Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

View attachment 3186808

Mnamo Januari 9, 2025, Zanzibar itashuhudia tukio la kihistoria itakapompokea Sultan Jamshid bin Abdullah kurejea kwenye pwani zake. Hili ni tukio muhimu sana kihistoria, kwani mtawala wa zamani wa Zanzibar anarudi baada ya miongo sita ya uhamisho nchini Uingereza na Oman, kufuatia kuondolewa kwake madarakani wakati wa mapinduzi ya 1964.

Cc Pascal Mayalla

Maelezo kuhusu jinsi ziara hii ilivyopangwa bado hayajafahamika, lakini umuhimu wake hauwezi kupuuzwa. Kurudi kwa Sultan Jamshid kunawakilisha ishara ya upatanisho wa kipekee kutoka kwa serikali ya Zanzibar. Ziara yake inaweza kuwa daraja kati ya enzi za kabla na baada ya mapinduzi, ikichochea mshikamano na uponyaji wa kitaifa.

Zanzibar inaweza kuchukua nafasi hii kumwalika Sultan kuishi katika mojawapo ya majumba yake ya zamani kama raia wa kawaida. Hatua kama hiyo haitaimarisha tu taswira ya Zanzibar kimataifa bali pia inaweza kuinua sekta yake ya utalii, kwani uwepo wake utavutia shauku kubwa. Zaidi ya hayo, inaweza kuashiria sura mpya ya upatanisho kati ya Sultan na serikali ya mapinduzi, ikitoa mfano wa maendeleo na mshikamano.

Dunia inaposhuhudia tukio hili la kihistoria, Zanzibar inasimama katika nafasi ya kubadilisha urithi wake kuwa simulizi ya mshikamano na heshima ya pande zote.
Issa AlHarthy.
Ujio wa Sultan Zanzibar uende sambamba na kufutwa neno MAPINDUZI kwenye utambulisho wa serikali ya Zanzibar, badala yake ibakia kutamkwa tu Serikali ya Zanzibar.
Kama tumeamua kuwa na mshikamano basi tuonyeshe kwa vitendo.
 
Ujio wa Sultan Zanzibar uende sambamba na kufutwa neno MAPINDUZI kwenye utambulisho wa serikali ya Zanzibar, badala yake ibakia kutamkwa tu Serikali ya Zanzibar.
Kama tumeamua kuwa na mshikamano basi tuonyeshe kwa vitendo.
kabisa, iitwe serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) hii iambatane na kufuta siasa za vyama, vyama vibaki kwenye kampeni tu na baada ya uchaguzi serikali iundwe kutoka wajumbe vyama vyote
 
Watu wanaongea tu hawajui km mpk Leo tupo ambao hatusahau walichofanyiwa ndugu zetu. Kuna watu mpk Leo wanaishi na trauma.
Ati mapinduzi matukufu.....mapinduzi my foot
Ndio maana nchi mpk Leo imekaa km imelaaniwa dhiki kila siku zinazidi, kumbe damu za watu zinalipa
Wataje hao wanaoishi na trauma!! Kinyume cha hapo ni hisia zako tu
 
Ukitaka kujua huyo mama hana akili, ngoja siku huyo Jamsheed atue Zanzibar ndio aelewe.

Jinsi wazanzibari huko alipotoka walivyogawanyika; hata siasa za kwao hazijui.

Watch this space, akili hana kabisa huyo mama.
Wewe ni mhafidhina tu, hakuna jema lolote unaliona kwa Serikali ya Samia
 
taarifa hii ya kurejea Sultan isije kuwa ni fake story,kwasababu nime cross check na Msemaji wa SMZ, Charles Hillary, wao hawana taarifa za ugeni huu, labda kama anakuja Zanzibar on a private visit kama mtalii tuu, then hahitaji kutoa taarifa popote bali kugongewa tuu visa na kuingia Zanzibar。

P
Ni vyema aalikwe sasa....
 
Huo auwezi kuwa ushauri wa CCM halisi Zanzibar hata chembe.

Mama ni wa hovyo kweli, hana akili hata kidogo.

