ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
My Take
Hivi nani Huwa anawadqnganya wanaojiita wasomi kwamba wananchi wanahitaji masoko ya gharama kubwa, ya gorofa na Mabilioni.
Ujinga huu wa kupoteza Rasilimali upo pia kwenye ujenzi wa stendi.
Nyie mnaojiita wasomi badilikeni na muwe na matumizi sahihi ya Kodi za Wananchi.
Soma pia Soko la Ndugai lililojengwa Dodoma kwa mabilioni na kuzinduliwa kwa mbwembwe limetelekezwa na wafanyabiashara
----------------
Takriban mwaka mmoja tangu lifunguliwe soko la kisasa Chuini, Mkoa wa Mjini Magharibi, bado wafanyabiashara katika soko hilo wanalalama kukosa wateja wakidai mitaji yao kufa.
Soko hilo lililogharimu zaidi ya Sh40 bilioni, lilizinduliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi Septemba 20, 2025 lengo ni kusogeza huduma za bidhaa karibu na wananchi na kuongeza vipato vya wafanyabiashara.
Hatua ya kukosa wateja inaelezwa ni kutokana na soko hilo kukosa aina yoyote ya mnada badala yake wananchi hukimbilia katika masoko mengine.
Wakizungumza mbele ya Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdulla alipotembelea soko hilo leo Julai 18, 2026 wamesema bidhaa zao zinaoza kwa sababu ya kutokuwa na wateja wa kutosha.
Fwarda Saidi Ali mmoja wa wajasiriamali wa viungo na bidhaa nyingine amesema licha ya kulipa Sh2,000 kwa siku ambayo ni sawa na Sh60,000kwa mwezi, lakini anadidimia katika biashara kwa kukosa wateja.
Chanzo: Mwananchi_official & The Citizen