Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Hivi hapa anayetumia kilevi ni nani? Je unaijua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Katiba: 1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

Je linapotajwa neno eneo, je ni pamoja na ardhi?
Katiba: 2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Kweli wewe ndiye mlevi wa kutupwa, je unajua JMT ni mdudu gani?
Mimi nilidhani JMT ni pamoja na Zanzibar yenyewe, sasa Kenya na Kuwait zinaingiaje hapa?
Ok
 
Zanzibar ni sehemu ya JMT, kwa maana ya kuuzwa kwa kipande cha ardhi ndani ya JMT ina maana gani kwa mamlaka ya JMT?
Je watu wanaonunua visiwa hivyo watatawalwa kwa sheria zipi? za JMT, SMZ, au za nchi zao?
ZANZIBAR NI Nchi na inamaanuz yake MCTUZINGUWE Ila hili ni tatizo
 
Habari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha. Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.... Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!

Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha

Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!

Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).

Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?

Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
Kuna tetesi kuwa USA ilijaribu mara kadhaa wakati wa utawala wa Jakaya kupata ridhio la kuweka military base Zanziba ambayo ingekuwa na kazi ya kulinda na kuendesha operations mbalimbali Africa ya mashariki mkawakatalia. Leo hii bilgate a Richmond from USA anauziwa/kukodishiwa zaidi ya hecta 200, mnafikiri military base inahitaji eneo la squremeter ngapi? na askari wangapi?
Basi kamandivyo Mission complete na nyie kalaghabao.
 
Yaani uzi wako upotoshe umma halafu walaumiwe serikali?? Kwani tulipoambiwa tuwe wazalendo maana yake ni nini?? Maana yake ni kuacha kuripoti uongo na ubaya unaohusu nchi zetu na watu wake.

Nchi zisizotutakia mema zinatuchafua, sisi tusiingie katika mtego wa kujichafua wenyewe.

Halafu pili, ni nani aliekwambia raia wa Tanzania hawaruhusiwi kwenda ku-lease hivyo visiwa?? Just for your information, mtu yoyote asie mzanzibar atapewa hivyo visiwa akikidhi vigezo kwa kukodishwa. Mnyamwezi atakodi, msukuma atakodi pia sasa wewe ni nani aliekwambia hao raia wa Tanzania hawajapewa kipaumbele?? Na ni nani pia kakwambia tahadhari kubwa haichukuliwi???

Mkuu, una elimu yoyoyte ya mambo ya mikataba?? Law of contract?? Huu ni mkataba na una masharti yake, ukikiuka kuna vipengele vinavyozungumzia hilo. Wasiwasi uko wapi?? Hilo la vipengele vya siri sasa ulizungumzie wewe ulielileta.

Msimamo wako baki nao, serikali ni uwakilishi wa watu. Serikali ya Zanzibar ni uwakilishi wa Wazanzibari na wao wanafanya kwa maslahi ya Wazanzibari.
Iyo mikataba imepitishwa wapi Kwa k we li Wazanzibar tunapelekwa siko
 
Yaani uzi wako upotoshe umma halafu walaumiwe serikali?? Kwani tulipoambiwa tuwe wazalendo maana yake ni nini?? Maana yake ni kuacha kuripoti uongo na ubaya unaohusu nchi zetu na watu wake.

Nchi zisizotutakia mema zinatuchafua, sisi tusiingie katika mtego wa kujichafua wenyewe.

Halafu pili, ni nani aliekwambia raia wa Tanzania hawaruhusiwi kwenda ku-lease hivyo visiwa?? Just for your information, mtu yoyote asie mzanzibar atapewa hivyo visiwa akikidhi vigezo kwa kukodishwa. Mnyamwezi atakodi, msukuma atakodi pia sasa wewe ni nani aliekwambia hao raia wa Tanzania hawajapewa kipaumbele?? Na ni nani pia kakwambia tahadhari kubwa haichukuliwi???

Mkuu, una elimu yoyoyte ya mambo ya mikataba?? Law of contract?? Huu ni mkataba na una masharti yake, ukikiuka kuna vipengele vinavyozungumzia hilo. Wasiwasi uko wapi?? Hilo la vipengele vya siri sasa ulizungumzie wewe ulielileta.

