Hatuombi yatokee mabaya hayo ila, naona muvie hii inaongozwa ki-ccm zaidi. CUF wamekaa kimya mno wenzao wanataka kuwa pekenyua mpaka watoke waliko.
Mola na aseme na wakuu wetu, wasiyachukulie kijuu juu maneno haya kwani hata roho ya taahira kichaa ina thamani mbele za Mola wetu. Tutadaiwa. Kwani ni lazima mtu uongoze?? Hukuzaliwa kuongoza, na kama unaotaka kuwaongoza vyema hawataki basi waache walione wenyewe. Mtoto akililia wembe, mpe. Natamani muwape hayo mamlaka kamili yao wanayolilia.
Bara tupo macho, Mmburushi wala Mmanga haingii pale, iwe kwa mlango wa msaada wala dini. Tutawapiga tuu. Lakini, mzalendo wa kweli mwenye uchungu na Zanzibari, asiguswe. Awe Mpemba au Muunguja, asiguswe kwa ajili ya kukusaidia weye ukae madarakani