Zanzibar: Padri auawa kwa kupigwa Risasi!

Zanzibar: Padri auawa kwa kupigwa Risasi!

Status
Not open for further replies.
Babu na bibi zetu walikuwa na imani zao. Waliishi nazo karne kwa karne mpaka tulipoletewa dini hizi za kuja. Kuna matatizo gani kwenye imani zao kiasi cha sisi kuzisahau kabisa?

Kuna dini nyingi sana hapa duniani zikitumia njia mbalimbali kuabudu. Dini zote hizi zinaabudu MUNGU. Nchi za Asia zinaongoza kwa kuendelea kuabudu imani zao za asili na kutokubali kuacha imani zao hizo kufuata imani za kuja. Wanaishi vizuri tu na Mungu anawabariki kwa kuwa mataifa ambayo yako njiani kuongoza dunia nzima kwenye kila nyanja ya maisha – Uchumi, Ulinzi, Sayansi, n.k.

Jambo la kusikitisha kwetu ni kwamba vijana wetu hawakupewa hata nafasi ya kuchungulia imani zetu zilikuwaje ili waweze kufanya tathmini na kuona kama wanahitaji kukumbatia dini hizi za kuja au warudi kwenye mizizi ya mababu na bibi zao. Historia yote ya dini hizi za mababu zetu imefutika na hakuna hata juhudi ya kuikusanya na kuihifadhi angalau kama historia ili vijana wetu waweze kuipitia na kufanya maamuzi yao. Hata mashuleni kwetu hakuna hata mitaala inayowafundisha vijana wetu imani zetu. Kwa nini tuone haya kuamini kwenye vitu ambavyo mababu na mabibi zetu waliviamini?

Sasa tunaburutwa na dini hizi za kuja na kwa kweli ninapopitia thread hii najisikia vibaya sana kiasi nashindwa kuzuia machozi kutirika jinsi ambavyo tumeanza kuchukiana na kunyoosheana vidole kwa dini hizi za kuja ambazo zililetwa kwetu si kwa ajili ya kusambaza dini zao bali kama chombo chao cha kuweza kutupotezea lengo ili watuibie na kutunyanyasa na kutufanya watumwa.

Naona humu watu wanaapizana kwamba wao kuanzia sasa ni maadui!!!! Tumefika hapa kweli ndugu zangu Watanzania? Wote tutakaokubali kufa kwa ajili ya kuzitetea dini hizi za kuja tutaishia motoni.
Tuanze sasa juhudi za kujitambua kwa kurejea na kupitia imani za Wazee wetu na kuacha kuburuzwa na imani hizi za kuja kwani Wazee wetu (R.I.P) nao walikuwa wakimwamini Mungu kama wengine.
Wanahistoria wa Tanzania tafadhali tutendeeni haki kwa kutafuta habari za dini za mababu na mabibi zetu ili tuweze kuzihifadhi na kuzitumia. Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kuzitumia.

Mwisho nawaomba Watanzania wenzangu tuepuke kuburuzwa na hisia za dini hizi za kuja kiasi cha kufika kuchukiana na kuuana wenyewe kwa wenyewe. Tuelewe kwamba Taifa letu ni masikini mno kuweza kupoteza Watanzania wenzetu wanaohitajika kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu kwa kuuwana wenyewe kwa wenyewe kama vile sisi ni MATAAHIRA.

Tutumie nguvu zetu kutafuta suluhu ya matatizo yetu kama Taifa ili tuweze kuwa na Taifa lenye neema.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA
 
Huu ni mpango mahsusi umepangwa ili Wazanzibari waonekane wakorofi na madai yao kuhusu Muungano yaonekane yana lengo baya! Mapadri Munawapiga wenyewe na sisi Wazanzibari kwa matukio kama haya wala hatupati tabu tena
 
Watu wengine wanataka tufungiwe humu jf unawezaje kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu umeambiwa vipeperushi vilitembea baada ya padre wa kwanza kupigwa risasi kwamba bado mapambano yanaendelea,ww huna uzalendo na huenda unavaa suruali fupi.

Unaweza kutupia hapa jf vipeperushi hivyo
 
sbb nyng 2. nakupa moja. yesu ni mjumbe wa m'mungu
kitoabu acha unafiki na
uwongo. kama ingekuwa mnamshitakia mungu mnapohisi kuzulumiwa haya ya
leo yasingetokea. mbona jana mliandamana juu ya shekh wenu ponda?
mkaanzisha vurugu pale watoto walipobishana na kufikia hatua ya mmoja
wao ambaye ni mkristo kuhakiki ukweli ule kwa kufnya experiment ya
kukojolea quraan? mmepandikizwa roho mbaya za kuuchukia ukristo bila
kupewa sababu ya kufanya hivyo. angalieni siku zinahesabika.
 
