Zanzibar one first ferry vs Azam marine

Zanzibar one first ferry vs Azam marine

Ambition plus

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2018
Posts
6,101
Reaction score
11,381
Habari za mida hii..?Pole na janga la corona.Tuombe mola wote atunusuru kwa sote..

Niende kwenye mada husika.Wakazi wa Zanzibar na Tanganyika tumekua tukitumia boti za Azam na flying horse.Biashara bila ushindani sio biashara..
Flying horse imekua haina ushindani sababu sio boti ya uhakika.Spear mkononi safar ya masaa mawili inaweza ikasafiri masaa manne au hata sita.

Je do we have another choice??Hakuna ni azam marine tu.Je vipi huduma zake?

Azam marine haijawai kua na huduma bora kwa classes zote.Ukiwa unataka ticket ya haraka lazima ulanguliwe kukiwa na madalali kila kona ticket ya 25k utapata kuanzia 35k lakin kwenye ticket wamechapa 25k..#shame

Kwenye mtandao unaona ticket zipo ila dirishani wanakwambia amna na hata ukiwaonyesha hawakubali kukupa ticket..

Unaweza fika pale ofisini kwao kukata ticket muudu asikuangalie wala asikusemeshe mpaka una maliza huduma yako ya kukata ticket (customer care mbovu kabisa)Anakinga tu mkono kibububu apokee pesa na kitambulisho..

Sasa umekwama sehemu jaribu kuuliza wanakujibu kama hawataki.Biashara bila mshindani sio biashara..

Boti ya Zanzibar one imeleta ushindani.Wana customer care nzuri kabisa kuanzia office zao mpaka kwenye boti (sijui labda ni mwanzo tu).Boti ni nzuri na yakisasa kuzidi azam..

Azam akae vizuri ajirekebishe anapokosea mana karundika waraabu wenzie wanafanya kazi ki mwinyi na tumeshalalamika sana tumekua tukipuuzwa..

Raha ya biashara kuwe na ushindani.Na sasa tuna chaguzi ingine...
1585286777772.png


Sent using Jamii Forums mobile app
 
nguvu ya Soda iyo, muulize Abood alipotaka kum challenge Azam kwa maji

uyo new comer hana mda, atachezea vitasa kama wenzie akina Burak, Sepidei, Sea Gull
Ooh ho sijasoma mbinu hizi Havard business school😎
 
Zanzibar one wamerudi tena kipindi cha nyuma walikuwa wana boti zao Sea Star.
Walimkimbiza Sana Azam mpaka fitna za kibiashara zikatumika kuwatoa mchezoni.

Hizo Sea Star zilikuwa zina balaa ilikuwa ikitoka bandarini hao Azam hata kama wametoka muda mchache lazima waachwe gepu kubwa mpaka kuwahi kufika bandarini.
 
Back
Top Bottom