Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Hapo hapo tukumbuke kwamba Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania. Mipaka ya Jamhuri imeainishwa kwa kujumlisha ardhi yote ya Zanzibar na ya Tanganyika. Serikali ya Jamhuri ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutamka kuhusu sehemu yo yote ya ardhi ya Jamhuri. Mahusiano na nchi za nje ni suala la Muungano. Zanzibar hairuhusiwi kuingia mkataba kuhusiana na ardhi yake bila kuihusisha Jamhuri. Kwa mfano haiwezi kuanzisha ubalozi na nchi ambayo haina mahusiano na Jamhuri. Hilo ndilo tatizo lililojitokeza wakati Zanzibar ilipotaka kujiunga na umoja wa nchi za Kiislamu.
Hizi ni nadharia tu.

Vitendo vinaendelea Zanzibar huko. Actions speak louder than words.
 
Wewe unaejua sana tuambie hizo hela zilizopatikana zimefanyia nini?

Sijui elimu yako lakini nina uhakika uelewa wako ni mdogo sana juu ya masuala ya sovereignity,eg.umeshindwa kabisa kujua kuwa kuuza ardhi ni sawa na kuuza nchi,uhuru au sawa na kuuza nyumba...na hakuna kurudishiwa ni forever.

Kwa maana nyingine Zanzibar imeuza uhuru wake kwa wageni,unaunga mkono upumbavu huu!?
Paragraph yako ya kwanza nimeshaijibu. Hata nilipokuwa nikipiga lectures kipindi hicho sikuwa na kawaida ya kurudiarudia kwa ambao hawaskilizi vizuri na kuelewa.

Paragraph yako ya pili ni kwamba: ni kweli hujui elimu yangu na ni busara hilo ukaniachia mwenyewe maana hata ukiijua haitokusaidia chochote. Uelewa wangu mdogo juu ya masuala ya Sovereignty?? Sawa if you say so, ila mimi nina wasiwasi wa uwezo wako hata wa kusoma tu na kuelewa leave alone issue kubwa na sensitive kama "Sovereignty " . Ni nani kasema ardhi ya Zanzibar imeuzwa?? Soma uelewe kabla ya ku-comment. Kuna utofauti kati ya kuuza na kukodisha.

Paragraph yako ya tatu ni kwamba: kwa kuwa Zanzibar haijauza ardhi yake basi haijauza uhuru wake.
 
Shukran mkuu, kuhusu maswali yako ni kama ifuatavyo

1) naomba muda ntakujibu kuhusu mpango wa matumizi ya kodi ya iliyopatikana kutoka kwenye visiwa vilivyokodishwa tayar.

2) wananchi wanazo taarifa, mimi ni mwananchi wa kawaida na ninazo taarifa kwamb visiwa vinakodishwa kwa kuanzia miaka 33 mpaka 99 maximum.

3) Mambo haya hayajakuwa siri. Yanatolewa taarifa kila uchao.

View attachment 2091185
Mkuu, epuka hawa watu wanajifanya wajuaji na wapingaji wa kila kitu. Vijana wa ki-leo Sisi tumekuwa wapuuzi sana ndio maana watu kama kina mkuchika itabidi waendelee kuteuliwa tu.
Mkuu mchakato ulikuwa wazi Mimi nafatilia na Niko Huku Bara, tangu muda na Kila siku huwa napitia website ya Zanzibar Investment Promotion Authority (ZIPA) Kila kitu kimeelezewa vizuri na ziara zote kuhusu huu uwekezaji wanaweka mrejesho.

Nina Gazeti la Daily News na The Guardian la Jumanne wiki hii walitoa Tangazo pia la kwenda kuwekeza, Nitapiga picha niiweke pia.

Watu watembelee link hii hapa chini ya ZIPA waone kila kitu kwenye uwekezaji kuanzia Blue Economy na Free Economic Zone.

 
It's the same approach ambayo Maldives waliichukua some years ago. Leo Sisi hapa watu wanalishwa matango pori tu.

Tutafika lakini
Kweli mkuu, huu uwekezaji utakuwa na faida mpaka Huku kwetu bara maana watalii wengi watapita hapa Dar es Salaam Kwa njia ya Boti au Ndege kabla ya kufika Zanzibar. Pia Ukanda wa Pangani na Bagamoyo nao watafaidika na watalii kuongezeka.
 
