Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

unashangazwa na aliesema naneno tu wala sio matendo mimi nilitalajia ushangazwe na maalim sefu muumini wa dini ya kiislam kukataa mkono wa umuumini mwenzie kwa swala dogo tu cheo huku akijua wazi kwamba ktk kupeana mikono kuna kusemehewa mazambi yao na kupotea chuki baina yao hatimae yaweza kuwa sababu ya mafikio mema
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

Kamgunga kama unataka kushangaa nenda Feli. Haki uombwa na mwenye haki, kwa mikono misafi. Huombwa kwa mamlaka inayohusika. Maalim mikono yake inanuka damu ataombaje haki kwa mtu baki asiyemkubali kama ni Rais?
 
Laiti tungejua athari za maneno yetu! Laiti Mungu Angetupa hata punje ya haradali tu, haya maneno yetu yakitoka yanaumiza sana sana, hayajengi yanachochea moto, moto ukiwaka kwenye nyumba zetu hizi tutaungua wote, hata yeye Yohane asidhani kama atabaki salama
 
Mbona viongozi wetu wanachuki namna hii hivi huyo Mungu wanayemuomba kila siku ni huyuhuyu Mungu ambaye tunamuomba makanisani na misikitini au wao wanamwingine,kama ni huyu wa makanisani na misikitini basi tunatwanga maji kwenye kinu Mungu anakufuliwa matokeo yake ni laana ktk nchi yetu
 
NIMEIPENDA HII. ...NIMECHEKA SANA..ENDELEA KUNG'ARA MH. RAIS WA NCHI YETU TANZANIA. ...UBARIKIWE SANA SANA. ...
 
Inasikitisha...
Maneno yaliyosemwa leo huko zanzibar ni ya kuongeza chuki na fitina juu ya wazanzibar ili wakose umoja watawaliwe milele...

Kusalimiana kwa kupeana mkono si lazima...ni sheria ipi inasema lazma umpe mkono rais wakati mkisalimiana?
Sitahiki za malim seif na viongiz wote wa juu zipo kisheria na wahusika wanatakiwa kusaini kwa kuwa ni wajibu wao ..mafao yao ni sheria imewapa siyo kwa hisani ya mh rais...

Ishu ya malim kutotoa mkono ni very personal haina uhusiano na kazi...

Hivi ni ujumbe gani anapeleka kwa wafanyakazi wa umma? Kwamba saiv ukikosana na mtu kwenye mambo ya kijamii basi tuhsmishie na kazini...mfano mkipishana na kauli na hakimu msibani basi siku ukiwa mahakamani asikutendee haki..
Ukihitilafiana na daktari mtaani basi daktari akunyime huduma siku ukizidiwa hospitalini...

This forest is not for any monkey
Wagawe uwatawale ndio anachofanya. Anataka mafuta ya Zanzibar haraka lazima awakunekune watu fulani ili wamruhusu kirahisi.
 
kwa kweli kuna haja ya kuongeza kipengele cha viongozi kupimwa afya ya mwili na ubongo kabla ya kuchukua fomu kugombea nafasi nyeti kama urais.
 
NIMEIPENDA HII. ...NIMECHEKA SANA..ENDELEA KUNG'ARA MH. RAIS WA NCHI YETU TANZANIA. ...UBARIKIWE SANA SANA. ...
haa haa kweli kila mtu na mawazo yake huyo mungu wa kutoa baraka kwa mtu anayepalilia chuki na visasi ni mungu yupi?
 
Naanza kumkumbuka marehemu Chiluba jinsi alivyoingia madarakani na kudharau waliomtangulia kama Mzee Kaunda. Kilichotokea ni kuwa baada ya yeye kuondoka madarakani aliyoyafanya kwa mwenzie yakajirudi kwake na alikaa sana "Segerea" ya Zambia na hakuna aliyemuunga mkono tena akajihisi upweke sana na ndio uliochangia safari yake ya peponi au jehanamu mapema. Madaraka ni dhamana unayoipata miongoni mwa wengi sio ujanja wako, hebu muoneni JK jinsi alivyoishi kwa kauli za hekima kiasi kuwa hata kama kamuumiza mtu bado unamuona binadamu.
Faiza Foxy aliyasema haya tukamdharau
 
Makes wanna puke, it makes me sick to the core...!! This guy he thinks he is god, does he even know kuna katiba ya nchi... Yaani unajiapiza kabisa hakanyagi mpinzani kwenye serikali yake.... Mbona mbaguz na wa waziwazi huyu...
Shein anamlisha Maalim kwa hisani au ni haki yake ki katiba??
 
Najiuliza tu. Mbona kama Mh Rais anaongea kwa kutisha sana?!

Kila akipata jukwaa la kuzungumza lazima 'taharuki fulani' hivi itokee. Currently aliwaambia wafanyabiashara waweke pesa kwenye mzunguko la sivyo atabadilisha pesa.

Kwenye historia ya ubadilishaji wa pesa nchi hii sijawahi kumsikia aliyesema anabadilisha pesa kwa ajili ya ku dili na wafanyabiashara ambao hawaweki pesa kwenye mzunguko.

Siku zote nia imekuwa ni kuboresha uchumi. Sasa siku Mh Rais akibadilisha pesa tafsiri ni kuwa anadili na wafanyabiashara wasioweka pesa kwenye mzunguko.

In fact mazingira rafiki ya biashara ndio yanayowashawishi wafanyabiashara kuingiza pesa kwenye mzunguko na sio tishio la kubadili pesa.

Na majuzi ZNZ nako ndo hvyo.

Ni kama vile Mh Rais akiongea taifa lina taharuki, lakini akikaa kimya Taifa linakuwa poooooaaaaa kabisa tunaendelea na mishe zetu.
 
Back
Top Bottom