Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Mkuu,

Inategemea bid na bid. Inategemea na negotiations pia ila kuanzia ni miaka 33 na haitozidi miaka 99.

Majenzi yatakayokuweko huko yatakuwa ni hotel na zenye ubora. Kila kampuni itakuwa inapeleka proposal yake na serikali kupitia mamlaka zake itaamua kwa kutumia vigezo mbali mbali.

Baada ya muda kuisha wewe unaondoka na unaacha kila kitu. Ni kama vile mnavyoingia ubia hapo kariakoo mkuu.

Moja ya eneo ambalo serikali imekuwa serious sana kuhusiana na miradi hii ni kwenye mazingira.

Tutumieni muda wetu kuishauri serikali yetu.

Taasisi ipi ndiyo inayoratibu haya. Maana ninataka kuwapa ushauri wa kitaalam bure kwa nchi yangu.
 
Ndio maana unapayuka kumbe NI miongoni WA wadaidika WA keki ya Taifa tuambie Wazanzibar WA Matemwe,Tumbatu charawe Kisiwapanza Kengeja wamefaifdikaje usitwambie ulivyofaidika ww na jamaa yako tu
Sheikh usitake kuniletea ubishi wako na hoja zako za ki CUF CUF hapa.

Huyo ninaekwambia anashika managerial position mnemba ni Mmatemwe, nenda Matemwe kigomani kule ukaone kituo cha afya kilichojengwa na &beyond, na wazanzibari wanafaidika. Nenda Matemwe ukaone miradi wa skuli ya kisasa kabisa unavyowanufaisha watoto wa ki Matemwe, unadhani ule sio kwa sababu ya sera bora za SMZ?? Jielewe hebu sio kila kitu kupinga pinga tu ebo!
 
Sisi Mwenyezi Mungu aliotujaalia kuwa na ardhi, hatuelewi maana ya kukosa ardhi. Tena tunaona ardhi ni cheap. Kuna nchi kadhaa duniani zinatafuta ardhi kwaudi na uvumba!
Kwani nani kakwambia Ardhi hii haitakuwa yetu?? Mkuu kwenye decision making tunatumia taarifa mbali mbali kufanya maamuzi flani.

Vizazi vyetu haviwezi kukosa ardhi ya kilimo wala ya makaazi. Nenda Cheju huko ukajionee, nenda kandwi huko ukajionee, nenda kiwengwa huko ukajionee. Serikali haiangalii leo tu kufanya maamuzi, inaangalia miaka 20 ijayo. Hivo visiwa vipo tangu karne na karne, tumefaidika navyo vipi sisi ????

Vitakuwepo for another 3000 years, tutafaidika navyo vipi?? Why not benefiting from today??
 
Ni kweli mkuu,

Kamwe si uamuzi mbaya. Hebu fikiria, uwepo wa visiwa hivi tangu mwaka 1964 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mpaka Leo ni kwa namna na ukubwa gani umevifaidisha/umeifaidisha jamii ya Wazanzibari??

Leo kwa maamuzi haya Bora kabisa kutoka kwa serikali watu wanaenda kufaidika kwa asilimia kubwa kabisa. Watu watapata ajira na serikali itapata fedha za kufanyia miradi mengine ya maendeleo.

Nauunga mkono uamuzi wa serikali kwa asilimia 100.
Mawazo ya kitumwa visiwa vikae tu visiingize pesa wakati vinaweza kukodishwa na maisha ya wazenji yakaboreshwa.
 
Kuna vitu ni Union Matter (vinavyohusu muungano) na Non Union Matter (visivyohusu muungano) watu wanasahau kufatilia.

