Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Mkuu wazanzibari huwa ni watu wepesi wa kusahau.
Huyo jamaa wanaye mualika kama ngamia, ataingiza kichwa , halafu baadaye watashitukia hela ya mwarabu inawatoa madarakani waafrika,
Believe you me.
mwarabu ana tatizo gani?
 
aliyeondolewa madarakani ni waziri mkuu Shamte, na wala nafasi ya sultan hakuna ilipofutwa na hata wakati wa mkoloni hakuwa na mamlaka ya kidola alisafiri tu kama watu wengine wanavyosafiri, na haji kutawala anakuja kuwa ceremonial leader kama chifu wa wahehe au kabaka mutesa wa uganda

So point yako ni nini, kuwa cheo cha usultan bado kipo zanzibar kwa hiyo anarudi kwenye kiti chake.. unaposema anarud kama ceremonial leader on what grounds? Lengo ni nini hasa ikiwa huko dunia aliishi kama raia wa kawaida inakuwaje mumlete na kumtambulisha kama kiongoz .. na kusema anakuja kama ceremonial leader kwa katiba ipi ambayo inatambua usultani?

Kama ana ndugu Zenji aje kama raia wa kawaida infact anatakiwa aombe hata visa maana sio raia wa zanzibar kumbuka hatutambui uraia pacha
 
Mtu amesha ondolewa madarakani, asiendekezwe, ama sivyo aliyemleta litamtokea puani.
Huyu Jamshe si sultani tena na hana madaraka yoyote kiutawala.
Kuendekeza kumrudisha ktaamsha hasira zilizolala za tarehe 12/1/1964 na maumivu ya utumwa, ubaguzi na maonevu yote.
Ndo maana nimewauliza waliposema sijui anakuja kuleta upatanishi upatanishi wa nani na nani na yeye anakuja kwa mwamvuli upi maana hana status yoyote kwenye dunia

Maana yake kitendo cha kumleta na kumtambulisha kama sultan wa zanzibar maana yake mnaeazodoa walioyasapoti mapinduzi na kuwaonyesha haikuwa sawa
 
Nafahamu mko hapa kupima upepo, ila katika jambo ambalo SAMIA asijethubutu hata kulizungumzia ni hili. Siku anafanya hivi ndiyo itakuwa mwisho wake. Kubwa zaidi Jamshid atakuwa ni MPUMBAVU asiyejifunza endapo atalazimisha kufika Zanzibar.
 
Huyo jamaa Jamshed aanze kwa kuomba radhi kwa babu zake kuuza watanganyika kama watumwa.
Na kwa vile usultani alisha vuliwa akaribishwe kama raia wa kawaida.
Kwanini usiwalaumu Machifu wa Kitanganyika waliouza mateka wao kwa waarabu? Kama akina Milambo na Abushiri wasingeuza watumwa ina maana waarabu wasingekuwa na mtu wa kumuuza.
 
Majumba yake ya zamani tena? Na nimesoma kuwa anarudi kwenye pwani zake?

Kwa hiyo sultan bado anatambulika kama mtawala au? Na hayo majumba yake bado yanatambulika kama
Mali zake.. basi msiishie kwenye majumba tu mrudishien na milki yake

Huo upatanisho unaosema hiyo ziara itasaidia kurejeshwa ni upatanisho upi yaani mnataka kusema mapinduzi yalikosewa hakutendewa haki.. ikiwa hata huko alikokimbilia (oman) he was nobody kiasi kwamba alifukuzwa huko na akapigwa ban asirudi akakimbilia UK wakamsitiri akawa anaishi portsmouth na familia yake kama mtu wa kawaida hadi mwaka 2020 ambapo ombi lake la kurudi nchini mwake Oman lilikubaliwa kwa shart kuwa hatambuliki kama Sultan bali raia wa kawaida sasa huku mnakomleta kama sultani mnataka mfikishe ujumbe upi.. kwa wanzanzibar na watu wa Oman kuwa je nyie bado mnamtambua kuwa ni Sultan wa Zanzibar au?
Sasa unadhani anaweza kuwa Sultan kwa Katiba ipi? Kwanza ZNZ siyo sovereign state, ni sehemu ya muungano wa Tanzania.

Pili mzee mwenye miaka 95 pengine ana dementia na alzheimer, atapata wapi hizo nguvu unazomuogopea? Huyu ametaka kuja kumailizia uhai wake mahali alipozaliwa tu.
 
Kwanini usiwalaumu Machifu wa Kitanganyika waliouza mateka wao kwa waarabu? Kama akina Milambo na Abushiri wasingeuza watumwa ina maana waarabu wasingekuwa na mtu wa kumuuza.
Kwa hiyo unaungana na slave traders waarabu?
 