God knows Kafikaje hapo halipo (ndio Kudra zenyewe za mungu).

The woman is kaput (kichwani zero).
Hana akili lakini anatawala watu 61 milioni na wewe ukiwapo. Wewe Mayor Quimby ni kiazi mbatata kweli.

Yaani unamuogopa mzee mwenye miaka 95 analiyeomba kurudi kuja kumaliza maisha yake ya mwisho mahali alipozaliwa.

Makaburu walibagua, walitesa , waliua na kuwafunga akina Mandela vifungo vya maisha.
Mwisho blacks under Mandela walitokomeza ubaguzi, wakasamehe kwani walichopigania ni Africa Kusini yenye kuheshimu haki sawa kwa watu wote . Alihamasisha msamaha kwa makaburu bila kulipiza kisasi.
Hivyo kusahau mabaya ya waarabu na kumkubali Sultani arudi ni jambo la afya saana.
 
Unazungumziaje watumwa aliowauza uarabuni
Hata akina Mirambo, Mkwawa, Abushiri waliuza watumwa.

Msiwalaumu waarabu kwa kuuza watumwa, waalaumu waliowauzia waarabu watumwa
 
Ukweli ni kwamba wa Zanzibar wengi wanapenda kujiona Waarabu hasa Bi.Ushungi maana alishawahi sena ujombani kwake ni Oman.
Wakati walio wengi asili yao ni Wamatumbi, Wanyamwezi, Wayao n.k waliokuwa wanachukuliwa utumwani.
Wivu tu. Ukitaka wawe wajomba zako wewe
 
Ile ni roho ,itawatafuna wazanzibari na watangayika muda sio mrefu.

Mungu alimtimua shetani kwenye utawala wake na kukiondoa kabisa kiti chake na nafasi yake kule mbinguni .

Roho ya utumwa imerejea rasmi na itapata nguvu kupitia dini.
Wacha kuhubiri ulokole hapa, hili siyo jukwaa la Mwamposa. Njoo na substance
 
Mkuu Situ, Stuxnet ,hii ni habari njema sana,na najisikia faraja sana kwa jambo uliloshauri litekelezwe,nilianzia hapa Dear Mama, Can you Offer An Unconditional Amnesty to All Zanzibaris Waliokimbia After Revolution, Incl Sultan, Be Free to Return & Start Afresh? nikaja Voices From Within: Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said atafurahi zaidi kama atarudi Zanzibar. Rais Samia, Rais Mwinyi, sameheni, utabarikiwa sana! halafu likatekelezwa Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni hata kama utekelezaji huo hauhusiani na ushauri wako,lakini ulishauri Sultani ajengewe mazingira ya kurejea Zanzibar, sasa anarejea Zanzibar, mtu unafarijika。

