Dunia inakwenda kasi sana. Kuna baadhi ya mambo yapo katika vitabu vya dini lakini wakati unakataa hivyo watu wanaishi kadri leo inavyotaka. MfanoBora wakatae kabisa, kwanza ukipata dharura na ukatakiwa kujifungua kwa upasuaji na ukakosa 150k basi upo hatarini kupoteza uhai wa Mama na Mtoto kama ilivyotokea mara 2 miezi kadhaa nyuma kanda ya ziwa na Tanga .
Utaratibu wa Wanaume kuingia Leba si katika tamaduni za Kiislam
Hilo la wanaume kuingia leba,ilikua wakati huo ila kwa sasa watu watalipuuza tu.
Mwanamke kuwa kiongozi, ilikua wakati ule ila kwa sasa watu wanapuuzia tu.
Unywaji wa pombe, kwa msisitizo sana imani inakataa leo watu kibao haijalishi imani zao wanapiga kilevi kama kawaida.
Uasherati, uzinzi n.k
Mwanadamu kwa sasa anakemea sana dhambi anayoona anaimudu kuikwepa asiyoimudu anaikaushia.
Jambo la msingi simamia imani yako wewe kama wewe,mengine achana nayo utaumiza kichwa bure.
Dunia kwa sasa ni mwingiliano wa watu hivyo hakuna cha mila,desturi wala tamaduni.