Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Hongera sana Zanzibar. Kumbe UNO mmewahi kuwako? Sasa mnafeli wapi na sasa mambo mswanooo? Fosini tu na hili liwezekane. Kwa population yenu ilivyo mtaenjoy sana. Fedha za kukodisha visiwa + watumishi wa ubalozi huko duniani na mashirikani na wafanyabiashara Tanganyika na ajira za ndani za seriklia ya zanzibar na muungano, loh, mtajikuta pato la Taifa lenu lipo juuu sana na mtaenjoy saana.
Nakubaliana na hoja hii pia
 
Habari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha. Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.... Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!

Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha

Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!

Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).

Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?

Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
Visiwa wanauza na bado pesa za mikopo wanapata
 
Wangefanya siri, usingejua!! Ungeshtukia tu Kisiwa X kinamilikiwa na Elon Musk!!

Na kwa sie tuliopita pita sana kwenye hivi visiwa, tunaona sawa tu kwa sababu hapa ifahamike kwamba, mtu anaposikia mathalani, Kisiwa cha Zanzibar, basi kisiwa hiki kikuu kinakuwa kimezungukwa na makumi ya visiwa vingine vidogo vidogo!!

Na kwa watu wenye uzoefu na maisha ya visiwani, wanafahamu baadhi ya hivi visiwa huwa HAVITUMIKI KABISA, na usishangae ukisikia vingine havijawahi hata kugusa mguu wa mwanadamu!

Ingawaje vipo vichache ambavyo vina makazi, lakini vinatumika zaidi kama dago tu kuliko kama makazi!!

All in all, Wazenji wenyewe wanaonekana hawana tatizo...

​

Hakika mkuu.

Akili kubwa tu ndio inaweza ikaelewa na kuchambua mambo haya
 
Katiba mpya inahitajika ama marekebisho ya katiba kwenye kipengele kinachohusu ardhi na mipaka ya Zanzibar kuondoa hii sintofahamu.
Wewe unataka hiyo katiba mpya isemeje kuhusu ardhi na mipaka ya Zanzibar???
 
Habari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha. Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.... Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!

Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha

Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!

Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).

Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?

Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
Kama Dr. Mwinyi hana lengo la kujitajirisha yeye binafsi baada ya madaraka mimi nasema ni jambo jema ikiwa nia yake na atafanikisha kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo kutoka na fedha hizo bila ya kuzikwapua kwapua na kupeleka kule mkuranga
 
Mkuu,

Hata kama nisingekuwa kada wa CCM basi suala hili ningeliunga mkono.

Yapo maswala kadhaa ambayo serikali hii hii ya CCM inayafanya sasa hivi ambayo yanafurahisha Sana haijalishi wewe ni CUF/ ACT au CCM.

Tatizo lako mkuu umeshindwa kuielewa CCM kwa miaka yote ambayo imekuepo. Tatizo la Dr.Mwinyi ni kufanya pupa kwenye hayo masuala, Visiwa ameviuza kwa bei chee kabisa, tungeanza kujiboresha kimiundo mbinu kwanza wawekezaji wangelikuja kupanga foleni kwa mikataba yenye masharti tunayoyataka sisi na si ivo alivyofanya yeye.

CCM siku zote wamkua ni failure na sababu kuu ni udogo wao wa IQ, wao wanawaza mambo matatu tu, Ni Vipi watabaki madaraki, Vipi wataaiba na kujilimbikizia mali za umma, Na vipi watafanya jambo lolote la kimaendeleo ili wajijengee sifa za kijinga. Tatizo kila wanapojaribu kufanya jambo la kimaedeleo wanaishi kuchemka kutokana na tamaa zao wizi pamoja low IQ zao. Eg wametumia zaidi ya Dola 100m kwa kujenga terminal mpya Zanzibar ambayo bado haijakidhi kiwango tunachohitaji kuwa nacho.
 
Uvamizi hauna sheria wala Katiba
Permitted land exploitation, ni organazide
Mimi sina jazba mkuu. Nadhani suala tumelizungumzia vya kutosha kwamba kinachofanyika ni kwa maslahi mapana sana ya Zanzibar na watu wake.
Ni mfumo mzuri wa unyakuzi wa Ardhi hasa unapokuwa katika Hali ya uwekezaji katika tasinia mbili, uwekezaji katika utalii na kilimo. Ubaya huanza pale ubaguzi unapoanzia. Hii mikataba iendane na haki sawa kwa wafanyakazi na wale wanaopaswa kuingia hapo
 
Kama Dr. Mwinyi hana lengo la kujitajirisha yeye binafsi baada ya madaraka mimi nasema ni jambo jema ikiwa nia yake na atafanikisha kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo kutoka na fedha hizo bila ya kuzikwapua kwapua na kupeleka kule mkuranga

Mendeleo hayaji kwa kuuza visiwa ambavyo ni mmoja ya hazina kubwa za nchi.
 
