Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe Bi Awena waambukizwa virusi vya Corona

Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe Bi Awena waambukizwa virusi vya Corona

Pumbafu ndo nini Wewe mjinga, Wewe unakumbushwa kuhusu ulichoandika kuwa kipo hapa toka ijumaa?

Unaleta ujingaujinga hapa Wakati ugonjwa wenyewe ni mafua tu mnapiga keleele, Mimi mwenyewe tangu ijumaa ya wiki iliyopita nimekuwa na huyo korona na hata not nninapoandika sasa ni mzima wa Afya Tele

Piga nyungu tumia limao, tangawizi, swaumu na asali, hakuna ugonjwa wa kuagizia chanjo zenye mashaka na gharama zake ni 16000 kwamtu mmoja
Pumbaf
 
TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

Chama cha ACT Wazalendo kinawajuilisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania, kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe, Bi Awena, pamoja na Wasaidizi wake kadhaa wa karibu, wamethibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi Madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalumu katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya Korona. Hivyo basi, tangu juzi Ijumaa jioni, Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa Madaktari.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa hali ya Maalim Seif pamoja na mkewe zinaendelea vyema kabisa, Viongozi wenzake pamoja na Wanafamilia wamekuwa na mawasiliano naye ya kawaida kila siku.

ACT Wazalendo tunawaomba wanachama wetu, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki ambacho amepumzishwa ili aweze kupona kwa haraka na arudi kuendelea na majukumu yake. Pia, tunarejea wito wetu kwa Watanzania wote kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo
31 Januari, 2021.

Chanzo: TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

MY TAKE:

Hivi karibu Januari 14, 2021 Seif alitembela Chato. Je, Watu aliyokutana nao tahadhari?

Soma: Rais Magufuli: Maalim Seif ni Kiongozi kweli, aliacha 'interest' zake na kutanguliza za Wazanzibari

je ni dhambi ya usaliti kwa CHADEMA ndiyo naye amelipwa>
 
Pumbafu ndo nini Wewe mjinga, Wewe unakumbushwa kuhusu ulichoandika kuwa kipo hapa toka ijumaa?

Unaleta ujingaujinga hapa Wakati ugonjwa wenyewe ni mafua tu mnapiga keleele, Mimi mwenyewe tangu ijumaa ya wiki iliyopita nimekuwa na huyo korona na hata not nninapoandika sasa ni mzima wa Afya Tele

Piga nyungu tumia limao, tangawizi, swaumu na asali, hakuna ugonjwa wa kuagizia chanjo zenye mashaka na gharama zake ni 16000 kwamtu mmoja
Hamna ujanja lazima chanjo iletwe tu hapa
 
Ugua pole Mzee

Mbona mtu kugua unaibeba kwenye ya Siasa!!!!! Mjitambue na kutenfa mengine.. Muendelee kusali na kutoogopa covid-19 mengi hadi muambiwe nini tena.. mpewe plan mufanyaje na familia zenu au.
Upotolo hata ulichokiandika hakijulikani
 
Yaani ACT ndio wanatoa taarifa za Makamu wa kwanza wa Rais ??

Huo ni ukiukwaji mkubwa wa protokali.
Hata akili huna wewe,Maalim ni Mwenyekiti wa ACT wazalendo hivyo kama chama wana haki ya kutoa taarifa ya Mwenyekiti wao.
 
Hata akili huna wewe,Maalim ni Mwenyekiti wa ACT wazalendo hivyo kama chama wana haki ya kutoa taarifa ya Mwenyekiti wao.
Haya ndio matatizo ya kuwapa nafasi vyama vya mifukoni kama ACT na Chadema kila kitu wanaleta uchama uchama tu, wewe unavyoona ni sawa mfano Samia taarifa zake zitolewe na Ofisi ya CCM badala ya ofisi yake??

Ndio maana Mungu anatuepusha Sana na vyama Kama hivi visutuletee majanga tu
 
Back
Top Bottom