Kuna haja ya serikali kutafakari masuala ya kidini kwa undani sio kuwa na majibu ya juu juu.kwani madhara yake yanakujaja kidogokidogo lakini yanauma
 
Raisi muislam, IGP muislam,mkurugenz usalama muislam, jaji mkuu muislam, makamu wa raisi muislam, raisi wa Zanzibar na baraza lake lote waislam! Usitegemee wakristo kutendewa haki hapo!
 
suluhu itapatikana vp wkt mnajua maskin wanajua kuna kundi linafaidi mali za nchi? acheni ujinga
Babu na bibi zetu
walikuwa na imani zao. Waliishi nazo karne kwa karne mpaka tulipoletewa
dini hizi za kuja. Kuna matatizo gani kwenye imani zao kiasi cha sisi
kuzisahau kabisa?

Kuna dini nyingi sana hapa duniani zikitumia njia mbalimbali kuabudu.
Dini zote hizi zinaabudu MUNGU. Nchi za Asia zinaongoza kwa kuendelea
kuabudu imani zao za asili na kutokubali kuacha imani zao hizo kufuata
imani za kuja. Wanaishi vizuri tu na Mungu anawabariki kwa kuwa mataifa
ambayo yako njiani kuongoza dunia nzima kwenye kila nyanja ya maisha –
Uchumi, Ulinzi, Sayansi, n.k.

Jambo la kusikitisha kwetu ni kwamba vijana wetu hawakupewa hata nafasi
ya kuchungulia imani zetu zilikuwaje ili waweze kufanya tathmini na
kuona kama wanahitaji kukumbatia dini hizi za kuja au warudi kwenye
mizizi ya mababu na bibi zao. Historia yote ya dini hizi za mababu zetu
imefutika na hakuna hata juhudi ya kuikusanya na kuihifadhi angalau kama
historia ili vijana wetu waweze kuipitia na kufanya maamuzi yao. Hata
mashuleni kwetu hakuna hata mitaala inayowafundisha vijana wetu imani
zetu. Kwa nini tuone haya kuamini kwenye vitu ambavyo mababu na mabibi
zetu waliviamini?

Sasa tunaburutwa na dini hizi za kuja na kwa kweli ninapopitia thread
hii najisikia vibaya sana kiasi nashindwa kuzuia machozi kutirika jinsi
ambavyo tumeanza kuchukiana na kunyoosheana vidole kwa dini hizi za kuja
ambazo zililetwa kwetu si kwa ajili ya kusambaza dini zao bali kama
chombo chao cha kuweza kutupotezea lengo ili watuibie na kutunyanyasa na
kutufanya watumwa.

Naona humu watu wanaapizana kwamba wao kuanzia sasa ni maadui!!!!
Tumefika hapa kweli ndugu zangu Watanzania? Wote tutakaokubali kufa kwa
ajili ya kuzitetea dini hizi za kuja tutaishia motoni.
Tuanze sasa juhudi za kujitambua kwa kurejea na kupitia imani za Wazee
wetu na kuacha kuburuzwa na imani hizi za kuja kwani Wazee wetu (R.I.P)
nao walikuwa wakimwamini Mungu kama wengine.
Wanahistoria wa Tanzania tafadhali tutendeeni haki kwa kutafuta habari
za dini za mababu na mabibi zetu ili tuweze kuzihifadhi na kuzitumia.
Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kuzitumia.

Mwisho nawaomba Watanzania wenzangu tuepuke kuburuzwa na hisia za dini
hizi za kuja kiasi cha kufika kuchukiana na kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Tuelewe kwamba Taifa letu ni masikini mno kuweza kupoteza Watanzania
wenzetu wanaohitajika kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu kwa kuuwana
wenyewe kwa wenyewe kama vile sisi ni MATAAHIRA.

Tutumie nguvu zetu kutafuta suluhu ya matatizo yetu kama Taifa ili
tuweze kuwa na Taifa lenye neema.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA
 
Nafikili tuliachie jeshi letu la polisi lifanye kazi yake na hapo ndipo tuanze kulaumu !
 
Usalama wa Taifa, Kazi yenu ni kutoa taarifa Za kiintelijensia Za CDM tu via maandamano plus vikao vyao Na kuacha kuwasaka, kuwabaini Na kuwatolea taarifa hizo za kiitelijensia wapuuzi wenye silaha Na mipango ya kuvuruga Amani ya Nchi Kwa kuwaua VIONGOZI Wa DINI????
 
Wakuu

Leo sina maneno mengi zaidi ya kuitaka serikali ichukue hatua za haraka na za dhati kuhakikisha wale wote ambao wamehusika na matukio yafuatayo wanakamatwa, wanafunguliwa kesi na kuhukumiwa adhabu(hata iwe ya kifo)

1.Waliohusika na mauaji ya Mchungaji kule Geita

2.Waliohusika na Mauaji ya Padri Mushi kule Zanzibar

Maandikio yapo wazi kuhusu kumwagika kwa damu ; Jambo hili linaruhusu Laana kutokea na nisingependa laana hii itokee na kuliathiri taifa zima.

Rais Kikwete, Rais Shein naomba mchukue Hatua na kama mnaona hamwezi kusema Hapana na masuala haya basi mnaweza kukubali kuachia wengine waongoze. Muda mnao na hili linahitaji hekima za kiuongozi

Hili suala si la waislamu wala wakristo kwa kuwa hakuna dini inayorudhusu kuua watu wasio na hatia. Qur’an Tukufu inasema: "…atakayemwua mtu bila ya yeye kuua mtu, au bila ya kufanya ufisadi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote …" (Al Maidah 5:32). Uislamu unawaona wanadamu wote ni kama ndugu wa familia moja. Kwa hivyo kumfanyia ukatili mmoja wao ni sawa na kuwafanyia ukatili wote.
 
Nasikitika kuwa Padre ameuawa leo asubuhi, ili sio jambo zuri kabisa na si ishara nzuri kwa nchi yetu iliyokuwa na amani kiasi cha kuwa mfano ulimwenguni.

Lakini pamoja na hayo siamini kama kundi la Waislam wasioijua dini yao na kuitumia kwa masirahi binafsi wakiua mkiristo basi waislam wote wamekosa, leo waislam wametukanwa sana hapa tena na watu ambao wana heshima zao kabisa tunawaona kama mifano ndani ya JF, sasa nauliza swali moja na mimi ambaye mama yangu ni mkiristo na mke wangu ni kiristo na mimi niwatukane wakristo si nitakuwa nimemtukana mama yangu na mke wangu! Ni kweli mwelekeo wa nchi hii sio mzuri kabisa kwani tumeacha misingi yetu tuliyoijenga na kuanza kushabikia mambo ya kisiasa.

Kama great thinkers (GT) hatutakikiwi kuwa na jaziba tuliyoionyesha leo, tunatakiwa kusimama sasa na kuiambia serikali huu ni upuuzi hatutaki kuuona tena, hatutaki kuishi kwa wasiwasi tunataka kuishi kwa amani na upendo kama ilivyokuwa mwanzo, serikali lazima iwatafute wauaji na wanaochochea dini ambao kwa sasa sio waislam tu ni pamoja na makanisa mengi tu, kazi zao ni kuchochea vurugu kwa kuwa wananufaika na vurugu hizo

Great thinkers (GT) think twice tuache ujinga tuliouonyesha leo na kusimama imara kwani fikiri leo mke wangu mkristo mimi muislam tuchinjane wenyewe kwa wenyewe watoto wangu wanabaki na nani? jirani zangu ni mchanganyiko wakristo na waislam, leo tunaanza kuacha kusalimiana inakuwaje?

TUIKEMEE SERIKALI NA KUIAGIZA KUWA LAZIMA WAWATAFUTE WAUAJI NA KUWAWAJIBISHA VINGINEVYO SISI TUWE TAYARI KUINGIA MITAANI KWA KIGEZO CHA KUIWAJIBISHA SERIKALI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA ULINZI WA WATU WAKE, TUSIKUBALI HATA KIDOGO KUKAA CHINI NA KUONA RAIA WASIO NA HATIA WANAKUFA NA SERIKALI HAICHUKUI HATUA KWA KIGEZO CHOCHOTE KILE
 
Mungu ampe pumziko la amani,na wahusika watafutwe na kukamatwa na kupelekwa mbele ya sheria

Mkuu, hakika inasikitisha sana.
Lakini ni kitu kinachochochewa na viongozi wa nchi na serikali.

Hebu mkuu fikiria picha au dhana hii;
Ni tarehe 25/12/....., Kiongozi mkuu wa nchi (rais) anakagua gwaride la heshima la majeshi ya ulinzi na usalama lililoandaliwa mahsusi kuadhimisha sikukuu ya Krismasi (kuzaliwa Yesu Kristo)!
Hivi si, wakristo wote wa nchi hiyo wataamini na kuona kwamba nchi na serikali yao ni ya dini ya Kikristo na wote waliomo watatakiwa kuwa wakristo vinginevyo waondoke!

Haya ndiyo yaliyotokea Zanzibar, ambako haikuwa picha wala dhana bali ni uhalisia wa Rais wa serikali tukufu ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar alipoadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume SAW kwa kufanikisha dhana niliyoieleza hapo juu.

Kwa mantiki hiyo wakristo hawatakiwi na hawatatakiwa Zbr, na serikali iliitia nguvu hoja hiyo kwa tukio lile.

RIP, father Evarist Mushi. Waliokuua wamekupunguzia mateso ya hapa duniani na kukuwahishia kuuona utukufu wa Mwenyezi Mungu mbinguni, uliyemtumikia kwa moyo wako wote hata kuutoa uhai wako kwa ajili ya kazi zake, Amen.
 
this is too much, nadhani tatizo la msingi ni upeo mdogo na ukosefu wa elimu dunia, hailet maana eti kumuua mtu aso wa dini yako utapata thawabu.huyo Mungu wa mauaji ni wa wapi?? something has to be done very quickly
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom