Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Kama ni mwenye hoteli ndo hatari kabisa. Nchi inataka watalii wewe unaanzisha kampeni ambayo itahatarisha uwepo wao nchini? Bora hata awe meneja tutasema alipitiwa.
Shida sio Stika, bali reaction ya Waisraeli yaani kwa sababu huipendi Yanga basi hadi mwenye hotel asiweke stika yake kwa kuipenda Team?

Wao walitakiwa tu kuona Bango halijawafurahisha na pengine hata kubadili Hotel nyingine.....ila kitendo cha kumtafuta kumjua ni nani kinatia mashaka sana.

Kidiplomasia ni kosa kutaka kuingilia Hisia za Watu wengine tena nyumbani kwao.
 
Hayupo sahihi. Hayupo sahihi kabisa. Ni sawa na refa wa mpira shabiki wa Yanga aje kuchezesha mechi na gari limeandikwa daima mbele mwiko nyuma.
Yupo sahihi kwa asilimia 100% juu ya chombo chake cha usafiri.

Kuona yupo sahihi au hayupo sahihi inatofautiana na uwezo wa kutazama mambo.
 
Mtu kaegesha gari yake kwenye maegesho ya hoteli, wao yanawahusu nini?

Mbona Ulaya huko hawawaambii, wanafanya maandamano na ,mabango na magari na kila kitu, kila kukicha.

Hao mazayuni mmoja alijidai kuwasemea hovyo wasauzi kwenye maandamano yao ya kupinga mauwaji ya kimbari yanayofanywa Ghaza, kidogo wampe kichapo, polisi wakamwokoa.

Wasauzi hawataki ujinga.
Ingekuwa mpalestina kalalamika kukuta gari ya anayemuhudumia ina stika "Israiel Allah is with you not them" ungeona ni sawa?
 
Kama ni mwenye hoteli ndo hatari kabisa. Nchi inataka watalii wewe unaanzisha kampeni ambayo itahatarisha uwepo wao nchini? Bora hata awe meneja tutasema alipitiwa.
Sticker ya kwenye gari inahatarisha vipi watalii ?

Kampeni ya kuhatarisha watalii unaiweka mizania sawa na sticker katika gari binafsi la mtu ? Upo serious kweli na unachosema
 
Hayupo sahihi. Hayupo sahihi kabisa. Ni sawa na refa wa mpira shabiki wa Yanga aje kuchezesha mechi na gari limeandikwa daima mbele mwiko nyuma.
Unachanganya mifano yako unataka kuonesha Manager ana makosa wakati sio kweli.

Manager wa Hotel ni mtu mwenye Weledi mkubwa wa hiyo Biashara usitake kumfundisha hapa.
 
Ingekuwa mpalestina kalalamika kukuta gari ya anayemuhudumia ina stika "Israiel Allah is with you not them" ungeona ni sawa?
Yupo sawa hata Israel kuna waislam pia nao wanautaifa wao wa Israel hivyo ni sahihi.
 
Yupo sahihi kwa asilimia 100% juu ya chombo chake cha usafiri.

Kuona yupo sahihi au hayupo sahihi inatofautiana na uwezo wa kutazama mambo.
Hayupo sahihi. Nikuulize, ukipata kazi ya kuhudumia nyama kwa wakristo na waislamu kwenye mkutano utaenda na lile shati lako lenye picha ya nguruwe na maneno nguruwe mtamu sababu ni shati lako?
 
Unachanganya mifano yako unataka kuonesha Manager ana makosa wakati sio kweli.

Manager wa Hotel ni mtu mwenye Weledi mkubwa wa hiyo Biashara usitake kumfundisha hapa.
Huyo si meneja ni mwanaharakati wa kipalestina.
 
Kabla hata ya kuzuiwa. Kama una akili timamu utajua kuwa kuweka ujumbe huo kutafurahisha aina fulani ya watalii na kutakasirisha aina nyingine ilihali wewe unawahitaji kuhudumia watalii wote kwa usawa
Hiyo sticker katika gari binafsi ina hatarisha vipi watalii ?
 
Ukisoma source ya hiyo habari ni ‘print press news’ chombo cha nje ya nchi. Tayari inakwambia hao waisrseli wameshapeleka kadhia yao nje ya nchi.

Thanks god media outlet imekuwa fair kwenye kuandika hiyo habari kama isolated case na sio msimamo wa nchi wala hotel husika ni mtu mmoja tu.

