Zeddicus Zu'l Zorander
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 804
- 951
Daaahh ila inaonekana wanachi wa Zanzibar wako delicate sana ndio serikali inajitahidi kuwalinda na tamaa mbalimbali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
View attachment 2518430
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Unguja, Rashid Simai Msaraka amepiga marufuku, Wafanyabiashara wa Wilaya hiyo kuweka midoli yenye nguo zisizo za staha nje ya maduka yao.
DC Msaraka ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Mfanyabiashara maeneo ya Kwahani Zanzibar akiwa ameweka midoli hiyo nje ya duka ikiwa imevalishwa nguo ambazo zinadaiwa kupotosha maadili ya Zanzibar hususan kwa Watoto pindi wanapoona midoli hiyo imevishwa nguo hizo
DC Msaraka ameiambia AyoTV kuwa maarufuku hiyo imetokana na Watoto na Vijana kuona vitu visivyo na staha na kupelekea kuvuraga akili za Vijana wa Zanzibar Hatuwakatazi kuwa na midoli hiyo wala hatuwakatazi kufanya biashara hizo ila biashara hizo zifanywe ndani na zisiwekwe nje, Mtu anayetaka kuvaa nguo hizo avae
mwenyewe anajua utaratibu gani wa kuzivaa na wapi azivae"
Chanzo: Millard Ayo
Pia soma
- Hii midoli ya fasheni kwenye maduka inayovalishwa nguo za ndani inavunja maadili
Watakuwa Nani serikali aliyoiweka Mvamizi kutoka Dodoma?Hawa jamaa wenye vichwa flat miaka siyo mingi watakuwa kama Al shabaab, au Boko haram! Maana wako dunia tofauti kabisa na sisi. Yaani midoli tu, wanapagawa!
Serikali mliiweka wenyewe watawala wavamizi , mnapiga kelele Za kazi gani?Yaani hili taifa lina vituko🤣 linafanya kila namna wananchi wake wasitende dhambi, wanawake hawatakiwi kukatiza maeneo ya misikiti siku za ibada, mara ukivaa hivi utamtamanisha mwanaume. Ila ndo wanaongoza kwa kusaliti ndoa zao. Golf club kule wateja wao ndo hao hao wanaotoa matangazo ya midoli huku. Kwanini msiachane na huu unafki ndugu zetu? Ishini tu kama sisi. Hakuna anaetaka kujiita msafi utaenda kujuana na Mungu wako huko.
Na tunakoelekea znz inaenda kuwa kama iran. Yaani mnaamka asubuhi sheria ya kunyongwa itapitishwa kama mtu akitenda kosa. Punguzeni unafki
Mumeleta majeshi mkauwa watu ili kuiweka Serikali ya vibaraka wenu , mnapiga kelele Za nini?Daaahh ila inaonekana wanachi wa Zanzibar wako delicate sana ndio serikali inajitahidi kuwalinda na tamaa mbalimbali
Waliiweka wakina nani? Anaepiga kelele nani? Kwani mi mzanzibari au umechanganya mafaili?Serikali mliiweka wenyewe watawala wavamizi , mnapiga kelele Za kazi gani?
Imewekwa na majeshi ya Uvamizi kutoka Dodoma. Anayepiga kelele mTanganyikaWaliiweka wakina nani? Anaepiga kelele nani? Kwani mi mzanzibari au umechanganya mafaili?
Kwahiyo wa dodoma wakaweke sheria kwenye nchi ambayo hawakai iwasaidie nini? Mbona kkoo midoli iko uchi kutwa hakuna sheria za kijingaImewekwa na majeshi ya Uvamizi kutoka Dodoma. Anayepiga kelele mTanganyika
Anzisheni mchakato wa kujitawala kwa 100%, na hivyo kuwa na nchi yenu kamili.Watakuwa Nani serikali aliyoiweka Mvamizi kutoka Dodoma?
Waambie Hao vibaraka mliowaweka kwa kutoa roho za watuKwahiyo wa dodoma wakaweke sheria kwenye nchi ambayo hawakai iwasaidie nini? Mbona kkoo midoli iko uchi kutwa hakuna sheria za kijinga