Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Zanzibar ni sehemu ya JMT, kwa maana ya kuuzwa kwa kipande cha ardhi ndani ya JMT ina maana gani kwa mamlaka ya JMT?
Je watu wanaonunua visiwa hivyo watatawalwa kwa sheria zipi? za JMT, SMZ, au za nchi zao?
Fuatilia vizuri juu ya hili mkuu.

Tunasema hivi, Zanzibar ni nchi kamili na ina mamlak na ardhi yake. Tunasema hivyo kwa vitendo na hatusemi kwa maneno maneno tu.

Halafu nikuweke tu sawa, hakuna kipande cha ardhi kinachouzwa. JMT kuna mambo itaiachia Zanzibar ili ifanye inavyoona inafaa kwa Wazanzibari.
 
Huu uzi ni mzuri lakini nina hofu usije ukatumika kupotosha.

Umeuweka kwenye mtindo wa swali. Jibu ni kwamba, visiwa hivyo vinakodishwa na wala haviuzwi.

Sisi tumekwenda Mnemba mara kadhaa na hata wanajamii wenzetu wanakwenda.

Ni maamuzi mazuri yaliyofanya na SMZ na mimi kama Mzanzibar nayaunga mkono.
Rabika
 
Habari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha. Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.... Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!

Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha

Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!

Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).

Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?

Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
Ule uchaguzi ulitumia pesa nyingi sana. Wanafukia mashimo.
 
Nadhani uko sahihi ila mleta uzi ameuliza maswali ambayo mimi naona yanapaswa kupatiwa majibu. Baadhi ya maswali hayo ni: 1. Pesa za mauzo/kodi ya hivyo visiwa zinafanyiwa nini? 2. Mbona wananchi hawaambiwi? 3. Mbona mambo haya yamekuwa siri? Nadhani haya maswali yanapaswa kujibiwa.
Pesa hizo zikijulikana zinakoenda mnishtue.
 
Yaani uzi wako upotoshe umma halafu walaumiwe serikali?? Kwani tulipoambiwa tuwe wazalendo maana yake ni nini?? Maana yake ni kuacha kuripoti uongo na ubaya unaohusu nchi zetu na watu wake.

Nchi zisizotutakia mema zinatuchafua, sisi tusiingie katika mtego wa kujichafua wenyewe.

Halafu pili, ni nani aliekwambia raia wa Tanzania hawaruhusiwi kwenda ku-lease hivyo visiwa?? Just for your information, mtu yoyote asie mzanzibar atapewa hivyo visiwa akikidhi vigezo kwa kukodishwa. Mnyamwezi atakodi, msukuma atakodi pia sasa wewe ni nani aliekwambia hao raia wa Tanzania hawajapewa kipaumbele?? Na ni nani pia kakwambia tahadhari kubwa haichukuliwi???

Mkuu, una elimu yoyoyte ya mambo ya mikataba?? Law of contract?? Huu ni mkataba na una masharti yake, ukikiuka kuna vipengele vinavyozungumzia hilo. Wasiwasi uko wapi?? Hilo la vipengele vya siri sasa ulizungumzie wewe ulielileta.

Msimamo wako baki nao, serikali ni uwakilishi wa watu. Serikali ya Zanzibar ni uwakilishi wa Wazanzibari na wao wanafanya kwa maslahi ya Wazanzibar
Upo Sahihi mkuu, Mtu yoyote wameruhusu kwenda kuwekeza,kampuni na uandae proposal kabla ya kwenda kuwekeza Kwenye kisiwa unachohitaji.

Wametumia mfumo wa Public Private Partnership (PPP), na unapoomba kuwekeza Kwenye kutuma tenda unatakiwa kudeposit USD 1500 non refundable. Na nimeona mfumo wa Lease Acquisition Cost hii wawekezaji wowote lazima watachangia gharama za tangu mwanzo Mpaka mradi utapofikia.

Zanzibar baada ya miaka michache hivyo visiwa vitakuwa kivutio kubwa cha utalii sawia na visiwa vya wenzetu huko Ulaya na America.
 
Wam
Kuna wazanzibar wamepata ajira kutokana na uwekezaji wa Bill?
Wamepata ajira wangapi wanalipwa kiasi gani. Maana siyo watu walipwe kama watumwa. Je hao walioajiriwa wakiacha kazi baada ya miaka 2 wanaweza waka survive muda gani kwa saving zao. Jamhuri ni Mali ya umma (Res Publica) kuna haja ya kila maamzi hekima na busara vikatumika maana hawa wazungu walishaonyesha hawana nia na sisi. Miaka ya 1903 Cuba leased Guantanamo bay to the US ,and now marekani haitako kuirudisha. Tuwe tu makini kwa tunavyofanya na kuamua leo, maana tunaweza kufanya makosa akawagharimu watoto wakaja kutulaumu. Uzalendo kwanza
 
Upo Sahihi mkuu, Mtu yoyote wameruhusu kwenda kuwekeza,kampuni na uandae proposal kabla ya kwenda kuwekeza Kwenye kisiwa unachohitaji.

Wametumia mfumo wa Public Private Partnership (PPP), na unapoomba kuwekeza Kwenye kutuma tenda unatakiwa kudeposit USD 1500 non refundable. Na nimeona mfumo wa Lease Acquisition Cost hii wawekezaji wowote lazima watachangia gharama za tangu mwanzo Mpaka mradi utapofikia.

Zanzibar baada ya miaka michache hivyo visiwa vitakuwa kivutio kubwa cha utalii sawia na visiwa vya wenzetu huko Ulaya na America.
It's the same approach ambayo Maldives waliichukua some years ago. Leo Sisi hapa watu wanalishwa matango pori tu.

Tutafika lakini
 
Habari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha. Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.... Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!

Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha

Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!

Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).

Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?

Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
Hapo hapo tukumbuke kwamba Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania. Mipaka ya Jamhuri imeainishwa kwa kujumlisha ardhi yote ya Zanzibar na ya Tanganyika. Serikali ya Jamhuri ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutamka kuhusu sehemu yo yote ya ardhi ya Jamhuri. Mahusiano na nchi za nje ni suala la Muungano. Zanzibar hairuhusiwi kuingia mkataba kuhusiana na ardhi yake bila kuihusisha Jamhuri. Kwa mfano haiwezi kuanzisha ubalozi na nchi ambayo haina mahusiano na Jamhuri. Hilo ndilo tatizo lililojitokeza wakati Zanzibar ilipotaka kujiunga na umoja wa nchi za Kiislamu.
 
Wakati mwengine ni Bora kukaa kimya ili kulinda heshima tu!

Sasa hujui chochote kuhusu hili suala, hujui mchakato ulifanyika lini na hujui walioamua ni kina nani na hujui ni kwa manufaa gani lakini bado unaita huo ni ujinga uliopitiliza??

ID yako ina heshima kiasi chake, ni busara pia kuitunza heshima hiyo.
Wewe unaejua sana tuambie hizo hela zilizopatikana zimefanyia nini?

Sijui elimu yako lakini nina uhakika uelewa wako ni mdogo sana juu ya masuala ya sovereignity,eg.umeshindwa kabisa kujua kuwa kuuza ardhi ni sawa na kuuza nchi,uhuru au sawa na kuuza nyumba...na hakuna kurudishiwa ni forever.

Kwa maana nyingine Zanzibar imeuza uhuru wake kwa wageni,unaunga mkono upumbavu huu!?
 
Back
Top Bottom