siijui wala sijui ilifikiwaje.
Waziri Mohamed Mchengerwa akiwa katika Wizara ya Muungano alitangaza. 21% bila kujali ni za eneo gani!
Yes Wazanzibari ni vilaza kwa elimu ya darasani compared to Watanzania bara, Shule za Zanzibar, zero zimeongozana, ila Wazanzibari ni wazuri sana tuu katika maeneo mengine mengi
P
21% inatuathiri , ama sivyo?
 
Ni mambo ya kujidanganya tu. Wanafeli sana kwasababu watoto hawasomi halafu badala ya kutatua tatizo wame tafuta njia ya kuficha.

Nilienda Ilboru 2022 pale wanafunzi ni lazima wasome hata weekend masaa matatu jumamosi na jumapili sasa wenzetu wanaolesha watoto, kazi za ndani na kushinda kupiga zogo. Hii haitasaidia jamii ni wazo baya sana
Oooh hodari sana wewe. Kusoma kwako kumeisaidia nini jamii inayokuzunguka?
 
Hili halina tatizo. Hivi sasa Watanzania wanaomba masomo nchi zote duniani nao wamefanya mitihani ya Tanzania kwa mitaala ya Tanzania. Muhimu mitaala ikidhi vigezo na iwe na kiwango kinachokubalika.

Mkuu huyo jamaa ana chuki binafsi sana mchukulie tu
 
Waangalie kilicho bora kwao, mimi nadhani kwa udogo wao wa kijiografia, idadi ya watu na harakati zao za kiuchumi wala hawahitaji wasomi wengi ki vile watasababisha tatizo la ajira bure! watafika tu, hata sisi wenyewe pamoja na makelele yote haya hatujafika mbali!... eti nchi ya watu milioni 65 tunajilinganisha na Zanzibar kielimu badala ya KENYA au UGANDA, GHANA SOUTH AFRICA etc. Utamsikia msomi 'shule za Zanzibar ni za mwisho kimatokeo sisi tunafanya vizuri' what a shame!

wi ujinga tu unaousumbua watu, Zanzibar Kijografia walivyo pamoja na idadi yao wakipata viongozi makini kidogo wanaweza kuisha Mbali sana Tanganyika kimaendeleo na wasomi wao.
 
Back
Top Bottom