TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

Allah ailaze royo yake mahala pema

Turky alikua muungwana sana.

Katika Jimbo lake la Mpendae-Zanzibar, kiuhalisia ni jimbo la UPINZANI.

Mwakilishi kutoka Upinzani, Kura za Uraisi pia upinzani unaongoza kwenye Jimbo lake.

Lakini Nafasi ya Ubunge, Wananchi wanaweka siasa pembeni Turky anasimamishwa kwa Ushindi wa kishindo.

Turky alikua hana ubaguzi wa kisiasa, akitoa misaada anatoa kwa nyumba zotee bila kuangalia itikadi.

Akisaidia wajasiriamali hakuangalii itikadi yako ya Chama wala wapi Unatokea.

Hakika tukipata Viongozi mfano wa Turky tutakuwa mbali mnoo..
 
Kafariki leo usiku ghafla,juzi alikuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni za Ccm Zanzibar.

Tulikuwa nae pamoja msibani Jumapili mwenye afya njema kabisa. I even joked with him, nikamwambia mavazi meupe kayapatia hasa kama kwenye msiba wa kihindi. Akacheka sanaa. Kwa wote wasiomjuwa, alikuwa the nicest guy ever, self depricated, hakujiweka kama muheshimiwa au tajiri. Alipenda kukaa pamoja na watu wa tabaka zote na kupiga nao stories za kijiweni.

The hole you have left with your sudden departure will never be filled up. Loved all and loved by all. Rest in eternal peace brother. Will be dearly missed but your presence will never leave us!
 
"Pengine msaada ume mletea tatizo maan ulimuoko mwiba"
 
Kumbe kwenye kundi la mashetani unaweza pata malaika japo mmja,rest in peace seems ulikuwa una ubinadamu sio Kama mwenyekiti na yule wa bungeni
 
Acha kunywesha watu sumu humu.
 
R.
R.I.P Turky,Mwana CCM aliyekuwa mzalendo,muungwana na mwenye huruma kwa binadamu wenzake bila kujalisha itikadi.
 
By

Pascal Mwakyoma TZA


September 15, 2020


Mgombea Urais kupitia chama Cha CHADEMA Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Njombe katika Viwanja vya National Housing ametoa pole kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Mpendae Salim Turk ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo.

“Wakati nilipopata matatizo, Marehemu Salim Turky alimuendea Mwenyekiti Mbowe akamwambia Mwenyekiti mimi nitatoa dola za Marekani laki moja ili ndege ipatikane mimi nipelekwe Nairobi” Tundu Lissu
 
Huo ndio utu!! Utamaduni wa watz, toka enzi na enzi sio hao washamba ndio wamegeuza siasa kuwa ni uadui!!! Yaani kwa sasa mzungu/mwarabu anaweza kuwa na uchungu na mwana chadema apatapo majanga kuliko mwana ccm?!! Atakavyoguswa!!!
 
Turky alitenda wema mweupe kabisa kutoka moyoni, kukodi ndege kwa ajili ya mtoto wa Mungu aliyepigwa marisasi na wakala wa shetani ili afe. Turky kazi yake imekwisha...
 
Huo ndio utu!! Utamaduni wa watz, toka enzi na enzi sio hao washamba ndio wamegeuza siasa kuwa ni uadui!!! Yaani kwa sasa mzungu/mwarabu anaweza kuwa na uchungu na mwana chadema apatapo majanga kuliko mwana ccm?!! Atakavyoguswa!!!
Chadema wana utu? Tuambie ni jambo gani jema Chadema wameshawahi kulifanya katika nchi hii. Siyo wakati majanga wala chochote kile, salamu za pole tu mwiko kwao. Misiba hawahudhurii, hata misaada tu ya kibinadamu hawana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…