Msimamo wako baki nao, serikali ni uwakilishi wa watu. Serikali ya Zanzibar ni uwakilishi wa Wazanzibari na wao wanafanya kwa maslahi ya
Sheikhnaa, usi assume sina elimu ya mikataba na zaidi. Pengine wanizidi, ila siko mbali sana. Mkataba ni mzuri 'as long as both sides act in good faith and hold identical interpretations thereof'!
Kitendo cha serikali kutoliweka jambo hili wazi kwa wananchi wengi ( usiniambie kuna mtandao. 70% ya Watanzania hawajui mtandao ni nini, tena wa Kiingereza!)...ni wazi pamekusudiwa kufichaficha. Wewe unayeamini sanaa serikali, good for you. I wish I were a fool!
Wananchi pekee ndiyo wangekuwa dhamana kubwa kwa wawekezaji kutekeleza masharti ya mkataba. Unapowaacha wananchi kwenye giza, unajenga mazingira ya mwekezaji kukiuka masharti ya mkataba na pengine kutoheshimu muda pindi mkataba huo unapoisha. Haya mambo yangewekwa dhahiri shahiri kwa kila raia. Haraka za nini?
Tajriba za nchi nyingine zilizofanikiwa usizilete uka cut and paste Tanzania. China imefanikiwa kwa Ujamaa, jee sisi tumefanikiwa? Indonesia imefanikiwa kwa kilimo cha michikichi, sisi tumefanikiwa? Halkadhalika, the Maldives wamefanikiwa kukodisha... Na usifananishe Maldives na Zanzibar. Waache wao wafanye haraka maana pengine visiwa vyao havitakuwepo miaka 50 ijayo!
Kuna umuhimu wa sisi kuuliza maswali maana tunazungumzia mustakbali wa vizazi vyetu. Hizi serikali zisizo na uwazi, zisizo na bunge huru linaloweza kupinga.... zisizowapa itibari rai wake........si za kuamini mnooooo!
Ehe, baada ya miaka 99 kutatokea nini? Maana hata waliotia saini hawatakuwepo na serikali zetu zimeshindwa hata kuchunga records. Nadhani unakumbuka marehemu Magufuli aliposema mwekezaji wa almasi kule shinyanga ilikuwa agawane na serikali 50% kwa mujibu wa mkataba, ikaendelea hadi akawa hatoi hata 1% kwa vile mkataba ulisahauliwa na waliokuja baadaye.
Please don't be naive if you really care for your posterity!
 
Ama ndiyo yale yalee...Katiba ni kipande tu cha karatasi. Au ni shati? Unavaa leo na kuivua ukipenda. Kwa yanayoendelea Tanzania hivi sasa hata sishangai.

Relief Mirzska, kweli umeivalia njuga hii habari...leo kula na kulala hapa hapa, hutoki! Kutetea uvunjwaji wa Katiba kunataka moyo. Nakutakia kila la kheri!
 
Iyo mikataba imepitishwa wapi Kwa k we li Wazanzibar tunapelekwa siko
Mkuu dega,

Mbona mikataba ya kui-lease ardhi inayotumiwa na Neptune hotel pale Pwani Mchangani haiuliziwi hivi?? Kwani mkataba wa Neptune hotel umepitishwa wapi??
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kuna tetesi kuwa USA ilijaribu mara kadhaa wakati wa utawala wa Jakaya kupata ridhio la kuweka military base Zanziba ambayo ingekuwa na kazi ya kulinda na kuendesha operations mbalimbali Africa ya mashariki mkawakatalia. Leo hii bilgate a Richmond from USA anauziwa/kukodishiwa zaidi ya hecta 200, mnafikiri military base inahitaji eneo la squremeter ngapi? na askari wangapi?
Basi kamandivyo Mission complete na nyie kalaghabao.
Serikali haifanyii kazi tetesi wala umbea umbea.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kuna tetesi kuwa USA ilijaribu mara kadhaa wakati wa utawala wa Jakaya kupata ridhio la kuweka military base Zanziba ambayo ingekuwa na kazi ya kulinda na kuendesha operations mbalimbali Africa ya mashariki mkawakatalia. Leo hii bilgate a Richmond from USA anauziwa/kukodishiwa zaidi ya hecta 200, mnafikiri military base inahitaji eneo la squremeter ngapi? na askari wangapi?
Basi kamandivyo Mission complete na nyie kalaghabao.
Mwelezee huyu Relief....kila kitu ni tetesi! Serikali zetu hazituamini kabisaaa. Wanaamua watu wachache tu mustakbali wa mamilioni yajayo!
 
Sana mkuu. Tena sana!