Ndio view ya Wazanzibari hio? Ama nyie wa Bara? Wazanzibari wengi ukiwaambia wachague utawala wa Sultan na huu wa sasa hawataki wa sasa, uchaguzi kila mwaka unaonesha.

Pia masultan wa Znz wengi wa miaka 100 iliopita ni weusi kushinda hata wewe.
Waarabu weusi sio.
We Jamaa Unazingua
 
So Zanzibar ya leo wakazi wa mwanzo kabisa walikuwa ni waoman au kuna namna walifanya wakaonekana wao zaidi wakahodhi madaraka?
kwanza ufahamu ukanda wa pwani wote huu ndio ulijulikana kama Zanzibar na sio vile visiwa kuanzia pwani ya kenya hadi msumbiji.

historia inaanzia mbali kabisa kwa mtu anayeitwa "Almuli" chief wa kilwa huyu alikua akiongoza kisehemu kidogo cha kilwa, at same time Iran mfalme wao alifariki, aliacha watoto kama 8 ambao walikua wakigombania urithi, mtoto mmoja alikua ni chotara mama toka Africa na baba Mfalme wa Iran, huyu mtoto alishindwa kupata ufalme akakimbilia Africa na watu wake, akaenda Mogadishu lakini kule hakupatana na wasomali akaja chini hadi Kilwa, Almuli akakubali kumuuzia kisiwa akipewa nguo nyingi zitakazozunguka kisiwa kizima, wakampa wakachukua kisiwa, inasadikika Almuli baadae alighairi akarudi awarudishie nguo ila jamaa walichimba ardhi na ndio Kukawa na kilwa kisiwani.

hio ni miaka ya kuanzia 900, kuanzia hapo hadi miaka ya 1500 kilwa ika expand kwenda hadi sofala hadi lamu, wakaipiga gape hadi mogadishu, wakati huo Oman wanakuja na Monsoon wind kufanya biashara ila sio watawala. miaka ya 1500 portugal wakaja, tofauti na watu wa middle east waliokuwa wakifanya biashara portugal walikua hawajui kufanya biashara wao wakija wanakuja na jeshi kama ni soko wanasomba na kuiba vitu vyote, so watawala wote wa pwani wakaanza kupigana vita na portugal. kilwa at that time ilikua ni trade Empire kila mji ulijiongoza wenyewe

sababu portugal walikua juu kivita waliwapiga watu wa pwani, watu wa pwani wengi walikuwa ni waisilamu waliomba msaada kwa Ottoman Empire likaja jeshi chini ya Mir Ali kupigana na Portugal nalo likapigwa.

turudi Oman sasa, kule nako mfalme Wa Oman alipinduliwa akakimbilia India ya zamani, akapokelewa na wabulushi akapewa eneo akakusanya kodi, akarudi na jeshi la wabulushi akampiga aliempindua na kuirudisha Oman, wabulushi walikua vizuri sana kwenye vita, portugal alikuwa na maeneo kuanzia India hadi huku kwetu, Oman alimpiga Portugal kule Asia na kumshinda, sababu Oman walikua na interest kibiashara East Africa wakaja kuwasaidia watu wa pwani na jeshi lao la wabulushi, kama tunavyojua Mreno akapigwa na kutolewa East Africa.

miaka hio ukaanza Utawala wa Oman sasa huku kwetu, Empire ya Oman kama ilivyo Kilwa haikuingilia Tawala za Ki Africa, walikua wanafanya Biashara tu na kama nilivyosema huko juu the so called makabila makubwa nchi hii ni makabila yaliyotoboa kwa kufanya biashara na Oman kama vile Wachaga, Wahaya etc, na tofauti na Ukoloni Zanzibar haikuwa koloni la Oman bali vice versa was true, Mfalme wa Zanzibar ndio alitawala Oman.

mwaka 1861 ndio ikagawanyika, ZNZ na Oman vikatengana na Znz ikawa na MAsultan wake, ukitoa masultan wa mwanzo masultan wote kuanzia mwisho miaka ya 80 hadi Jamshid walikua ni weusi ama machotara.
 
View attachment 3186808

Mnamo Januari 9, 2025, Zanzibar itashuhudia tukio la kihistoria itakapompokea Sultan Jamshid bin Abdullah kurejea kwenye pwani zake. Hili ni tukio muhimu sana kihistoria, kwani mtawala wa zamani wa Zanzibar anarudi baada ya miongo sita ya uhamisho nchini Uingereza na Oman, kufuatia kuondolewa kwake madarakani wakati wa mapinduzi ya 1964.

