Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 6,076
- 15,685
NdioKwenye website ya zipa inaweza kuonekana?
NdioKwenye website ya zipa inaweza kuonekana?
Kukodisha au kuuza ni kitu kilekile; mtu anakodi kwa miaka 100 ni vizazi vingapi hivyo vitapita bila kuwa na haki ya kupatumia mahali hapo? Neno kukodisha huwa ni neno laini linalotumiwa kuwapooza wale wanaohoji lakini madhara ya kukodidha kwa wa a chi ni yaleyale sawa na kuuza.Ile kauli ya kupigwa mnada ya masta Ndugai isije kuwa kweli tu jamani.
Ibakie tu kwamba vinakodishwa na tusiwape wageni ardhi yetu.
Yes, haya ndio maswali ya kuuliza.
In short muda wa kuanzia ni miaka 33. Lakini haitozidi miaka 99
Akaulizwe baba yakeNi sawa! Mbona baba yake nae aliipiga bei sehemu ya Loliondo ? Nako ni Zanzibar?
Mtafanya nn watu wana haki ya kutokushtakiwa!Kuanzia miaka hiyo mpk leo na hatujui mkataba ule upoje,wanyama wanapakiwa kwenye ndege huko huko kimya kimya,watanzania tunaendaga kufanya vibarua vya ujenzi mkuu,Pori la Loliondo ni nchi ya muarabu
Nadhani sio uamuzi mbaya kukodisha visiwa. Kwani pesa inayopatikana inakwenda kuendeleza huduma za jamii. Mleta uzi kaja kisiasa zaidi.Huu uzi ni mzuri lakini nina hofu usije ukatumika kupotosha.
Umeuweka kwenye mtindo wa swali. Jibu ni kwamba, visiwa hivyo vinakodishwa na wala haviuzwi.
Sisi tumekwenda Mnemba mara kadhaa na hata wanajamii wenzetu wanakwenda.
Ni maamuzi mazuri yaliyofanya na SMZ na mimi kama Mzanzibar nayaunga mkono.
Umeambiwa Barabara ya Malawi sio ya kwenda Malawi.Zanzibar kuna barabara ya kwenda malawi?
Mkuu, kwa vile wewe unajua hilo suala vizuri sana, ni vyema sasa kumuelimisha huyo ndugu na wengine wengi ambao hili jambo ni mara ya kwanza kulisikia kwa kueleza ukweli wa jambo hilo kama walivyouliza:Wakati mwengine ni Bora kukaa kimya ili kulinda heshima tu!
Sasa hujui chochote kuhusu hili suala, hujui mchakato ulifanyika lini na hujui walioamua ni kina nani na hujui ni kwa manufaa gani lakini bado unaita huo ni ujinga uliopitiliza??
ID yako ina heshima kiasi chake, ni busara pia kuitunza heshima hiyo.
Naamini ushauri wako utafanyiwa kazi kikamilifunashauri Environment impact assement iwe kali TOR ziwe za kimataifa idara ya mazingira wawezeshwe usafir na vifaa vya kuvizungikia mara kwa mara kufanya tathmin
Mbona nyie mmekodisha ardhi watu wachimbe madini wao wapo kimyaaHabari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha. Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.... Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!
Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha
Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!
Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).
Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?
Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
Mkuu,Tafadhali naomba kujua yafuatayo.
= Vinakodishwa kwa muda gani?
= Majenzi yatakayowekwa huko yatakuwa ya aina na ubora gani?
=Baada ya muda wa kukodi kuisha, majenzi yatakuwa ya nani?
= Suala la mazingira limezingatiwa kwa kiasi gani?
Hii kauli tu imenifanya wala nisijihangaishe kujibu hoja zako.Kukodisha au kuuza ni kitu kilekile;
Mkuu mimi nimesoma kawaida tu.We we waonyesha in msomi wa hali ya juu,unajibu maswali kisomi na kistaarabu.Napenda unavyojibu maswali,ningekuwa na kiwango cha elimu kama yako,ningeringa sana.
Ni kweli mkuu,Nadhani sio uamuzi mbaya kukodisha visiwa. Kwani pesa inayopatikana inakwenda kuendeleza huduma za jamii. Mleta uzi kaja kisiasa zaidi.
Kaandika mada kiuchokozi ili kuigombanisha serikali ya Mwinyi na wote watakaosoma andiko lake.
Mimi nalijua hili suala kwa kiasi mkuu. Hofu yangu tu niliitanguliza mwanzo kabisa kwamba huu uzi usije ukatumika kupotosha jambo jema lililofanywa na serikali ya mainduzi ya Zanzibar.Mkuu, kwa vile wewe unajua hilo suala vizuri sana, ni vyema sasa kumuelimisha huyo ndugu na wengine wengi ambao hili jambo ni mara ya kwanza kulisikia kwa kueleza ukweli wa jambo hilo kama walivyouliza:
1. Ni lini suala hilo lilijadiriwa? Je ni kikao cha Bunge/Baraza la Wawakilishi liliridhia?
2. Je nini matumizi ya pesa za mauzo ya hivyo visiwa
3. Jambo hilo kiujumla linafaida gani hasa kwa nchi?
Mimi nadhani mgao wa pesa hizi ni kwa ajili ya Zanzibar tu. Ila najua kwamba kwa namna mbali mbali hata Tanzania itafaidika na suala hili.Na je mgao wa pesa hizo zinaihusu pia Upande wa Tanganyika? Au pesa kutoka zenji ni inaihusu zenji peke yake?
Hivyo visiwa hiyo Project ni ya huko huko. Hata Huku Tanzania bado tuna nafasi kubwa zaidi ya kuwekeza Kwenye eneo letu la Bahari. Tuna visiwa Vingi Kwenye mwambao wa Bahari ukianzia Tanga Mpaka Mtwara wengi wetu tunavijua Mbudya,Bongoyo,Pole pole kipo Mafia.Mimi nadhani mgao wa pesa hizi ni kwa ajili ya Zanzibar tu. Ila najua kwamba kwa namna mbali mbali hata Tanzania itafaidika na suala hili.
Kwahiyo na Tanganyika wakodishe visiwa vyaoHivyo visiwa hiyo Project ni ya huko huko. Hata Huku Tanzania bado tuna nafasi kubwa zaidi ya kuwekeza Kwenye eneo letu la Bahari. Tuna visiwa Vingi Kwenye mwambao wa Bahari ukianzia Tanga Mpaka Mtwara wengi wetu tunavijua Mbudya,Bongoyo,Pole pole kipo Mafia.
Inawezekana mkuu,nadhani kama kisiwa Cha Pole Pole kule Mafia wale wamekodishiwa wale wazungu ili sio geni.Kwahiyo na Tanganyika wakodishe visiwa vyao