:behindsofa: Hakika sijui nini kiko nyuma ya haya mauwaji ya watumishi wa Mungu hasa kwa Kanisa Katoliki. Hakika kama hao nao ni wana wa Mungu basi kuna kila sababu ya kuamini ya kuwa kweli kila mtu/watu wana Mungu wao, maana haingii akilini wengine Mungu anawaelekeza kutenda mema ili kumpendeza Mungu aliyetuumba na wakati huo huo wengine kwa njia ya Mungu wao anawaambia watende mabaya tena mauaji, kutoa roho kiumbe wa mwenyezi Mungu. Hakika hao wana Mungu wao tofauti na huyu Mungu wa amani . Inatia simanzi sana, lakini maadamu imeandikwa "Kila nafsi itaonja mauti" basi kwa wenye imani kama yangu tuendelee kumwombea huyu mtumishi wa Mungu Padre Mushi ili Mwenyezi ampokee na ampumzishe kwa amani mahali pema peponi. Amina.
Nina imani alitimiza wajibu wake hapa duniani na hata mauti yanamkuta alikuwa njiani kuelekea kuendeleza wito wake wa hapa duniani, jiulize mwana jf mwenzangu mimi na wewe vipi?. Hakika ni changamoto kwetu sisi watanzania kwa ujumla wetu na viongozi wa serikali walio apa kuilinda amani ya Tanzania na watu wake kupitia vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama, ambavyo kila siku iendayo kwa Mungu tunatozwa kodi za haki na zisizo za haki ili kuviwezesha kufanya kazi kwa masilahi ya umma wa watanzania.
Eee Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, bwana wa viumbe wote, uliye asili ya mema yote tunakuomba kwa unyenyekevu mkuu ushushe roho wako mtakatifu juu ya mioyo ya Watanzania hawa hasa hawa wenye kujaa roho ya mauaji ili waweze kukurudia wewe na amani yako ipate kutawala daima kama yalivyo mapenzi yako. Amina