Nano tena huyo ameanza kuuza nchi! Siyo Ndugai kweli!
 
Hizi ni nadharia tu.

Vitendo vinaendelea Zanzibar huko. Actions speak louder than words.
Kwenye geti kuu la base ya Navy USA wameweka neno la kilatini "Acto non Verbo" ikimaanisha "Kazi kwanza si maneno".

Watanzania wakizubaa tutashangaa wakenya na warwanda wamewekeza Zanzibar Hata Uwekezaji ambao watu wa kawaida wangefanya.

Kuna uwekezaji wa vifaa vya kutengeneza vifaa vya uvuvi, Bioprocessing na utunzaji wa mazao ya uvuvi, Kuna tenda za ujenzi wa barabarani,masoko.
 
Hiyo pesa inafika na huku au wao tu ndio wanataka zetu....
Zanzibar inatabia ya 'last born', kupenda dezo..
 
Kwenye geti kuu la base ya Navy USA wameweka neno la kilatini "Acto non Verbo" ikimaanisha "Kazi kwanza si maneno".

Watanzania wakizubaa tutashangaa wakenya na warwanda wamewekeza Zanzibar Hata Uwekezaji ambao watu wa kawaida wangefanya.

Kuna uwekezaji wa vifaa vya kutengeneza vifaa vya uvuvi, Bioprocessing na utunzaji wa mazao ya uvuvi, Kuna tenda za ujenzi wa barabarani,masoko.
Sisi kazi yetu kupingapinga tu kila kitu
 
Wam
Wamepata ajira wangapi wanalipwa kiasi gani. Maana siyo watu walipwe kama watumwa. Je hao walioajiriwa wakiacha kazi baada ya miaka 2 wanaweza waka survive muda gani kwa saving zao. Jamhuri ni Mali ya umma (Res Publica) kuna haja ya kila maamzi hekima na busara vikatumika maana hawa wazungu walishaonyesha hawana nia na sisi. Miaka ya 1903 Cuba leased Guantanamo bay to the US ,and now marekani haitako kuirudisha. Tuwe tu makini kwa tunavyofanya na kuamua leo, maana tunaweza kufanya makosa akawagharimu watoto wakaja kutulaumu. Uzalendo kwanza
Mkuu mimi nimeuliza swali, badala kunijibu naona umeniandikia insha
 
Mwenye uwezo wa kuwekeza katika visiwa hivyo bado anayo nafasi.

Tarehe ya mwisho ya maombi ya kupata lease ni 16/02/22 saa 6 mchana .

Tuma maombi yako kwa ZIPA. Ofisi zao zipo barabara ya Malawi.
Zanzibar kuna barabara ya kwenda malawi?
 
Huu uzi ni mzuri lakini nina hofu usije ukatumika kupotosha.

Umeuweka kwenye mtindo wa swali. Jibu ni kwamba, visiwa hivyo vinakodishwa na wala haviuzwi.

Sisi tumekwenda Mnemba mara kadhaa na hata wanajamii wenzetu wanakwenda.

Ni maamuzi mazuri yaliyofanya na SMZ na mimi kama Mzanzibar nayaunga mkono.
nashauri Environment impact assement iwe kali TOR ziwe za kimataifa idara ya mazingira wawezeshwe usafir na vifaa vya kuvizungikia mara kwa mara kufanya tathmin
 
Huu uzi ni mzuri lakini nina hofu usije ukatumika kupotosha.

Umeuweka kwenye mtindo wa swali. Jibu ni kwamba, visiwa hivyo vinakodishwa na wala haviuzwi.

Sisi tumekwenda Mnemba mara kadhaa na hata wanajamii wenzetu wanakwenda.

Ni maamuzi mazuri yaliyofanya na SMZ na mimi kama Mzanzibar nayaunga mkono.

Tafadhali naomba kujua yafuatayo.
= Vinakodishwa kwa muda gani?
= Majenzi yatakayowekwa huko yatakuwa ya aina na ubora gani?
=Baada ya muda wa kukodi kuisha, majenzi yatakuwa ya nani?
= Suala la mazingira limezingatiwa kwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom