Zanzibar: Midoli ya kutangazia nguo zisizo na stara yapigwa marufuku kuwekwa nje ya maduka

Zanzibar: Midoli ya kutangazia nguo zisizo na stara yapigwa marufuku kuwekwa nje ya maduka

Hiyo midoli ilikuwa inatamanisha sana! Unakuta mdoli wa kike umevaa bikini tako lote nje, mapaja yanaonekana. Bora waipige marufuku tu. Ila wanaweza kuivalisha hijabu na ushungu ikalipa tu. Chupi, bikini na brazia wanaozihitaji watazikuta ndani ya duka
 
View attachment 2518430
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Unguja, Rashid Simai Msaraka amepiga marufuku, Wafanyabiashara wa Wilaya hiyo kuweka midoli yenye nguo zisizo za staha nje ya maduka yao.

DC Msaraka ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Mfanyabiashara maeneo ya Kwahani Zanzibar akiwa ameweka midoli hiyo nje ya duka ikiwa imevalishwa nguo ambazo zinadaiwa kupotosha maadili ya Zanzibar hususan kwa Watoto pindi wanapoona midoli hiyo imevishwa nguo hizo

DC Msaraka ameiambia AyoTV kuwa maarufuku hiyo imetokana na Watoto na Vijana kuona vitu visivyo na staha na kupelekea kuvuraga akili za Vijana wa Zanzibar Hatuwakatazi kuwa na midoli hiyo wala hatuwakatazi kufanya biashara hizo ila biashara hizo zifanywe ndani na zisiwekwe nje, Mtu anayetaka kuvaa nguo hizo avae
mwenyewe anajua utaratibu gani wa kuzivaa na wapi azivae"

Chanzo: Millard Ayo

Pia soma
- Hii midoli ya fasheni kwenye maduka inayovalishwa nguo za ndani inavunja maadili

Kukosa kazi huko,hao vijana hawana maadili wawape maadili kwanza hao vijana,pia kama vipi watunge sheria sio kutafuta kiki.[emoji706]
 
Yaani hili taifa lina vituko🤣 linafanya kila namna wananchi wake wasitende dhambi, wanawake hawatakiwi kukatiza maeneo ya misikiti siku za ibada, mara ukivaa hivi utamtamanisha mwanaume. Ila ndo wanaongoza kwa kusaliti ndoa zao. Golf club kule wateja wao ndo hao hao wanaotoa matangazo ya midoli huku. Kwanini msiachane na huu unafki ndugu zetu? Ishini tu kama sisi. Hakuna anaetaka kujiita msafi utaenda kujuana na Mungu wako huko.

Na tunakoelekea znz inaenda kuwa kama iran. Yaani mnaamka asubuhi sheria ya kunyongwa itapitishwa kama mtu akitenda kosa. Punguzeni unafki
 
Serikali mliiweka wenyewe watawala wavamizi , mnapiga kelele Za kazi gani?
 
Serikali mliiweka wenyewe watawala wavamizi , mnapiga kelele Za kazi gani?
Waliiweka wakina nani? Anaepiga kelele nani? Kwani mi mzanzibari au umechanganya mafaili?

Alafu hizo sheria zingekua zimetungwa dodoma zingefanyika hadi bara. Ila too sad. Unafki unaendeshwa huko huko kwenu visiwani
 
Badala ya kuhangaika na kufeli fomfoo kwa kizazi kijacho, wako bize na vitu visivyo na tija.
Stars ndio kitu gani? Hayo magauni Yao yanayo ficha uso yamewafikisha wapi?
 
Back
Top Bottom