Lakini ni damage kiasi kwa reputation ya utalii wa Zanzibar (well at least kwa wafuatiliaji wa hiyo taasisi ya habari) who knows where else hiyo habari imeandikwa na with what perspective, sio kila mtu ataandika fairly and responsibly kama huyo mwandishi wa ‘print news press’ wengine wanaweza kuza mambo.
 
Mbona unaropoka kaka??
Palestina ilikubali 1947 kugawana ardhi na Israel,je ni Palestina aliyekataa 1948 UN kuitambua kimataifa!?
1948 Mataifa makubwa yalikataa kuitambua Palestina na walikua wakimuangaisha sana Yasser Arafat.
2005 Gaza imewekewa blockade je huo sio ukandamizaji??
Ramallah kila mwaka Israel hifadhili ubomoaji wa nyumba za wapalestina ili kupanua jewish settlements je huo sio ukandamizaji??
Acheni kuropoka bhana dunia inaelewa ukweli kuwa toka 1948 Palestina iko chini ya ukandamizaji.
Wewe endelea kudanganywa.
 
Mtu kaegesha gari yake kwenye maegesho ya hoteli, wao yanawahusu nini?

Mbona Ulaya huko hawawaambii, wanafanya maandamano na ,mabango na magari na kila kitu, kila kukicha.

Hao mazayuni mmoja alijidai kuwasemea hovyo wasauzi kwenye maandamano yao ya kupinga mauwaji ya kimbari yanayofanywa Ghaza, kidogo wampe kichapo, polisi wakamwokoa.

Wasauzi hawataki ujinga.
Inawezekana wamefika hotelini wakaona gari wakafikiria kuna wanaharakati wa Hamas wamefikia hapo Hotelini, wakauliza wakaambiwa ni gari la meneja ndipo wakamueleza hofu yao na kutoridhika na hali hiyo.
 
Hayupo sahihi. Nikuulize, ukipata kazi ya kuhudumia nyama kwa wakristo na waislamu kwenye mkutano utaenda na lile shati lako lenye picha ya nguruwe na maneno nguruwe mtamu sababu ni shati lako?
Sina shati la hivyo na hata kama ninalo la hivyo shati langu halitoi huduma.
 
Zanzibar watalii wanne wa Ki Israel wametimuliwa baada ya kuleta fujo ndani ya hotel baada ya kuona gari la manager wa Hotel Hiyo Ina stika za Free Palestine

🚨🇮🇱🇵🇸 FOUR ISRAELIS were KICKED OUT OF A HOTEL in Tanzania for complaining about the "FREE PALESTINE" badge on the manager's car.
View attachment 2968844

Four Israelis were kicked out of a hotel in Tanzania for complaining about the free Palestine badge on the manager's car.

The Canary Nungwi Hotel in Zanzibar kicked out four Israelis who interrogated a receptionist about a vehicle parked outside the premise with stickers that read "Free Palestine." The Israelis were told the vehicle belonged to the manager of the hotel, and they were eventually kicked out after complaining that the vehicle was causing them "concern."
Hii haina afya kwa sekta ya utalii
 
Mtu kaegesha gari yake kwenye maegesho ya hoteli, wao yanawahusu nini?

Mbona Ulaya huko hawawaambii, wanafanya maandamano na ,mabango na magari na kila kitu, kila kukicha.

Hao mazayuni mmoja alijidai kuwasemea hovyo wasauzi kwenye maandamano yao ya kupinga mauwaji ya kimbari yanayofanywa Ghaza, kidogo wampe kichapo, polisi wakamwokoa.

Wasauzi hawataki ujinga.
Hata hivyo,hii ni habari ya upande mmoja.Bado hatujui kilichojiri hasa ni kipi.Hapa tunatoa yetu bila "washtakiwa"!
 
Zanzibar watalii wanne wa Ki Israel wametimuliwa baada ya kuleta fujo ndani ya hotel baada ya kuona gari la manager wa Hotel Hiyo Ina stika za Free Palestine

🚨🇮🇱🇵🇸 FOUR ISRAELIS were KICKED OUT OF A HOTEL in Tanzania for complaining about the "FREE PALESTINE" badge on the manager's car.
View attachment 2968844

Four Israelis were kicked out of a hotel in Tanzania for complaining about the free Palestine badge on the manager's car.

The Canary Nungwi Hotel in Zanzibar kicked out four Israelis who interrogated a receptionist about a vehicle parked outside the premise with stickers that read "Free Palestine." The Israelis were told the vehicle belonged to the manager of the hotel, and they were eventually kicked out after complaining that the vehicle was causing them "concern."
Ila hapo Unguja pana ujinga mwingi sana.
 
Back
Top Bottom