Sio kuuza wamesema ni kukodisha, Mbona huko tanganyika mama anapiga makelele wawekezaje waje watapewa maeneo na kenda mbali zaidi kasema vibali wasicheleweshwe wapewe haraka haraka wale maofisa vibali waondoe urasimu., amefika mpaka jumuiya za kimataifa huko kuwaomba wawekezaji? Ulitaka Zanzibar wakodishe nini? Mavuzzi?

Tanganyika siku zote muna wivu wa Zanzibar kupiga hatua za kimaendeleo ndio mana mnaishikilia kila ikitaka kupiga hatua mnaleta maneno ya jikoni jikoni., piriad.,
 
Hahahahahaahahahah

Just point of correction. dos.2020 ni Mzanzibar safi kabisa na huwa yupo sana pale Mkunazini.

Sijui kama hakai kai pale Jaws corner maana hahahaha
 
Tatizo lako mkuu umeshindwa kuielewa CCM kwa miaka yote ambayo imekuepo. Tatizo la Dr.Mwinyi ni kufanya pupa kwenye hayo masuala, Visiwa ameviuza kwa bei chee kabisa, tungeanza kujiboresha kimiundo mbinu kwanza wawekezaji wangelikuja kupanga foleni kwa mikataba yenye masharti tunayoyataka sisi na si ivo alivyofanya yeye.

CCM siku zote wamkua ni failure na sababu kuu ni udogo wao wa IQ, wao wanawaza mambo matatu tu, Ni Vipi watabaki madaraki, Vipi wataaiba na kujilimbikizia mali za umma, Na vipi watafanya jambo lolote la kimaendeleo ili wajijengee sifa za kijinga. Tatizo kila wanapojaribu kufanya jambo la kimaedeleo wanaishi kuchemka kutokana na tamaa zao wizi pamoja low IQ zao. Eg wametumia zaidi ya Dola 100m kwa kujenga terminal mpya Zanzibar ambayo bado haijakidhi kiwango tunachohitaji kuwa nacho.
Mkuu,

Hatuwezi kuendelea kukalia rasilimali zisifaidishe watu wetu ili kusubiria hali flan itufikie. Hili lililofanyika ndio linaenda kuboresha hiyo miundombinu ili baada ya 33 years from today tuweze kuvikodisha visiwa vyetu kwa masharti Bora zaidi kwetu.

Halafu hebu nitajie watu kumi tu tangu tupate uhuru ambao wamejilimbikizia mimali from Zanzibar
 
Mkuu hiyo sio lease price, lease price itatofautina from one area to the other based on different factors.

Hiyo ni minimum capital ambayo investor anatakiwa awe nayo.

NOTE: Investor anaweza akawa na hiyo hela, na bado application yake ikapigwa na chini kutokana na factors nyengine.
Shukran
 
Sio kuuza wamesema ni kukodisha, Mbona huko tanganyika mama anapiga makelele wawekezaje waje watapewa maeneo na kenda mbali zaidi kasema vibali wasicheleweshwe wapewe haraka haraka wale maofisa vibali waondoe urasimu., amefika mpaka jumuiya za kimataifa huko kuwaomba wawekezaji? Ulitaka Zanzibar wakodishe nini? Mavuzzi?

Tanganyika siku zote muna wivu wa Zanzibar kupiga hatua za kimaendeleo ndio mana mnaishikilia kila ikitaka kupiga hatua mnaleta maneno ya jikoni jikoni., piriad.,

Acha matusi binti, Wanasema ni kukodisha, ushahidi wa kuwa vimekodishwa upo wapi? kwanini mikataba iwe siri? hivi miaka 99 hiyo bado unaita kodi?
 
Mkuu,

Hatuwezi kuendelea kukalia rasilimali zisifaidishe watu wetu ili kusubiria hali flan itufikie. Hili lililofanyika ndio linaenda kuboresha hiyo miundombinu ili baada ya 33 years from today tuweze kuvikodisha visiwa vyetu kwa masharti Bora zaidi kwetu.

Una uhakika kama ni miaka 33 na si 99? hapo ndipo watu wanapoanza kuhoji.
 
Mkuu,

Halafu hebu nitajie watu kumi tu tangu tupate uhuru ambao wamejilimbikizia mimali from Zanzibar

Mzee Karume
Karume Jr
Mansour Himid
Dr Shein na Genge lake, Kuanzia Dr Khalid, Balozi Seif, Mohammed Aboud, Haji Kheri, Omar Yussuf.
Uliwahi kuwasikia akina Omar King? Abiola?
Hivi yule mkurugenzi wa ZSSF bi Sabra alisimamishwa kazi kwa shutuma gani?
Na sasa ni zamu ya Mwinyi Family.

SMZ wamekua wakipiga billions of Money kwa miaka mingi sana.
Mall la Michenzani wamepiga mabilions, Meli ya Mapinduzi wamepiga mabillions, Mnara wa Michenzania wamepiga ma billions, Majumba yake ya Kwahani nio hayo hayo, Uwanja wa ndege ndio hayo hayo.

Kuendelea kuwaamini CCM kwa chochote kile ni Uwendawazimu
 
Back
Top Bottom