TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

CCM mna roho mbaya sana inawezekana kumsaidia Lisu ndio kimemponza.
Kwa haya yanayoendea unaweza kuwaza haya, WA Kwanza Makonda, Kwa kusababisha risasi zaidi ya tatu kushinda kuua, SASA Mr White Kwa kufanya connection ndege kupatikana haraka. 😔😔😔😔
 
Kama umefika zenji na kama uliona magari plate namba imeandikwa Mr white basi mwenyewe ndiye huyu
R. I. P Mr white

Ova
 
Mwanasiasa mkongwe na mfanyabiashara maarufu Turk wa Zanzibar afariki dunia.

===

Mheshimiwa Salim Hassan Abdullah Turky, afariki dunia usiku huu akiwa hospitali ya Tasakhta global chanzo cha kifo chake inadaiwa kuwa aliugua ghafla. Swala ya maiti itafanyika leo Alasiri September 15 katika msikiti wa Othman Maalim na baada ya hapo atazikwa Fumba, Zanzibar.


Salim Turky alikuwa mfanyabiashara maarufu Zanzibar na mbunge wa jimbo la Mpendae tangu 2010, alizaliwa February 11, 1963. Mpaka anafariki alikuwa mwenyekiti wa makampuni ya Turky ambapo chini yake yalikuwa makampuni 12 yanayoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na visiwa vya Comoro.

Baadhi ya makampuni hayo yanajumuisha hoteli ya Golden Tulip, hospitali kubwa ya Tasakhtaa Zanzibar, pia ilijihusisha na biashara ya cement, Nitak communications, vyakula na mafuta.

Turks Group iliazishwa mwaka 1978 kama duka la nguo na ndugu wa familia moja ambao ni Salim, Murtadha na marehemu Yunus pamoja na baba yao, Hassan Turky na miaka 40 baadae wakalibadilisha kuwa moja ya makampuni yanayoongoza Tanzania.

Mwaka 2017 Lissu aliposhambuliwa kwa risasi, Turky alitafuta ndege iliyompeleka Lissu Nairobi na kuwa mdhamana wa deni la kukodi ndege iliyokuwa inamilikiwa na FlyghtLink ambao ni jamaa zake katika biashara.

Zaidi, soma:

Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Salim Hassan Turky: CHADEMA walilipia gharama za Ndege iliyomsafirisha Lissu

= Taarifa zaidi juu ya kifo hiki kukujia hivi punde =

View attachment 1570123
Rest in paradise Salim Turky
 
R.I.P
Ndg. Salim Hassan Turky (MB).
Wanazanzibar watakukumbuka sana kwa utendaji wako uliotukuka ukiwa kama mtumishi Serikalini.
IMG_1219.JPG
 
Pumzika kwa Amani Mheshimiwa Salim Turky. Wema hawadumu hapa Duniani. Utakumbukwa kwa mengi, zaidi mchango wako kwa Taifa hili.

Utaliliwa na Wanasiasa wote wenye mapenzi mema, kama ilivyo kwa Watanzania wa kawaida waliokufahamu na wengine kukusikia.
Mwenyezi Mungu akupumzishe sehemu salama, Amen.
 
RIP Mr White, ushiriki wako katika kuokoa maisha ya Kamanda Lissu hautasahauliwa. Mola awe nawe.
 
Back
Top Bottom