Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Mkuu suala la dini usiliunderlate ukweli utabaki kuwa wakiristo watazidi kuwaona wazungu kama ndugu zao kwa kuwaletea dini ya kikiristo bila wao leo hii tusingekuwa na akina john na peter hapa kwetu tz

Vilevile waislam watazidi kuwaona waarabu ndugu zao na watu waliowaletea dini ya kiislaam bila wao tusingekuwa na akina Abdallah na Mohammed hapa kwetu tz

Huu ukweli huwezi kuukwepa balance tu minzani usijipe shida
 
Ana miaka 95. Anataka tu kumalizia uhai wake mahali alipozaliwa. Hizi ndiyo 4Rs za Samia
 


Ile ni roho ,itawatafuna wazanzibari na watangayika muda sio mrefu.

Mungu alimtimua shetani kwenye utawala wake na kukiondoa kabisa kiti chake na nafasi yake kule mbinguni .

Roho ya utumwa imerejea rasmi na itapata nguvu kupitia dini.
 
Umemlenga nani kwa ujumbe huo?
 
Mkuu Situ, Stuxnet ,hii ni habari njema sana,na najisikia faraja sana kwa jambo uliloshauri litekelezwe,nilianzia hapa Dear Mama, Can you Offer An Unconditional Amnesty to All Zanzibaris Waliokimbia After Revolution, Incl Sultan, Be Free to Return & Start Afresh? nikaja Voices From Within: Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said atafurahi zaidi kama atarudi Zanzibar. Rais Samia, Rais Mwinyi, sameheni, utabarikiwa sana! halafu likatekelezwa Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni hata kama utekelezaji huo hauhusiani na ushauri wako,lakini ulishauri Sultani ajengewe mazingira ya kurejea Zanzibar, sasa anarejea Zanzibar, mtu unafarijika。

Kuhusu kurejea Sultani Zanzibar, Ushauri wangu ni huu。
  1. Serikali ya Zanzibar igharimie kila kitu kwenye ziara hiyo, apokelewe na kutembezwa na ving'ora as a healing process ya machungu aliyopitia。
  2. Aandaliwe an ad hoc protocal ya Sultan mpinduliwa,kwa jinsi ile ile katiba ya JMT,haitambui katiba ya Zanzibar lakini protocal inawatambua na wana ving'ora。
  3. Akabidhiwe part ya lile kasri lake la Beit Al Ajab, sehemu ibaki open kwa public,watalii waendelee kutembelea, sehemu iwe ni private ya makazi yake, watakao taka kupita na kumuona tuu akiwa amekaa kwenye kiti chake cha enzi cha Sultani, malipo yawe $100, kumsalimia $500 na kuzungumza na Sultan kwa dakika 5 ni $1000, matajiri wote wa kiarabu toka dunia kote watakuja Zanzibar, Sultan ndie atageuka kivutio kikubwa cha utalii Zanzibar!。
  4. Sehemu ya mapato hayo yatumike kumtegemeza na ziada iingie serikalini kama mapato ya utalii。
  5. Katika kuzungumza nae kwa dakika 5,inawekwa caveat,sio kuzungumzia machungu ya Mapinduzi,kuzungumzia mema na mazuri tuu ya Zanzibar。
  6. Media turuhusiwe kufanya mahojiano for healing process,tusimuulize maswali ya maudhi kuepuka kutonesha makovu ya Mapinduzi。Mfano mimi sitamuuliza kitu kuhusu hoja hii Kumbe Sultan Jamshid Alifurahia Kuuawa kwa Karume!. Alitaraji Kurejea Kama Sultani, Kumbe...
  7. Zanzibar ianzishe truth and reconciliation commission watu waruhusiwe to vent,hivyo to heal machungu ya mapinduzi。
  8. Decemba 10 iwe ni siku ya mapumziko ya uhuru wa Zanzibar,sio lazima iadhimishwe kwa shamra shamra,inaweza kubadili jina ikaitwa Sultan Day。
  9. Neno Matukufu kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,lisiendelee kutumika,yaitwe tuu Mapinduzi ya Zanzibar na vibwagizo Mapinduzi Daima, na Tutayalinda kwa gharama yoyote, tuachane nayo ili kuponya wapinga mapinduzi
  10. Falsafa ya 4R za Samia,itumike hadi Zanzibar,mshindi wa kweli wa uchaguzi wa Zanzibar atangazwe,mfano mzuri ni huu Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda na ili kumuondolea posibility ya aibu ya kushindwa,nimetoa ushauri hapa kwenye HII
P
 
Ccm Yako huijui bado vizuri wewe.....hapo namba 10 utasubiri Sana.
 
X anarudi nyumbani kwa mkewe kikongwe
 
Umemlenga nani kwa ujumbe huo?
Wewe si ndio shabiki wa huyu mama, sasa unadhani nimemwandikia nani mwingine.

Katika move ambayo huyu mama kaitibua CCM ni hii hasa upande wa Zanzibar.

Yaani ni kiazi, hamna kitu kichwani kwake.

Subiri utaelewa baadae namna gani kawakera CCM.

Mambo mengine mpaka uone matokeo yake ndio utaelewa.

Ugomvi wake utakuwa na CCM Zanzibar kwenda, mbele; yaani hana akili hata chembe.

Watch it
 
Ndio view ya Wazanzibari hio? Ama nyie wa Bara? Wazanzibari wengi ukiwaambia wachague utawala wa Sultan na huu wa sasa hawataki wa sasa, uchaguzi kila mwaka unaonesha.

Pia masultan wa Znz wengi wa miaka 100 iliopita ni weusi kushinda hata wewe.
Wazanzibar wako tayari kurudishwa utumwani chini ya mwarabu sultan wa Oman
 
Tatizo wazanzibar wanafikra za utumwa vichwani mwanao hata Mombasa Kuna jamii ya kiarabu lakini huwezi kusikia watu wa Mombasa wakiwalilia waOman waje wawatawale
Sababu Znz ni mix ya Waoman na wabantu, hilo ni jambo ambalo huwezi ukalifuta.

Oman ni Nchi ya kiarabu ila viongozi wao wote wana Asili ya Africa, na hutasikia Waoman wakilalamika kwanini tunatawaliwa na Wa Africa.

Masultan walileta maendeleo thats a fact, Wazanzibari waliheshimika, Znz waliingia mkataba na mataifa kama Marekani wasinunue kitu chochote toka kwa yoyote Africa bila kupitia wao, nani leo ana ubavu kama huu?
 
Vipi kuhusu wahindi na waarabu 5,000 waliookufa wakati wa mapinduzi ? Ni nani atafidia familia zao?
Watafidiwa na makwao walipotoka.....kikubwa hili bara ni la mu Afrika watajua wao walipotoka huko na kuja kufanya ufedhuli wao.......mtu mweusi alijibu mapigo maana walianza wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…