Cc Pascal Mayalla

Maelezo kuhusu jinsi ziara hii ilivyopangwa bado hayajafahamika, lakini umuhimu wake hauwezi kupuuzwa. Kurudi kwa Sultan Jamshid kunawakilisha ishara ya upatanisho wa kipekee kutoka kwa serikali ya Zanzibar. Ziara yake inaweza kuwa daraja kati ya enzi za kabla na baada ya mapinduzi, ikichochea mshikamano na uponyaji wa kitaifa.

Zanzibar inaweza kuchukua nafasi hii kumwalika Sultan kuishi katika mojawapo ya majumba yake ya zamani kama raia wa kawaida. Hatua kama hiyo haitaimarisha tu taswira ya Zanzibar kimataifa bali pia inaweza kuinua sekta yake ya utalii, kwani uwepo wake utavutia shauku kubwa. Zaidi ya hayo, inaweza kuashiria sura mpya ya upatanisho kati ya Sultan na serikali ya mapinduzi, ikitoa mfano wa maendeleo na mshikamano.

Dunia inaposhuhudia tukio hili la kihistoria, Zanzibar inasimama katika nafasi ya kubadilisha urithi wake kuwa simulizi ya mshikamano na heshima ya pande zote.
Issa AlHarthy.
Yaani aliondoshwa kwenye utaeala miaka 60 iliyopita mpaka Leo yupo hai?
 
😀
Watarudisha utawala wake kimtindo
Huyo mfalme sio kaja kutembea tu,huwezi jua yaliyo nyuma ya pazia.
Labda kuna makubaliano ya aina fulani ikiwa atarudi Zenj.
Na siyo ishara nzuri kwa baraza la mapinduzi.Mwenye nchi anakuja.
 
Kwa hiyo una support slave trade, kuonewa kwa waafrika, na mapinduzi ya 1964 ya waafrika kujikomboa, kwako ni upuuzi tu?
boss slave trade ni mbaya ila hakuna ambaye hajafanya, tena afadhali hao waarabu walikua na ustaarabu kidogo soma slave trade ya machief ni mbaya kupita maelezo, chief anakufa watumwa kadhaa watoto wa kike vigoli wanazikwa nae, mfalme anatoka tu na farasi wake anaenda vijijini anakamata watumwa etc.

waarabu mtumwa aliweza kujinunua mfano wewe umeuzwa utumwani kwa laki 5, ukaenda znz mashamba ya karafuu, kule unalipwa 20,000 kwa mwezi, ukisave hela zako zikatimia laki 5 unanunua uhuru wako na kuondoka. na hao walikua ni watu wa bara. watu wa pwani walikua hawauzwi kabisa utumwani, mfano wazaramo tabia yao walikua wanajiuza wenyewe kwenye utumwa znz, ndugu anachukua hela akifika kule anapanda kidau anarudi zake huku, wakapiga marufuku kununua mzaramo utumwani.
 
Mimi ni mkristo siwezi tetea maovu ya wazungu kwa sababu tu walileta ukristo wazungu pamoja na warabu walifanya biashara ya utumwa hata utumie lugha ipi huwezi badilisha huu ukweli

Njoo kwa waislamu wanatetea kile alichofanya mwarabu hata kama ni kibaya vipi sababu tu aliwaletea dini waislamu akili zenu zimefungwa

Utawala wa sultan umetesa wafrika sana yaani huyo sultan kwa nchi wanaojielewa anatakiwa akitua tu uwanjani aelekee ukonga familia yake imetesa watu sana

Zanzibar haikuwa trading port bali sehemu ya mateso kwa waafrika ashukuriwe sana john okelo kwa kazi nzuri aliyofanya
kama unachosema ni kweli basi wa znz wangeipenda kweli serikali yao na CUF/ACT zingekua vyama kama UDP ila tunajua kitu gani kinaendelea ZNZ, inatumika nguvu nyingi toka bara kuwaweka madarakani, wa ZNZ wenyewe hawaitaki. ikiwa ZNZ wenyewe hawataki mapinduzi wewe nani bara kuwasemea?

nikikuuliza sasa hivi mwanamuziki wa miaka 100 iliopita bara ama Africa humjui hata mmoja ila znz wapo na mpaka leo wanafanyiwa remake ya nyimbo zao, marekani Bahari yake anapakana na West Africa ila alikua anaacha NCHI zote Anakuja ZNZ, umeme, barabara za kisasa, mpaka nyumba zenye lift zilikuwepo way before.

