Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

A

Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

ALISEMA HIVYO KUONESHA SI UUNGWANA ALICHO KIFANYA MAALIM.....SIASA HAIENDI HIVYO.............
 
Kwa upeo wangu mdogo wa mambo ya siasa, natambua kuwa Katibu Mkuu wa CUF, ana hadhi yake ya kikatiba baada ya kushikilia wadhifa mkubwa sana katika serikali iliyopita ya Zanzibar.

Hivyo basi kama kiongozi mwingine yeyote mkubwa wa nchi au taifa huru ana stahiki zake. Matibabu, makazi, sina hakika sana na ulinzi japo yafaa iwe ktk stahiki zake.

Alipokataa kumpa mkono Rais wa sasa wa Zanzibar, ilikuwa ni utashi binafsi pengine inatokana na tofauti zao na mkanganyiko uliosababisha kuwepo kwa serikali ya sasa ya visiwani. Ana sababu zake, anaelewa madhumuni ya kufanya vile.

Kwa kitendo kile, sidhani kama anakuwa amevunja katiba wala kustahili kunyimwa stahiki zake za kikatiba. Matibabu ni stahiki kubwa sana na ni haki yake.

Nilistaajabu sana, kusikia mkuu wa kaya anasema anamshangaa Rais mwenzake wa visiwani kusaini karatasi zile.

Jamani hivi iko wapi nguvu ya sheria ambazo kwazo viongozi wetu wanaapa?

Masikini nchi yangu. Tutayaona na kuyasikia mengi
 
Hekima za kiongoz huonekana kwa wafuasi wenye hekima, wasio na hekima kila kitu kwao ni kifungo, na mpuuzi akiongozwa kwa hekima ni huduwaa. Hatua za magufuli zimepita ufaham wenu ndo mmekosa ajenda sasa mnahaha kutega wapi atajisahau mdandie! Watu wengine familia yake inadumaa afu anaota kupaisha nchi tena anajiita kijana msomi. Achati kuota, ndoto huota wazee, vijana huona maono!
 
Jamani mimi hata siandiki kitu..nikiandika kesho nitasimama kizimbani kwa kosa la uchochezi kama siyo uhaini..
 
Ndio kitu pekee ulichokiona cha muhimu alichosema Rais hicho??
Mkuu usijifanye kufumbia macho jambo kubwa kama hilo..rais wa nchi unapandikiza chuki kwa wananchi..sijawahi ona au hata kusikia. Tena kwa msisitizo kabisa anarudia na hata kumshawishi Dr shen..mzee mwenye hekima na busara...tusiwashangae wakuu wa wilaya wanapotoa maagizo na matamashi ya hovyo...
 
Angalau umemwelewesha vyema huyu aliyeamua kujitoa fahamu. Jambo la mustakabali na maslahi mapana ya nchi ni la muhimu na kipekee kabisa. Mtu yeyote yule awaye akichezea au kuonyesha kuyumbisha hali hii lazima akemewe vikali sana
 
Kiuhalisia Magufuli yuko sahihi kwa asilimia 100%.
Kwa kweli mtu aliekataa kupokea mkono basi huyo sina time naye.
Shein alisain kwa sababu ya katiba ni kiuhalisia ni lazima atii katiba.
Najua ingekua ni kesi ya magufuli asinge sain sasa hapa ndio naona shida kwa sababu katiba inamlazimu asaini.

Potelea mbali nampa mtu mkono anakataa halaf niendelee kuwa nae karib nasema siwez kumsalimia.
Watanzania wengi ni wanafiki sana hawasimami kwenye ukweli ndo maana naona wengi mnatoa povu sana.
Na pia nimejifunza sio kila anaekusalimia anakupenda wengine ni wanafiki tuu kama nyie wote mnaomsema magufuli hapa.
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

hivi magufuli anasoma au ameshawahi kusoma katiba ya nji hii
 
Hata mimi nisinge saini.[/QUOTE hana jeuri hiyo
mambo ya hivyo yanafanyika nyumbani kwako na familia yako hii ni nji inaendeshwa kikatiba atake asitake atasain unless ingekuwa ni talaka ama kishika uchumba cha bintiye ndo angeweza kukataa acheni chuki

na huyo/hao wazee wawili wanajua wako hapo kwa njia gani ndo maana wana kauli za ajabuajabu..................
 
Lowasa ni muungwana by nature
mnafiki tuu huyu na janjajanja nyingi. tungejilaumu sana tungempa madaraka huyu mtu.
ila watu vilaza kama nyie msiokuwa na maono ya mbali bado mnamsifia lowasa mtu ambae mlikua mnamuita fisadi. shame on you.
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

Me nahis jamaa huwa mwepesi kuongea vitu..kwa haraka bila kuvitafakari kwanza!!
..Me napita tu na hisia zangu ila km kuna mkubwa km Mungu anihukumu...
 
Hakika tuna matatizo hasa. kwa nini wote tunaanza kutolea macho mambo mepesi kama haya? Tunalisaidiaje taifa kupitia haya? wananchi wananufaika na nini kupitia haya?
unaweza kurudi kazini umechoka halafu unauliza chakula unanyooshewa kidole na mwenzio tena cha mguu... " hukioni hapoo?" hebu tujadili huu uchumi na maisha kwanza!
kwa sasa watawala hawatakiwi kukosolewa kwa nini? kila kitu kiko sawa!
 
NA MAPENZI PIA
 
Back
Top Bottom