Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Kuanzia miaka hiyo mpk leo na hatujui mkataba ule upoje,wanyama wanapakiwa kwenye ndege huko huko kimya kimya,watanzania tunaendaga kufanya vibarua vya ujenzi mkuu,Pori la Loliondo ni nchi ya muarabu
Viongoz washauza kila kitu Kwa sasa wameelekeza akili zao kuuza viwanjwa vya polisi na wakivimaliza vya polisi wata amia maeneo ya Jwtz na magereza
 
Fuatilia vizuri juu ya hili mkuu.

Tunasema hivi, Zanzibar ni nchi kamili na ina mamlak na ardhi yake. Tunasema hivyo kwa vitendo na hatusemi kwa maneno maneno tu.

Halafu nikuweke tu sawa, hakuna kipande cha ardhi kinachouzwa. JMT kuna mambo itaiachia Zanzibar ili ifanye inavyoona inafaa kwa Wazanzibari.
Mbona kwenye swala la kukopa hwakopi kama nchi Wana tegemea Samia akawakopee aje awagaiye?
 
Kama itapotosha, lawama moja kwa moja yaenda kwa serikali kwa kulifanya hili siri kwa Watanzania. Ningetegemea kwanza wangetangaza kwa raia na kutoa ufafanuzi. Pia wangewapa raia wa Tanzania kipa umbele. Sipingi kwa ujumla jambo hili, ingawaje tajriba inaonesha katika ku deal na wenye pesa na nguvu, tahadhari kubwa lazima ichukuliwe (Nyerere hakukosea).
Wangefanya siri, usingejua!! Ungeshtukia tu Kisiwa X kinamilikiwa na Elon Musk!!

Na kwa sie tuliopita pita sana kwenye hivi visiwa, tunaona sawa tu kwa sababu hapa ifahamike kwamba, mtu anaposikia mathalani, Kisiwa cha Zanzibar, basi kisiwa hiki kikuu kinakuwa kimezungukwa na makumi ya visiwa vingine vidogo vidogo!!

Na kwa watu wenye uzoefu na maisha ya visiwani, wanafahamu baadhi ya hivi visiwa huwa HAVITUMIKI KABISA, na usishangae ukisikia vingine havijawahi hata kugusa mguu wa mwanadamu!

Ingawaje vipo vichache ambavyo vina makazi, lakini vinatumika zaidi kama dago tu kuliko kama makazi!!

All in all, Wazenji wenyewe wanaonekana hawana tatizo...

​
 
Kuanzia miaka hiyo mpk leo na hatujui mkataba ule upoje,wanyama wanapakiwa kwenye ndege huko huko kimya kimya,watanzania tunaendaga kufanya vibarua vya ujenzi mkuu,Pori la Loliondo ni nchi ya muarabu
Katiba yetu mbaya sana. Inampa mtu anaeitwa Rais mamlaka za kimungumutu.

Mbaya zaidi hahojiwi popote awe madarakani au akiwa nje ya madaraka.

KATIBA MBOVU SANA HII
 
Juu ya hayo yote, hizo Fedha walizovuna kwenye biashara hiyo ya visiwa wamezitumia vipi?
Wewe unajua Zanzibar hakuna vyanzo vingine vya mapato? Je unajua hayo mapato mengine yametumikaje Hadi uhoji haya ya kukodisha visiwa tuu? Ebu tueleze mapato mengine yametumikaje Hadi huoni hayo ya kukodisha visiwa yalivyotumika.
 
Kwa muda gani kiongozi? isijekuwa miaka 99, maana hata kiwanja unachokimiliki umekodishwa na serikali lakini tukijenga tunasema nyumba ni zetu.
Na ndiyo jiwe akazivunja nyumba Za watu bila wasiwasi
 
Viongoz washauza kila kitu Kwa sasa wameelekeza akili zao kuuza viwanjwa vya polisi na wakivimaliza vya polisi wata amia maeneo ya Jwtz na magereza

Watauza mpaka makalio yao 😛😛😝😝
 
Kuna siku nilichangaia mada fulani kwamba, ikiwa nchi ina viongozi waaminifu na waadilifu, siyo vibaya kuuza eneo la nchi na kupata pesa nyingi za kuendeleza maeneo mengine, kwa sababu hakuna sababu ya kuishi maisha magumu utafikiri tumehamia hapa Duniani.

Kwa mfano, kuna ubaya gani mwekezaji anataka kuinunua mbuga ya Serengeti kwa trilion 500? Hiyo hela itajenga SGR, bandari, mashule, hospital nk. Mbuga za Wanyama zipo nyingi tu. Au Geita ya dhahabu ikiuzwa kwa trilion 400-500 kuna ubaya gani wakati madini yapo kila kona ya nchi?



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna siku nilichangaia mada fulani kwamba, ikiwa nchi ina viongozi waaminifu na waadilifu, siyo vibaya kuuza eneo la nchi na kupata pesa nyingi za kuendeleza maeneo mengine, kwa sababu hakuna sababu ya kuishi maisha magumu utafikiri tumehamia hapa Duniani.

Kwa mfano, kuna ubaya gani mwekezaji anataka kuinunua mbuga ya Serengeti kwa trilion 500? Hiyo hela itajenga SGR, bandari, mashule, hospital nk. Mbuga za Wanyama zipo nyingi tu. Au Geita ya dhahabu ikiuzwa kwa trilion 400-500 kuna ubaya gani wakati madini yapo kila kona ya nchi?



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

Kwa hali hiyo Mali zikiisha utauza kitu gani Na wewe Una shida?
 
Hapana mkuu,

Kwenye maisha kuna fantasy na reality. Yaliyoandikwa kwenye katiba ya JMT kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na reality ilivyo ni tofauti kabisa.

In reality Zanzibar ni nchi kamili, hayo mengine tunawaachia nyinyi na nadharia zenu. Ndio maana kwenye moja ya post zangu huko juu nikasema "ACTIONS SPEAK LOUDER THAN WORDS"
Katiba mpya inahitajika ama marekebisho ya katiba kwenye kipengele kinachohusu ardhi na mipaka ya Zanzibar kuondoa hii sintofahamu.
 
Serekali ya Zanzibar si uwakilishi wa wazanzibari, Kura za wananchi hazikuheshimiwa waliongia madarakani waliingia kwa mtutu wa bunduki.
Sawa mkuu ila hii itakuwa ni mada nyengine.

Tunaweza tukaifungulia uzi na kuijadili na nitatoa mawazo yangu juu ya hilo
 
Ucwe na jazba mm c Cuf c CCM Wazanzibar tumecheleweshwa xana Kwa dizain izo hapo weka Uzanzibar wako mbele wacha kuhemkwa hizi NI rasilimali zetu sote regardless chama chak au itikadi yako
Na ndio maana katika hili sikuweka uchama mbele.

Nafahamu sana kwamba tofauti zetu za kisisasa ndio ilikuwa changamoto yetu kuu na hata Mzee wetu al marhuum Maalim Seif Shariff Hamad alilijua hili na ndio akaamua Zanzibar kwanza.

Sasa ukiangalia kwa jicho kuu, kinachofanyika Zanzibar kuhusu ukodishwaji wa hizi ardhi basi ni kwa faida kuu ya Wazanzibari kwa ujumla wao bila kujali itikadi zao za kisiasa.
 
Relief Mirzska ni kada mtiifu wa CCM, musipate tabu nae kabisa.

Nchi inauzwa kiholela yeye kifua mbele yupo anatetea.
Mkuu,

Hata kama nisingekuwa kada wa CCM basi suala hili ningeliunga mkono.

Yapo maswala kadhaa ambayo serikali hii hii ya CCM inayafanya sasa hivi ambayo yanafurahisha Sana haijalishi wewe ni CUF/ ACT au CCM.
 
Samahani hii USD 2,500,000 ni Capital anayotakiwa awenayo investor ama ni lease price?
Mkuu hiyo sio lease price, lease price itatofautina from one area to the other based on different factors.

Hiyo ni minimum capital ambayo investor anatakiwa awe nayo.

NOTE: Investor anaweza akawa na hiyo hela, na bado application yake ikapigwa na chini kutokana na factors nyengine.
 
Hujajibu kitu. Ulichofanya ni kuongeza suspicion kuwa kuna kitu kinafichwa. Hamna haja ya kumbeza mtu aliyekuuliza swali kwa sababu hupendi tu jinsi alivyoliuliza. Kwa majibu hayo aliyeuliza ataenda kuyapeleka kwa hao wananchi ambako hautakuwa na njia ya kumsahihisha. Obfuscation haisaidii.

Kujificha nyuma ya pazia kuwa serikali inafanya yote hayo kwa maslahi ya raia wake hakusaidii maana kuna mifano mingi tu ya wananchi kuumizwa kutokana na mikataba ambayo serikali yao imeingia kwa niaba yao. Mpe heshima yake kwa sababu ni kodi yake na za watu kama yeye ndio kwa kiasi kikubwa inaipa serikali yake uwezo wa kufanya hayo inayofanya. Na ni kodi yake ndio itakayotumika kurekebisha makosa yoyote yanayoweza kutokea hapo baadae.

Wewe kama unaweza kulipia chumba cha dola 2000 usimdharau yule anaedhani kuwa anakatazwa hata kuogelea katika maji yaliyozunguka kisiwa cha Bill Gates. Kama anatuhusiwa, mueleze hivyo kwa lugha ya staha ambayo wewe ungependa aitumie. Muonyeshe kwa mfano.

Amandla...
Ok
 
Back
Top Bottom