Hii mifumo ya kimaisha na shule zenu inalemaza sana watu akili.
Just imagine, Okello ametoka huko Kijijini kwao, tena miaka hiyo, akaenda Kampala, akajifunza mambo kadhaa, akaamua kwenda Zanzibar akiwa na miaka 22 akaenda kuwasaidia kupambana na Sultan hadi kumuondoa. Akakabidhi madaraka kwa raia wa pale, then akafukuzwa.
Leo kijana gani katika umri huo anaweza akafanya hayo.
Ila Iddi Amin alikuwa mtu mzuri sema makosa yake yalikuwa ni 'deadly/grave'. Okello alitengwa na akateseka sana nchini Uganda kiasi cha kukosa hata hela ya kula, akalazimika kurudi kijijini. Iddi Amin alipoingia alimfuata Okello na kumuahidi uwaziri ili waiongoze Uganda, lakini Okello akachomoa, Iddi Amin hakukata tamaa, akamuahidi umakamo wa rais, lakini Okelleo akachomoa, akabembelezwa sana, akakubali kwa masharti apewe urais, Iddi Ammin ndiye awe Makamo...hapo ndiyo story ilipoanzia na kuishia