Zanzibar: Soko la Bilioni 40 limekosa wapangaji kama lilivyo Soko la Job Ndugai

Zanzibar: Soko la Bilioni 40 limekosa wapangaji kama lilivyo Soko la Job Ndugai

Kuna kitu kidogo TU cha kurekebisha .

Wawaweke wapangaji kwa mfumo wa catalog Yan categories.

Kuwe na upande wa matunda ,nafaka, viungo, mbogamboga, samaki , nyama.

Hii itawasaidia wapangaji kukaa kwa kutulia pasipo , kukimbilia kukaa karibu na mlango ili waonekane na wateja.
Niache kununua huku chini nianze kukisumbua na mangazi?
 
Wananchi wanahitaji masoko na stendi nzuri katika maeneo sahihi, tatizo la chama chako cha CCM kinafikiri ni jambo la maana kwenda kuweka hii miondombinu mbali tena pasipofikika na usafiri wa umma ili watu wateseke kuifuata, na hii ni kwa sababu ya ukosefu wa mipango miji ya muda mrefu kila jambo wanafanya kama zimamoto.
Duuh, kama ya Iringa ile sijui kwanini waliipeleka kule ati
 
Muhimu watu watazoea talatibu tuwape muda👈

Tunakumbuka mwanzo wa mchikichini ilikuwa ivi ivi wateja
hakuna kabisa lkn mwisho mambo yakawa MOTO👈

Faida kujengwa masoko makubwa kwanza yanabeba eneo kubwa
Kwaajili ya matumizi ya Wananchi siku za mbele lkn watu wataenda talatibu 👈
Jinga kweli wewe,watu wataendelea wanapoendaga Kila siku.

Kuna masoko na mastendi ya hovyo kama hayo mengi tuu yamefeli Wala hili sio la kwanza.
 
Jamii inabidi kustaarabika.

Hatuwezi kuendelea kutandaza bidhaa kwenye vumbi kila siku.

Stendi na masoko ya kisasa ni muhimu.
Soko ukishaliweka kisasa kila mtu anakimbia

Ova
 
Ujuaji unawagharimu sana hawa so called wataalamu
Hawa hata wakisafiri nje huwa macho yao kuangalia magorofa tu
Hivyo kudhani hata nyanya zimo humo

Akili ndogo sana na matumizi mabaya ya hela
Soko na gorofa wapi na wapi
 
Hiyo mentality inabidi kubadilika

Hatuwezi kuwa hivyo kila siku.
Jirani kwangu kinondoni bwawani wamejenga soko
La kisasa lakini hakuna watu
Wateja wote wanakimbilia soko la mapinduzi na mtambani,ujenzi wa masoko
Wafanyabiashara hawataki mbwembwe...sasa mtu unamuwekea tiles wakati wafanyabiashara wana mambo yao 😄

Hivyo vitu wanavyoweka inabidi waviupdate viendane na teknolojia ya sasa bila kufanya hivyo watatuchelewesha kwenye maendeleo.
 
Niache kununua huku chini nianze kukisumbua na mangazi?
Unapoenda mlimani City , kila kitu unakikuta chini ?.
Si unavikuta kwenye ma shelf, zimepangwa kwenye catalog, categories.

Tujifunze mbinu za kisasa za kuuza mazao ya kilimo
 
Hivyo vitu wanavyoweka inabidi waviupdate viendane na teknolojia ya sasa bila kufanya hivyo watatuchelewesha kwenye maendeleo.
Upo sahihi,
Private sectors inahusika hapo Sasa kule kwenye minada na shambani , mazao ya kilimo, uvuvi, matunda, nafaka yawe processed kwa ajili ya mtumiaji wa mwisho.

Na sio kuleta magunia ya vitunguu, Kuja kupukuchuliwa sokoni , na soko kugeuka kuwa dampo la uchafu.

Ndogo ndogo tutafika TU
 
watanzania washazoea sehemu chafu chafu penye matusi - kwa ufupi masoko mjinga.
 
Back
Top Bottom