Mimi ni mfaidika pia kutokana na mradi wa mnemba island.

Jamaa yangu mmoja anashika managerial position pale mnemba.
Ndio maana unapayuka kumbe NI miongoni WA wadaidika WA keki ya Taifa tuambie Wazanzibar WA Matemwe,Tumbatu charawe Kisiwapanza Kengeja wamefaifdikaje usitwambie ulivyofaidika ww na jamaa yako tu
 
Ama ndiyo yale yalee...Katiba ni kipande tu cha karatasi. Au ni shati? Unavaa leo na kuivua ukipenda. Kwa yanayoendelea Tanzania hivi sasa hata sishangai.

Relief Mirzska, kweli umeivalia njuga hii habari...leo kula na kulala hapa hapa, hutoki! Kutetea uvunjwaji wa Katiba kunataka moyo. Nakutakia kila la kheri!
Hapana mkuu,

Kwenye maisha kuna fantasy na reality. Yaliyoandikwa kwenye katiba ya JMT kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na reality ilivyo ni tofauti kabisa.

In reality Zanzibar ni nchi kamili, hayo mengine tunawaachia nyinyi na nadharia zenu. Ndio maana kwenye moja ya post zangu huko juu nikasema "ACTIONS SPEAK LOUDER THAN WORDS"
 
Hapo hapo tukumbuke kwamba Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania. Mipaka ya Jamhuri imeainishwa kwa kujumlisha ardhi yote ya Zanzibar na ya Tanganyika. Serikali ya Jamhuri ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutamka kuhusu sehemu yo yote ya ardhi ya Jamhuri. Mahusiano na nchi za nje ni suala la Muungano. Zanzibar hairuhusiwi kuingia mkataba kuhusiana na ardhi yake bila kuihusisha Jamhuri. Kwa mfano haiwezi kuanzisha ubalozi na nchi ambayo haina mahusiano na Jamhuri. Hilo ndilo tatizo lililojitokeza wakati Zanzibar ilipotaka kujiunga na umoja wa nchi za Kiislamu.
Na nyinyi Watanganyika msituzinguwe Zanzibar ni yetu Sisi mipaka ya Tanganyika ndio yenu
 
Kukodisha au kuuza ni kitu kilekile; mtu anakodi kwa miaka 100 ni vizazi vingapi hivyo vitapita bila kuwa na haki ya kupatumia mahali hapo? Neno kukodisha huwa ni neno laini linalotumiwa kuwapooza wale wanaohoji lakini madhara ya kukodidha kwa wa a chi ni yaleyale sawa na kuuza.
Hivi serikali ikitaka kutumua visiwa hivyo kwa mambo ya kijeshi labda miaka kumi ijayo jiulize itakuwaje ? Itabidi wavilipie kwa waliyemkodisha?
Huo ni mwanzo tu baadae wataingilia hata maeneo wanayoishi watu wa tabaka la chini kwa gia ya miji ya kisasa au kuboresha. Nakwambia hata national parks na game reserve zitamegwa na kuuzwa/ kukodishwa.

Hata haya madeni tunayofakamia huenda wadai wetu wakalazimisha wamegewe ardhi pale itakapodhihiri tumeshindwa kulipa.

Ukizingatia idadi ya watu inaongezeka kwa kasi maana yake wananchi watahitaji ardhi zaidi kwa kujenga, mashamba na makaburi lakini viongozi wamekazana kuwapa ardhi wageni!

Maisha ya watoto wetu na wajukuu yatakuwa magumu sana kutokana na maamuzi ya hovyo yanayofanywa sasa.
Sisi Mwenyezi Mungu aliotujaalia kuwa na ardhi, hatuelewi maana ya kukosa ardhi. Tena tunaona ardhi ni cheap. Kuna nchi kadhaa duniani zinatafuta ardhi kwaudi na uvumba!
 
Wewe unaejua sana tuambie hizo hela zilizopatikana zimefanyia nini?

Sijui elimu yako lakini nina uhakika uelewa wako ni mdogo sana juu ya masuala ya sovereignity,eg.umeshindwa kabisa kujua kuwa kuuza ardhi ni sawa na kuuza nchi,uhuru au sawa na kuuza nyumba...na hakuna kurudishiwa ni forever.

Kwa maana nyingine Zanzibar imeuza uhuru wake kwa wageni,unaunga mkono upumbavu huu!?
Mm siungi mkono na kwakweli sijui wapi tunaoelekwa
 
Mwelezee huyu Relief....kila kitu ni tetesi! Serikali zetu hazituamini kabisaaa. Wanaamua watu wachache tu mustakbali wa mamilioni yajayo!
Mkuu, ipo post yako moja nimeiruka nitaijibu wala usijali.

Unanishangaza unapolalamika mambo kuamuliwa na watu wachache. Hahahahahhaha utanifanya niulize umri wako mkuu. Huo ndio mfumo dunia nzima enzi na enzi.

Nenda China ukaone maamuzi yanafanywa na watu wangapi, USA, UK na hata Tanganyika maamuzi hufanywa na wachache tu mkuu.

Unajua hao wachache wanaofanya maamuzi wanapatikanaje?? Most of the time ni through box la kura. Hapa Tanzania mara ya mwisho walichaguliwa Oktoba 2020.

Ielewe mitaa mkuu
 
Pia hili nimekujibu mkuu Relief. Hata huko kwenye 'kura' za kweli, siyo zetu za magumashi, maamuzi makuu yanayoihusu nchi wananchi bado wanashirikishwa, ingawaje kuna Bunge hai!
 
Mkuu,

Hatuongelei kuuza, tunaongelea kukodisha visiwa ambavyo hatuvitumii. Kwani mkuu inakuuma Zanzibar kukodisha visiwa vyake?
Kuna vitu ni Union Matter (vinavyohusu muungano) na Non Union Matter (visivyohusu muungano) watu wanasahau kufatilia.

Suala la Bahari na Bandari sio la Muungano ndio maana Zanzibar wana Mamlaka Yao(ZPA) na Mamlaka inayosimamia usafishaji wa majini (ZMA) huku Bara tuna Mamlaka ya Bandari (TPA) na hutokuta wakisimamia huko na tuna Mamlaka ya udhibiti ambayo ni (TASAC) ambayo inatumia Merchant Shipping Act(MSA,2003) Kule Zanzibar wana Marine Transport Act (MTA, 2005) hapa Tanzania bara Kwa kutumia MSA Huwa Kuna vipengele kama Jamhuri ya Muungano huwa anaweza kuzuia au kusimamia baadhi ya Sheria Kwa upande wa Zanzibar kwenye Usajili wa Meli ikiwa na kufuta huo Usajili.

Kwenye bahari Kuna Inland water, Territory water na Economic Exclusive Zone (EEZ), International water na Continental Shelf. Sheria ya uvuvi Bara Ipo nyingine na Zanzibar nyingine kasoro DeepSea Fishing Act iliundwa karibuni ndio inashea kote. Kwenye mipaka ya Bahari Tanzania Bara kipande ambacho Ipo Zanzibar hatuna EEZ, sababu tukihesabu 12nm za Territory Water, baada ya kuanza kuhesabu EEZ tukilenga eneo la Unguja na Pemba inabidi tuvuke 200maili ndio maana hapo hatuna EEZ. Zanzibar wana eneo lao la EEZ na Bara tuna EEZ yetu. Mwisho kwenye Territory Water wao Zanzibar kwenye 12 nautical miles ambazo wana uwezo wakuzi control (Jurisdiction as a sovereign state) na ndipo hivyo visiwa vinapatikana ndani ya hizo maili pia ndani na hata meli au Ndege inayopita bila kibali Juu ya hizo itaadhibiwa na wao.
 
nimeupenda huu Muungano Uko vizuri sana yaani ni sawa na kujiita soda wakati unaweza kunywa sukari na ukaacha maji yake ..

[emoji847] daah elimu yangu ndogo haina msaada kabisa kwa nchi hii niidhibiwe kwa kweli
 
Mkuu, ipo post yako moja nimeiruka nitaijibu wala usijali.

Unanishangaza unapolalamika mambo kuamuliwa na watu wachache. Hahahahahhaha utanifanya niulize umri wako mkuu. Huo ndio mfumo dunia nzima enzi na enzi.

Nenda China ukaone maamuzi yanafanywa na watu wangapi, USA, UK na hata Tanganyika maamuzi hufanywa na wachache tu mkuu.

Unajua hao wachache wanaofanya maamuzi wanapatikanaje?? Most of the time ni through box la kura. Hapa Tanzania mara ya mwisho walichaguliwa Oktoba 2020.

Ielewe mitaa mkuu
Natamani kama ungekua NI uvhaguzi
 
Back
Top Bottom