Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Mchezo huu hauhitaji hasira, mtu ni kwao, karibu sana Sultan Jamshid.

TOKA MAKTABA:
AIISHUKURU SERIKALI YA TANGANYIKA KWA KUMPA NJIA YA KUPITA KUELEKEA UGAIBUNI

Karibu sana nyumbani.

Hapa clip fupi akitoa shukrani kwa serikali ya Uingereza kumpatia hifadhi na pia serikali ya Tanganyika kwa kumpa ruhusa kupita Dar es Salaam baada ya mapinduzi ili afanye taratibu za kwenda Uhamishoni


View: https://m.youtube.com/watch?v=TKE2C5svBLo
Maafisa nchini Kenya walifikiri kwamba kuingia kwa Sultan Mombasa kunaweza kusababisha hali tete ya usalama na misukosuko ya Waarabu wanaoishi Mombasa; hivyo, iliamuliwa kutompa kimbilio, wala kwa wasaidizi wake; badala yake, iliamuliwa waelekee Dar es-salaam.

Jijini Dar es-Salaam, Sultani na msafara wake waliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika nyumba mbili za serikali zinazolindwa na polisi na ziko katika eneo la kifahari la Oyster Bay.

Nyumba moja ilitengwa kwa HM. Sultani na familia yake huku wa pili akikalisha wasaidizi wake. Walikaa Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 18 Januari 1964, siku ambayo walisafiri kwa ndege kuelekea Uingereza
 
Dah. Hatimaye watu wazima wamepata ujasiri wa kukabiliana na nuru (light) baada ya kujificha gizani miaka 60.

We can easily forgive a child for being afraid of the dark but the real tragedy of life is when men become afraid of the light - Plato

Ukweli hupanda ngazi na, hakika, utafika.
 
Sasa mapinduzi yatakaaje waungwana, je atatmbulishwa kama Sultani Jamshid au kama Bw. Jamshid?

Wataalamu muongozo wenu muhimu hapa.
Hawakawii kusema wakoloni walikuwa wazungu sio waarabu😂😂😂🤣🤣 maana hao wazenji wametekwa na waarabu hao,mpaka sasa huwa wanasema waarabu ni ndugu zao🤣🤣🤣
 
sultan sio mwanasiasa ujio wake hauna uhusiano na mambo yenu ya kisiasa akifika ataenda msikitini kuswali badae anaenda nyumbani kwake
Kwa hiyo huyu Sultan Freeman ni sultan uchwara!
 
Dunia inaposhuhudia tukio hili la kihistoria, Zanzibar inasimama katika nafasi ya kubadilisha urithi wake kuwa simulizi ya mshikamano na heshima ya pande zote.
Issa AlHarthy.
Waingereza siyo wajinga wa muhifadhi huyu ndugu miaka yote hiyo bure! Tena nchini mwao. Kikubwa tujue Waingereza wametuandalia nini ili tuwe tayari kulipokea hicho kilichoandalawi!

Karibu sana "Sultan" Jamshid bin Abdullah!!
 
taarifa hii ya kurejea Sultan isije kuwa ni fake story,kwasababu nime cross check na Msemaji wa SMZ, Charles Hillary, wao hawana taarifa za ugeni huu, labda kama anakuja Zanzibar on a private visit kama mtalii tuu, then hahitaji kutoa taarifa popote bali kugongewa tuu visa na kuingia Zanzibar。

P
 
Unaweza mtoa nyani porini lakini huwezi litoa pori kwenye kichwa Cha nyani
 
Tunamtaka Richard Turnbull Tanganyika ili tusameheane naye pia😒
Nilitarajia utawauliza CCM enzi za Maalim Seif CUF, hoja yao kubwa ya kampeni ilikuwa kudai hatari ya hao Hizbu (CUF) kurejesha utawala wa sultani na waarabu Zanzibar.

Kelele zao zilikuwa dhidi ya “machotara wa Hizbu” (CUF) kumrejesha sultani huko Zanzibar!

Leo wanataka maridhiano na Sultani? Good. Inasemwa ukweli hupanda ngazi. Nasubiri ukweli utakapofika kauli ya mwisho itakuwaje.

Hii nchi tumeishi kwa uongo miaka yote. Mengi yatawekwa sawa muda muafaka ukifika.
 
Leta source ya story yako kati ya Iddi Amin na Okello
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…