Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Ujinga uliopitiliza. Huo mchakato ulifanyika lini? Nani waliamua hayo na kwa manufaa gani?
Mzee mwanzo wa ngoma ni lele. Hii nchi ina mambo mengi yanayofanyika chini ya kapeti. Yakishaparaganyika ndipo unaanza kusikia TUME za uchunguzi. Kikubwa ni Serikali kulitolea ufafanuzi na kuliweka sawia.
 
Kuanzia miaka hiyo mpk leo na hatujui mkataba ule upoje,wanyama wanapakiwa kwenye ndege huko huko kimya kimya,watanzania tunaendaga kufanya vibarua vya ujenzi mkuu,Pori la Loliondo ni nchi ya muarabu
Mimi huwa nasema hatujawahi kupata viongozi bali midude tu ya kutawala na kujineemesha. Wote toka awamu ya 1 mpaka hivi leo. Usiri usiri tu shenzi sana hawa watu, kana kwamba wao ndio wana haki sana na hii nchi.
 
Ile kauli ya kupigwa mnada ya masta Ndugai isije kuwa kweli tu jamani.

Ibakie tu kwamba vinakodishwa na tusiwape wageni ardhi yetu.
Huu uzi ni mzuri sana Kwa kutupa elimu

Lakini kauli kama hizi zitauharibu

Je Unajua kwamba hata bara kuna visiwa vimeshawahi iukodishwa?
 
Mkuu umeenda Serengeti?
Ambapo huko kuna hoteli (tented camp), unalipa $3,290 kwa siku?
Hata kupatazama tu hujiruhusu mwenyewe!
 
Kuna wazanzibar wamepata ajira kutokana na uwekezaji wa Bill?
 
Msiishie huko tu.
Hata huku bara bora nchi iiuzwe KILA mmoja afe na chake mmkononi.
Maana hatuoni tumaini kabisa toka serikali hii ya ccm.
 
Yaani uzi wako upotoshe umma halafu walaumiwe serikali?? Kwani tulipoambiwa tuwe wazalendo maana yake ni nini?? Maana yake ni kuacha kuripoti uongo na ubaya unaohusu nchi zetu na watu wake.

Nchi zisizotutakia mema zinatuchafua, sisi tusiingie katika mtego wa kujichafua wenyewe.

Halafu pili, ni nani aliekwambia raia wa Tanzania hawaruhusiwi kwenda ku-lease hivyo visiwa?? Just for your information, mtu yoyote asie mzanzibar atapewa hivyo visiwa akikidhi vigezo kwa kukodishwa. Mnyamwezi atakodi, msukuma atakodi pia sasa wewe ni nani aliekwambia hao raia wa Tanzania hawajapewa kipaumbele?? Na ni nani pia kakwambia tahadhari kubwa haichukuliwi???

Mkuu, una elimu yoyoyte ya mambo ya mikataba?? Law of contract?? Huu ni mkataba na una masharti yake, ukikiuka kuna vipengele vinavyozungumzia hilo. Wasiwasi uko wapi?? Hilo la vipengele vya siri sasa ulizungumzie wewe ulielileta.

Msimamo wako baki nao, serikali ni uwakilishi wa watu. Serikali ya Zanzibar ni uwakilishi wa Wazanzibari na wao wanafanya kwa maslahi ya Wazanzibari.
 
Hili nalo ni jambo zuri na zito..ni vizuri mkuu akalisemea vizuri kwamba maslai yake kwa serikali ya Zanzibar na ya Muungano ni yapi kwasababu limeshaleta sintofahamu..Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Mnaanza sasa! Serikali ya Zanzibar na ya Muungano kivipi yaani???

Hahahaahahhaha
 
Shukran mkuu, kuhusu maswali yako ni kama ifuatavyo

1) naomba muda ntakujibu kuhusu mpango wa matumizi ya kodi ya iliyopatikana kutoka kwenye visiwa vilivyokodishwa tayar.

2) wananchi wanazo taarifa, mimi ni mwananchi wa kawaida na ninazo taarifa kwamb visiwa vinakodishwa kwa kuanzia miaka 33 mpaka 99 maximum.

3) Mambo haya hayajakuwa siri. Yanatolewa taarifa kila uchao.


Mkuu, epuka hawa watu wanajifanya wajuaji na wapingaji wa kila kitu. Vijana wa ki-leo Sisi tumekuwa wapuuzi sana ndio maana watu kama kina mkuchika itabidi waendelee kuteuliwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…