Kuhusu kurejea Sultani Zanzibar, Ushauri wangu ni huu。
  1. Serikali ya Zanzibar igharimie kila kitu kwenye ziara hiyo, apokelewe na kutembezwa na ving'ora as a healing process ya machungu aliyopitia。
  2. Aandaliwe an ad hoc protocal ya Sultan mpinduliwa,kwa jinsi ile ile katiba ya JMT,haitambui katiba ya Zanzibar lakini protocal inawatambua na wana ving'ora。
  3. Akabidhiwe part ya lile kasri lake la Beit Al Ajab, sehemu ibaki open kwa public,watalii waendelee kutembelea, sehemu iwe ni private ya makazi yake, watakao taka kupita na kumuona tuu akiwa amekaa kwenye kiti chake cha enzi cha Sultani, malipo yawe $100, kumsalimia $500 na kuzungumza na Sultan kwa dakika 5 ni $1000, matajiri wote wa kiarabu toka dunia kote watakuja Zanzibar, Sultan ndie atageuka kivutio kikubwa cha utalii Zanzibar!。
  4. Sehemu ya mapato hayo yatumike kumtegemeza na ziada iingie serikalini kama mapato ya utalii。
  5. Katika kuzungumza nae kwa dakika 5,inawekwa caveat,sio kuzungumzia machungu ya Mapinduzi,kuzungumzia mema na mazuri tuu ya Zanzibar。
  6. Media turuhusiwe kufanya mahojiano for healing process,tusimuulize maswali ya maudhi kuepuka kutonesha makovu ya Mapinduzi。Mfano mimi sitamuuliza kitu kuhusu hoja hii Kumbe Sultan Jamshid Alifurahia Kuuawa kwa Karume!. Alitaraji Kurejea Kama Sultani, Kumbe...
  7. Zanzibar ianzishe truth and reconciliation commission watu waruhusiwe to vent,hivyo to heal machungu ya mapinduzi。
  8. Decemba 10 iwe ni siku ya mapumziko ya uhuru wa Zanzibar,sio lazima iadhimishwe kwa shamra shamra,inaweza kubadili jina ikaitwa Sultan Day。
  9. Neno Matukufu kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,lisiendelee kutumika,yaitwe tuu Mapinduzi ya Zanzibar na vibwagizo Mapinduzi Daima, na Tutayalinda kwa gharama yoyote, tuachane nayo ili kuponya wapinga mapinduzi
  10. Falsafa ya 4R za Samia,itumike hadi Zanzibar,mshindi wa kweli wa uchaguzi wa Zanzibar atangazwe,mfano mzuri ni huu Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda na ili kumuondolea posibility ya aibu ya kushindwa,nimetoa ushauri hapa kwenye HII
P
Well put, naamini system wanachukua notes
 
Wewe si ndio shabiki wa huyu mama, sasa unadhani nimemwandikia nani mwingine.

Katika move ambayo huyu mama kaitibua CCM ni hii hasa upande wa Zanzibar.

Yaani ni kiazi, hamna kitu kichwani kwake.

Subiri utaelewa baadae namna gani kawakera CCM.

Mambo mengine mpaka uone matokeo yake ndio utaelewa.

Ugomvi wake utakuwa na CCM Zanzibar kwenda, mbele; yaani hana akili hata chembe.

Watch it
Wewe ni tabular rasa kabisa. Hamna namna ya kukusaidia, labda tukuwekee akili bandia
 
Well put, naamini system wanachukua notes
nilikuuliza source ya hii habari sio fake news?。Mapendekezo 10 Muhimu, Ujio Sultan wa Zanzibar, apewe Ving'ora, Kasri, atangaze Utalii,Mshindi wa Kweli Zanzibar 2025 Atangazwe To Heal Zanzibar!。kwasababu nime cross check na Msemaji wa SMZ, Charles Hillary, wao hawana taarifa za ugeni huu, labda kama anakuja Zanzibar on a private visit kama mtalii tuu, then hahitaji kutoa taarifa popote bali kugongewa tuu visa na kuingia Zanzibar。

P
 
Naona waarabu wa Zanzibar (bara la watu weusi) wanayo furaha kubwa sana kumkaribisha mkoloni wao na aliyewaketea dini.
 
Makaburu walibagua, walitesa , waliua na kuwafunga akina Mandela vifungo vya maisha.
Mwisho blacks under Mandela walitokomeza ubaguzi, wakasamehe kwani walichopigania ni Africa Kusini yenye kuheshimu haki sawa kwa watu wote . Alihamasisha msamaha kwa makaburu bila kulipiza kisasi.
Hivyo kusahau mabaya ya waarabu na kumkubali Sultani arudi ni jambo la afya saana.
Maneno ya busara sana haya。
P
 
Muislamu mwenzangu nimuangalie akipigwa na maadui kisha nikuangalie tu hahaa😄 patachimbika mzee

hahah mbona somalia 99% “waislamu wenzako” wanapigwa kila siku na guess who? saudi arabia, anayefund al shabaab kuuwa waislamu somalia ni saudi arabia “muislamu mwenzako”, anayeuwa na kutesa waislamu yemeni ni saudia na emir wa emitate pia “ waislamu wenzanko” mbona hapachimbiki? mashehe kibao walifungwa wakati wa awamu ya 4 na “muislamu mwenzako” mbona haukupachimba?
 
Back
Top Bottom