Zanzibar kuvuliwa uanachama wa CAF hii imekaaje kisiasa?

Zanzibar kuvuliwa uanachama wa CAF hii imekaaje kisiasa?

..hizo ni chokochoko za katiba mpya.

..warudishieni Znz mamlaka yao.

..vinginevyo mashindano ya CAF tushiriki kwa zamu.

..mwaka mmoja washiriki Znz, halafu unaofuatia tushiriki Tz bara.🤣🤣

Cc Kibunango
Juzi kati mbunge wa zamani wa CUF na mwandishi mashuhuri wa BBC tokea Visiwani, aliweka nia ya kugombea nafasi ya Mweyekiti wa TFF.

Jina lake lilikatwa katika hatua za awali kabisa, ikidaiwa kuwa ZFF ni memba wa CAF. Japo kimsingi sio memba rasmi, yeye alitia nia kwa kuwa ni wananchi wa JMT...

Kimsingi katiba ina mapungufu mengi katika kila setka hapa nchini!
 
..walichomtendea Ally Saleh siyo haki.

..kuweka mambo sawa kuwe na chama cha mpira Znz na chama cha mpira Tgk.

..juu ya vyama hivyo kuwe na chama cha mpira cha Tanzania.

..lakini siyo haki kwa Watgk kuhodhi chama cha mpira kwa kujifanya wao ndio Tanzania.
 
😆😆😆si majuzi tu Ally Saleh kafungua shauri dhidi ya TFF kutaka kujua nafasi ya Znz ktk JMT, itakuwa Karia kawachongea nini ?
 
Habari wadau..!

Nyinyi niwajuvi na maguru wa siasa ,je hili swala la Zanzibar kutolewa shirikisho la mpira la CAF na kutoshiriki mashindano yote ya CAF limekaaje kisiasa?
hii naona imekaa sawa na itazidi kuimarisha muungano wetu wa mfano africa na duniani. kwa siku za karibuni kumetokea sintofahamu nyingi za baadhi ya viongozi au maafisa wa Zanzibar kutaka Zanzibar ijulikane na iwakilishwe kama inavyowakilisha Jamhuri ya muungano wa Tanzania jambo ambalo linaleta sintofahamu kubwa sana katika muungano wetu. na pia maadui wa nchi yetu wamekuwa wakilitumia hili kuichagiza zanzibar kudai na hata kujiunga na taasisi ambazo kiuhalisia kuwa mwananchama ni kwa nchi tu hapa namaanisha siyo tanganyika wala zanziba inaweza kujiunga ila TANZANIA. Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kama imelala na haifualtilii kwa ukaribu baadhi ya mambo yanayoendelea zanziba ambayo hayana afya kwa utaifa wetu; mfano zanzibar kwa kusaidiwa na kenya imeweza kuwa mwanachama wa shirika la uuandaaji wa viwango afrika, zanzibar kupitia zbs wameandika barua shirika la uaandaaji wa viwango duniani kutaka kujiunga yenyewe lakini kiuhalisia mashirika haya ili kuwa mwanachama unatakiwa uwe nchi na si sehemu ya nchi na kama zanzibar inaruhusiwa kujiunga na taasisi hizo kwanini na Tanganyika isiruhusiwe?
 
Kupika UROJO tofauti na kusakata KABUMBU
 
Hawajakidhi vigezo.. Hili halina uhusiano na Tanganyika
Ngoja mama wa "chokochoko" aje na AMRI, mwaka huu TFF itoe timu na mwakani ZFA nao wanatoa timu.
Kwa vile amri yake ni sheria MATAGA watashangilia (huku roho zinauma) kuwa "tunampongeza kwa kudumisha muungano"
Wakiambiwa katiba mpya ni muhimu kuondoa fikra hizo wanabisha. Subirini.
 
WATANGANYIKA TUAMKE, KAMA ZANZIBA ITAENDELEA KUKUBALIWA NA SERIKALI YA MUUNGANO KUJIUNGA NA TAASISI NA MASHIRIKA YA KIMATAIFA KAMA NCHI, HII DOUBLE STANDARD, NA TANGANYIKA TUFUFULIWE NA SISI TUFAIDIKE KWA UTANGANYIKA WETU KAMA ZANZIBA
 
Wabadilishe Muundo kuwe na ligi moja itakayojuisha timu za zanzibar, chama cha
mpira cha zanzibar kivunjwe iwe taasisi ya kuendeleza mpira zanzibar ila ubinafsi na ulafu wa madaraka hawatakubali hilo
 
Wabadilishe Muundo kuwe na ligi moja itakayojuisha timu za zanzibar, chama cha
mpira cha zanzibar kivunjwe iwe taasisi ya kuendeleza mpira zanzibar ila ubinafsi na ulafu wa madaraka hawatakubali hilo
UPO SAHII KABISA, KWA AFYA YA MUUNGANO WETU INABIDI MAMBO MENGI YANAYOTUWAKILISHA KAMA TAIFA NA MATAIFA MENGINE YAWE YA MUUNGANO, Kwasasa ni kawaida mzanzibar kujisikia fahari kujitambulisha ametoka zanziba na si tanzania tunapokuwa wote nje, najiuliza hivi kwanini na mimi nisitumia tanganyika?
 
Juzi kati mbunge wa zamani wa CUF na mwandishi mashuhuri wa BBC tokea Visiwani, aliweka nia ya kugombea nafasi ya Mweyekiti wa TFF.

Jina lake lilikatwa katika hatua za awali kabisa, ikidaiwa kuwa ZFF ni memba wa CAF. Japo kimsingi sio memba rasmi, yeye alitia nia kwa kuwa ni wananchi wa JMT...

Kimsingi katiba ina mapungufu mengi katika kila setka hapa nchini!
Ni rais wa tff si mwenyekit
 
Back
Top Bottom