viongozi wao walikuwa smart wamesoma, we mpaka mtu mweusi upo huku mwisho wa dunia unakuwa coronated kama Sir sio jambo la kitoto, kaangalie serikali ya 1963 iliopinduliwa speech yao UN then compare na hawa wa leo.
 
boss slave trade ni mbaya ila hakuna ambaye hajafanya, tena afadhali hao waarabu walikua na ustaarabu kidogo soma slave trade ya machief ni mbaya kupita maelezo, chief anakufa watumwa kadhaa watoto wa kike vigoli wanazikwa nae, mfalme anatoka tu na farasi wake anaenda vijijini anakamata watumwa etc.

waarabu mtumwa aliweza kujinunua mfano wewe umeuzwa utumwani kwa laki 5, ukaenda znz mashamba ya karafuu, kule unalipwa 20,000 kwa mwezi, ukisave hela zako zikatimia laki 5 unanunua uhuru wako na kuondoka. na hao walikua ni watu wa bara. watu wa pwani walikua hawauzwi kabisa utumwani, mfano wazaramo tabia yao walikua wanajiuza wenyewe kwenye utumwa znz, ndugu anachukua hela akifika kule anapanda kidau anarudi zake huku, wakapiga marufuku kununua mzaramo utumwani.
Basically unajidhalilisha kwa kuunga mkono arab slave trade.
 
View attachment 3186808

Mnamo Januari 9, 2025, Zanzibar itashuhudia tukio la kihistoria itakapompokea Sultan Jamshid bin Abdullah kurejea kwenye pwani zake. Hili ni tukio muhimu sana kihistoria, kwani mtawala wa zamani wa Zanzibar anarudi baada ya miongo sita ya uhamisho nchini Uingereza na Oman, kufuatia kuondolewa kwake madarakani wakati wa mapinduzi ya 1964.

Cc Pascal Mayalla

Maelezo kuhusu jinsi ziara hii ilivyopangwa bado hayajafahamika, lakini umuhimu wake hauwezi kupuuzwa. Kurudi kwa Sultan Jamshid kunawakilisha ishara ya upatanisho wa kipekee kutoka kwa serikali ya Zanzibar. Ziara yake inaweza kuwa daraja kati ya enzi za kabla na baada ya mapinduzi, ikichochea mshikamano na uponyaji wa kitaifa.

Zanzibar inaweza kuchukua nafasi hii kumwalika Sultan kuishi katika mojawapo ya majumba yake ya zamani kama raia wa kawaida. Hatua kama hiyo haitaimarisha tu taswira ya Zanzibar kimataifa bali pia inaweza kuinua sekta yake ya utalii, kwani uwepo wake utavutia shauku kubwa. Zaidi ya hayo, inaweza kuashiria sura mpya ya upatanisho kati ya Sultan na serikali ya mapinduzi, ikitoa mfano wa maendeleo na mshikamano.

Dunia inaposhuhudia tukio hili la kihistoria, Zanzibar inasimama katika nafasi ya kubadilisha urithi wake kuwa simulizi ya mshikamano na heshima ya pande zote.
Issa AlHarthy.
Tanganyika hiyooo inarudi taratibu
 
kama unachosema ni kweli basi wa znz wangeipenda kweli serikali yao na CUF/ACT zingekua vyama kama UDP ila tunajua kitu gani kinaendelea ZNZ, inatumika nguvu nyingi toka bara kuwaweka madarakani, wa ZNZ wenyewe hawaitaki. ikiwa ZNZ wenyewe hawataki mapinduzi wewe nani bara kuwasemea?

nikikuuliza sasa hivi mwanamuziki wa miaka 100 iliopita bara ama Africa humjui hata mmoja ila znz wapo na mpaka leo wanafanyiwa remake ya nyimbo zao, marekani Bahari yake anapakana na West Africa ila alikua anaacha NCHI zote Anakuja ZNZ, umeme, barabara za kisasa, mpaka nyumba zenye lift zilikuwepo way before.

viongozi wao walikuwa smart wamesoma, we mpaka mtu mweusi upo huku mwisho wa dunia unakuwa coronated kama Sir sio jambo la kitoto, kaangalie serikali ya 1963 iliopinduliwa speech yao UN then compare na hawa wa leo.
Karume aliwasaliti wakina okelo na wenzake walioshiriki mapinduz tukufu
Kwa hofu ya usaliti karume akaona auze uhuru ambao hajaupigania kwa nyerere hakuona thaman ya ule uhuru sababu hakuupigania

Okello na wenzake walikua loyal kwake akawasiti ndo chanzo cha migogoro mpaka leo
 
Back
Top Bottom