Suala la Bahari na Bandari sio la Muungano ndio maana Zanzibar wana Mamlaka Yao(ZPA) na Mamlaka inayosimamia usafishaji wa majini (ZMA) huku Bara tuna Mamlaka ya Bandari (TPA) na hutokuta wakisimamia huko na tuna Mamlaka ya udhibiti ambayo ni (TASAC) ambayo inatumia Merchant Shipping Act(MSA,2003) Kule Zanzibar wana Marine Transport Act (MTA, 2005) hapa Tanzania bara Kwa kutumia MSA Huwa Kuna vipengele kama Jamhuri ya Muungano huwa anaweza kuzuia au kusimamia baadhi ya Sheria Kwa upande wa Zanzibar kwenye Usajili wa Meli ikiwa na kufuta huo Usajili.

Kwenye bahari Kuna Inland water, Territory water na Economic Exclusive Zone (EEZ), International water na Continental Shelf. Sheria ya uvuvi Bara Ipo nyingine na Zanzibar nyingine kasoro DeepSea Fishing Act iliundwa karibuni ndio inashea kote. Kwenye mipaka ya Bahari Tanzania Bara kipande ambacho Ipo Zanzibar hatuna EEZ, sababu tukihesabu 12nm za Territory Water, baada ya kuanza kuhesabu EEZ tukilenga eneo la Unguja na Pemba inabidi tuvuke 200maili ndio maana hapo hatuna EEZ. Zanzibar wana eneo lao la EEZ na Bara tuna EEZ yetu. Mwisho kwenye Territory Water wao Zanzibar kwenye 12 nautical miles ambazo wana uwezo wakuzi control (Jurisdiction as a sovereign state) na ndipo hivyo visiwa vinapatikana ndani ya hizo maili pia ndani na hata meli au Ndege inayopita bila kibali Juu ya hizo itaadhibiwa na wao.
Mkuu Sijali hebu jaribu kupitia haya madini pengine utaelewa kidogo.

Watu wengi humu wanaendeshwa na mihemko, au wanaongea vitu kwa sababu hawana taarifa kamili juu ya mambo mbali mbali
 
Kuna vitu ni Union Matter (vinavyohusu muungano) na Non Union Matter (visivyohusu muungano) watu wanasahau kufatilia.

Suala la Bahari na Bandari sio la Muungano ndio maana Zanzibar wana Mamlaka Yao(ZPA) na Mamlaka inayosimamia usafishaji wa majini (ZMA) huku Bara tuna Mamlaka ya Bandari (TPA) na hutokuta wakisimamia huko na tuna Mamlaka ya udhibiti ambayo ni (TASAC) ambayo inatumia Merchant Shipping Act(MSA,2003) Kule Zanzibar wana Marine Transport Act (MTA, 2005) hapa Tanzania bara Kwa kutumia MSA Huwa Kuna vipengele kama Jamhuri ya Muungano huwa anaweza kuzuia au kusimamia baadhi ya Sheria Kwa upande wa Zanzibar kwenye Usajili wa Meli ikiwa na kufuta huo Usajili.

Kwenye bahari Kuna Inland water, Territory water na Economic Exclusive Zone (EEZ), International water na Continental Shelf. Sheria ya uvuvi Bara Ipo nyingine na Zanzibar nyingine kasoro DeepSea Fishing Act iliundwa karibuni ndio inashea kote. Kwenye mipaka ya Bahari Tanzania Bara kipande ambacho Ipo Zanzibar hatuna EEZ, sababu tukihesabu 12nm za Territory Water, baada ya kuanza kuhesabu EEZ tukilenga eneo la Unguja na Pemba inabidi tuvuke 200maili ndio maana hapo hatuna EEZ. Zanzibar wana eneo lao la EEZ na Bara tuna EEZ yetu. Mwisho kwenye Territory Water wao Zanzibar kwenye 12 nautical miles ambazo wana uwezo wakuzi control (Jurisdiction as a sovereign state) na ndipo hivyo visiwa vinapatikana ndani ya hizo maili pia ndani na hata meli au Ndege inayopita bila kibali Juu ya hizo itaadhibiwa na wao.
Mkuu Offshore Seamen umemaliza vizuri, asiyeelewa hapa atakuwa mlemavu
 
Habari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha. Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.... Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!

Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha

Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!

Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).

Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?

Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
Waachieni Wazanzibari wafanye maendeleo yao. Kwa miaka zaidi ya 56 tumewang'ania utadhani ni mkoa wa Morogoro. Hawapati mgao nzuri wa misaada toka nje kupitia Muungano, hawapati mikopo toka nchi za Kiislamu kama OIC.

Huu ndiyo muda mwafaka wakati Rais wa Muungano ni Mzenj na wa Zenj naye Mzenj. Wakikosa sasa kujipanga wamekwisha
 
Yaani uzi wako upotoshe umma halafu walaumiwe serikali?? Kwani tulipoambiwa tuwe wazalendo maana yake ni nini?? Maana yake ni kuacha kuripoti uongo na ubaya unaohusu nchi zetu na watu wake.

Nchi zisizotutakia mema zinatuchafua, sisi tusiingie katika mtego wa kujichafua wenyewe.

Halafu pili, ni nani aliekwambia raia wa Tanzania hawaruhusiwi kwenda ku-lease hivyo visiwa?? Just for your information, mtu yoyote asie mzanzibar atapewa hivyo visiwa akikidhi vigezo kwa kukodishwa. Mnyamwezi atakodi, msukuma atakodi pia sasa wewe ni nani aliekwambia hao raia wa Tanzania hawajapewa kipaumbele?? Na ni nani pia kakwambia tahadhari kubwa haichukuliwi???

Mkuu, una elimu yoyoyte ya mambo ya mikataba?? Law of contract?? Huu ni mkataba na una masharti yake, ukikiuka kuna vipengele vinavyozungumzia hilo. Wasiwasi uko wapi?? Hilo la vipengele vya siri sasa ulizungumzie wewe ulielileta.

Msimamo wako baki nao, serikali ni uwakilishi wa watu. Serikali ya Zanzibar ni uwakilishi wa Wazanzibari na wao wanafanya kwa maslahi ya Wazanzibari.
Sawasawa..
 
Mkuu,

Hatuongelei kuuza, tunaongelea kukodisha visiwa ambavyo hatuvitumii. Kwani mkuu inakuuma Zanzibar kukodisha visiwa vyake?
Inauma kwa sababu mainland wamewekewa kauzibe hauwezi hata uziwa eneo la choo , mzanzibar anamiliki maeneo kama yote mainland huku Yuko busy kuuzia beberu visiwa ambavyo kama si Zanzibar kuikalia bara kimabavu vinatakiwa viwe vyetu sote. Huo si uroho wa kombamwiko baba ?
 
Kuna tetesi kuwa USA ilijaribu mara kadhaa wakati wa utawala wa Jakaya kupata ridhio la kuweka military base Zanziba ambayo ingekuwa na kazi ya kulinda na kuendesha operations mbalimbali Africa ya mashariki mkawakatalia. Leo hii bilgate a Richmond from USA anauziwa/kukodishiwa zaidi ya hecta 200, mnafikiri military base inahitaji eneo la squremeter ngapi? na askari wangapi?
Basi kamandivyo Mission complete na nyie kalaghabao.
Wewe umechanganyikiwa. Kinachofanyika visiwa vinavyokodishwa kwanza havifiki ukubwa huo. Utaratibu wa kukodisha ni kuwa unasema unataka kutekeleza mradi gani. Masharti pia kufanyike SIA (Strategic impact assessment) ya eneo kulingana na Mradi na Mamalaka ya mazingira itoe vibali. Pia kuna timu ya wataalamu kutoka Sekta mbalimbali ambao wanachambua maombi hayo. Moja ya masharti ni kuwa wananchi waendelee kuvitumia visiwa hivyo kwa shughuli zao za kijamii na kiuchumi
 
Inauma kwa sababu mainland wamewekewa kauzibe hauwezi hata uziwa eneo la choo , mzanzibar anamiliki maeneo kama yote mainland huku Yuko busy kuuzia beberu visiwa ambavyo kama si Zanzibar kuikalia bara kimabavu vinatakiwa viwe vyetu sote. Huo si uroho wa kombamwiko baba ?
Pole mkuu wangu.
 
Back
Top Bottom