Wewe ni duni sana katika kila kitu. Maana unaamini kubadilisha muda wa kula ndiyo kufunga.
Yesu alifunga usiku na mchana kwa siku 40, akijaribiwa na ibilisi. Yesu hakuwa na sababu ya kufunga bali aliyoyatenda ilikuwa ni mpango wa Mungu Baba kutaka kutuonesha sisi wanadamu tunavyotakiwa kuenenda kwa kadiri ya mpango wa Mungu. Yesu alipofunga, hakuna siku alienda kuwachapa watu barabarani eti kwa sababu hawajafunga. Na katika kufunga kwake, lililokuwa kubwa siyo kutokula bali ilikuwa kumshinda shetani, yaani kuishinda dhambi. Sasa wewe huli mchana, usiku mzima unafakamia chakula, tena unakula kuliko wanaokula mchana, unatoka na chuki tele kwa wanadamu wenzako, umefunga nini mnafiki wewe?
Wanaofanya hivyo ndio hao ambao Yesu aliwaona toka nyakati hizo pale aliposema, msiwe kama wale wanafiki, ambao wakifunga, wanakunja sura zao, wakitaka watu wote wajue kuwa wamefunga. Hakika hao hawana thawabu yoyote maana sifa wanayoitafuta wamekwishaipata. Ila ninyi mfungapo, jipakeni mafuta, tabasamuni ili watu wasijue kama mmefunga bali Baba yenu wa Mbinguni".
Wakristo wa kweli hawafungi kwa maonesho kama baadhi yenu mnavyofanya. Huwezi kujua nani amefunga na nani hajafunga.
Endeleeni kubadilisha ratiba ya kula ili kutafuta sifa kwa wanadamu.